André Onana aondolewa kwenye kikosi cha Cameroon

André Onana aondolewa kwenye kikosi cha Cameroon

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Ikiwa imebaki mechi moja kwa kila group kwenye fainali za kombe la dunia hali si shwari katika kikosi na kambi ya team ya taifa ya CAMEROON baada ya mlinda mlango namba moja wa nchi hiyo kutofautina na kocha wake kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Switzerland na kufanya kocha huyo kumuondoa kwenye mipango ya michezo iliyofuata ikiwemo jana dhidi ya serbia.

Adres onana amesimamishwa kuichezea team ya taifa ya CAMEROON baada ya kocha wake rigobert song kumuacha kwenye mechi dhidi ya serbia.

Devis epassy alianza kwenye mechi dhidi ya Serbia iliyomalizika kwa sare ya goli tatu kwa kila team, huku report inadai kuondolewa kwa onana imesababishwa na mlinda mlango huyo kutokukubaliana na kocha wake juu ya style yake ya uchezaji kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Switzerland .

Wakati huo shirikisho la soka nchini CAMEROON limethibitisha taarifa hizo na kudai kwamba mlinda mlango huyo ameomba kukaa kando kwenye majukumu ya team ya taifa kwa mda usiojulikana wakati huo kocha akimuondoa kwenye kambi ya team ya taifa na chama cha soka nchini CAMEROON kimesema kipo nyuma ya maamuzi hayo na wanaungana na kocha wao kwenye hilo.

Kwenye mechi dhidi ya uswis onana alikuwa na touches (26) nje ya box lake mara ya mwisho kwa mlinda mlango kufanya hivyo ilikuwa ni mwaka 1996.

Wakati sakata hilo likiendelea onana amekiri hawezi kuacha style yake hiyo ya uchezaji kwani ndio walinda mlango wa kisasa wanavyotakiwa kucheza huku akisisitiza samir handanovic ndio kocha wake anayemfindisha aina hyo na neur ndio role model wake katika aina hiyo mpya ya uchezaji wa kisasa kwa walinda mlango.

20221129_115118.jpg
 
Hii ndio style ya yule mdaka mishale wa utopolo..
Ila sijui kwanini ukitofautiana na kocha inakuwa imekula kwako wewe mchezaji
 
Soka letu kivyetu vyetu
FB_IMG_16697170430261300.jpg
 
Gk ameonesha ujinga, inabidi atambue walimu wanatofautiana approach, hivyo mchezaji aingie kwenye mfumo, sio mfumo uingie kwa mchezaji. Very good kocha.
 
Onana ni mpumbavu, kuna namna angekaa na kuongea na kocha wake na sio kumkosoa wazi wazi, makocha wengi wanapokea ushauri wa wachezaji, hilo moja.

Pili, onana ajue mchezaji bora ni yule anaecheza kwa maelezo ya mwalimu, kwakuwa unafundishwa na guardiola ndio unataka kwa mourinho ucheze hivyo hivyo utaigharimu timu. Kuna watu club wanacheza beki national team ni midfielder. Mchezaji cheza kama kocha atakavyo ukienda toffauti unaharibu mipango yake.
 
Mechi ya Kwanza hawa jamaa niliona viazi kweli , et mtu anang'ang'ana kupiga shuti mwenyewe wakat pembeni yake mwenzakeyupo tuu yeye na kipa na yupo onside , mara mbili kabisa , wenzao walipota chance waliwanyoosha, rigobert song ni Mfa maji
 
Onana ni mpumbavu, kuna namna angekaa na kuongea na kocha wake na sio kumkosoa wazi wazi, makocha wengi wanapokea ushauri wa wachezaji, hilo moja.

Pili, onana ajue mchezaji bora ni yule anaecheza kwa maelezo ya mwalimu, kwakuwa unafundishwa na guardiola ndio unataka kwa mourinho ucheze hivyo hivyo utaigharimu timu. Kuna watu club wanacheza beki national team ni midfielder. Mchezaji cheza kama kocha atakavyo ukienda toffauti unaharibu mipango yake.
Ni kweli kabisa kwa mfano rodri Guardiola anamchezesha central midfielder ila Spain anacheza centre back ila hoja ya onana ni kwamba CAMEROON hawana watu hao wa system anayoitaka kocha wao wakupiga long balls yaani mfumo hauendani na wachezaji sasa kuliko onana kubeba lawama za kufungwa open goal bora ajitoe kabla hayajatokea ya kutokea.
 
Kutofautiana na kutukana ni vitu viwili tofauti mkuu.. halafu kwenye timu sio jeshini ambapo ni utii tu bila kuhoji

Mwafrika hajui kutofautiana ni jambo la lawaida na muhimu wakati mwingine.
Tukiwa na mawazo yanayofanana huo ni upopoma sasa
 
Back
Top Bottom