View: https://www.youtube.com/live/h9cHr7NLIBA?si=L-nYOeceS1NrpmnVKasoro kubwa katika interview hii ya leo katika kipindi cha hiki cha 360° Clouds TV:
1. Ni mtangazaji huyu wa kike (Kijakazi Yunus) kutokuwa makini ktk kazi yake. Angalia alivyokaa, anachofanya, anauliza swali na haoneshi umakini wowote ktk kusikiliza na matokeo yake maswali nyongeza (follow up questions) kutoka kwake ktk interview hii kuwa "very vague" kuonesha kuwa hafuatilii majibu ya maswali aliyouliza mwenyewe...
2. Ni wazi kuwa hakujiandaa kwenda kufanya mahojiano na mtu wa aina ya Tundu Lissu ambaye naweza kusema hamjui vizuri au alidhani anajua zaidi kuliko yeye...
3. Hili #2 hapo juu inathibitishwa na kukosa kwake umakini kiasi cha maswali yake kuwa ya shaghala-baghala kwa sababu hasikilizi majibu yake toka kwa anayemuuliza maswali. Ikafika time anamtaka mfanyiwa mahojiano aanze kumhoji mtangazaji...!!
4. Ilifika wakati Tundu Lissu (mhojiwa) kumrejesha mtangazaji kwenye mstari na kumwambia "kuwa makini, Fuatilia logic ya maelezo yangu..."
5. Kwa maoni yangu huyu Mtangazaji (Dada Kija), hafai kuongoza kipindi cha kuhojiana na watu wenye akili na ufahamu mkubwa kama Tundu Lissu badala yake ahojiane na waimba taarabu na miziki ya mipasho huko...!!
CC: @CloudsTV