Andres Iniesta 'The Magician' kuondoka Barcelona mwisho wa Msimu huu. Je, utamkumbuka kwa lipi?

Andres Iniesta 'The Magician' kuondoka Barcelona mwisho wa Msimu huu. Je, utamkumbuka kwa lipi?

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kiungo mchezeshaji wa klabu ya Soka ya Barcelona, Andres Iniesta(33) ametangaza kuondoka klabuni hapo ifikapo mwisho wa msimu huu 2017/18

IMG_20180427_190655_409.jpg


Kiungo huyo raia wa Uhispania aliyeichezea klabu hiyo kwa miaka 22 na kushinda mataji 31 amesema hataweza kucheza dhidi ya Barcelona atakapoondoka klabuni hapo

Iniesta maarufu kama 'Magician' ni mchezaje pekee kuwahi kuwa mchezaji bora(Man of the match) katika fainali ya EUROs, fainali ya Kombe la Dunia na fainali ya Klabu Bingwa Ulaya

IMG_20180427_185643.jpg


Aidha, Iniesta amecheza misimu 16 na kuifungia klabu hiyo ya Barcelona magoli 57 ikiwemo magoli mawili ambayo hayawezi kusahaulika kwa mashabiki wa Barcelona(Kombe la Dunia dhidi ya Nertherland, 2010 na dhidi ya Chelsea katika dakika za nyongeza kwenye michuano ya Klabu bingwa Ulaya, 2009) na kucheza mechi 669

IMG_20180427_184704.jpg


Je, mwanasoka utamkumbuka Iniesta kwa lipi wakati akiwa Barcelona
 
Kama mchang’ombe Shafii Dauda anavyo chambua..... naseemaaa Booooongeee la Player. Nimemaliza kuchambua.
 
Zaidi kwa lile goli alikuwa funga chelshit ktk dimba lao la Stamford bridge
 
Aisee muda unaenda kasi sana yani Iniesta umri umeshamtupa mkono?
 
Namkumbuka babu yangu kwa mengi sana, alikuwa anaenda kunywa gongo upande wa pili wa barabara kwa miaka 37 bila kugongwa, Pamoja na kuwa njwiiiiiii lakini barabarani anavuka.
 
Fundi ambae anauwezo wa kubadilisha mchezo anaweza kuamua mchezo uwe na kasi au uwe slow n yeye peke yake

Katka match iniesta yupo uwanjan sahau kuwa man of the match, labda tu itokee lakn sahau kabisa

Akiwa katka kutafuta ushind, anachukua pass kwa players wote lakn yeye humpasia messi tu( game ya juz barca walipokua ugenin kwa Chelsea goal anachomoa messi)

Kiungo ambae kamkosesha raha modric kwa muda mrefu sana,

Kiuongo ambae katka ubora wake hauchukui mpira mguuni kwake, labda kwa rafu

Iniesta mpira utam-miss sana, ila clip zake zitabak miaka buku
 
Back
Top Bottom