GE2025 Angalia Citizen TV kuna hot debate about "Tanzania and its Samia"

GE2025 Angalia Citizen TV kuna hot debate about "Tanzania and its Samia"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa sababu utekaji na mauaji yapo kwao basi ni sawa tuu na hawatuzidi kitu? Kwa akili hizi tuna safari ndefu sana kama Taifa
Je umekwishatoka kuandamana? Au unasubiri waandamane wengine ndiyo uje kuandika humu JF? Key board warrior wahedi
 
29 October 2025

Dakika 30 zilizopita, 5,619View

Vyombo vya media nje ya Tanzania vinavyo ripoti waandamanaji wangoa mabango yenye picha za mgombea urais wa CCM ndugu Samia Suluhu Hassan yaliyotapakaa barabara kuu na ....

Tanzanians Destroy Polling Stations and President Samia's BillBoards!​


View: https://m.youtube.com/watch?v=z86jCyTmgko
 
Vyombo huru visivyo na minyororo ya katazo la kidola vya nje vinaripoti na kutafsiri wanachokiona leo tarehe 29 October 2025

Breaking News! Tanzania Military TAKESOVER the Streets JOINS Massive Demonstration!


View: https://m.youtube.com/watch?v=fxF2NZ4OAPg


TOKA MAKTABA:

DAWATI LA SOMO LA HISTORIA

Mtego mbaya wa serikali kujaribu kutumia jeshi la ulinzi wa taifa kisha likawageuka watawala wa chama dola kongwe kilichotaka kubaki madarakani kwa ubabe

TOKA MAKTABA :


Katika mahojiano exclusive Luteni Mwamba Luchembe anafunguka miaka mingi baadaye nini kilimsukuma kuvamia studio za Shirika la Habari la Zambia ZBC mwaka 1990 kutangaza mapinduzi ya kungoa serikali ya chama dola UNIP iliyokuwa inaongozwa na Rais Kenneth Kaunda baba wa taifa hilo.


27 May 2022
Luteni Mwamba Luchembe, Tuliitwa kusaidia polisi walioshindwa kuzima maandamano

View: https://m.youtube.com/watch?v=yY6JDPWaHuY
Former Zambian army officer Mwamba Luchembe reflects on the day he tried to overthrow Kenneth Kaunda in a military coup. (This interview was recorded while PF were in power and Kenneth Kaunda was still alive.)
Tulikuwa katika kambi yetu kilometa 500 kutoka mji mkuu wa taifa la Zambia, jiji la Lusaka.

1990 hali ya kisiasa na kiuchumi ilikuwa mbaya, wananchi walikuwa na manunguniko mengi ikiwemo ugumu wa maisha, ughali wa bidhaa muhimu kama unga wa sembe, ukandamizaji wa kisiasa uliokuwa unafanywa na chama dola kongwe kimoja UNIP

Maandamano yakatokea jeshi la Polisi likatumwa kudhibiti mandamano hayo lakini wakazidiwa na nguvu ya umma uliojitokeza .

Rais Kaunda akatoa amri jeshi la ulinzi la Zambia watoke kambini kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Hivyo mimi nilikuwa katika Battalion 5 Kaoma, nasi tukapewa amri tuende Lusaka kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Wakati tukiwa mesi tunakula chakula cha jeshi ambacho hatulipii, mawazo yetu yakaguswa na madhila ya wananchi wasiokuwa na uwezo wa kula ambao walijitokeza kwa wingi kuandamana huku sisi tukila chakula kwa uhakika kupitia kodi zao.

Hivyo tukaona nchi inaenda kubaya kutokana na kuwa na chama kimoja kongwe tawala kilichoishiwa mawazo ya kutanzua changamoto za raia.

Wazo letu likawa kuchukua nchi na kuiongoza kwa miezi sita huku tukijenga mazingira vyama angalau vitatu makini viundwe ili demokrasia iwepo nchini. Hatukutaka kuona vyama zaidi ya vitatu maana tunajua vyama vingine ni vya mfukoni ( briefcase) siyo vyama vya ukweli vya mawazo mbadala

Tukiamini demokrasia ya uwazi, uchaguzi huru, bunge makini vingeweza kuiondoa nchi ktk changamoto iliyokuwa nchi inapitia ...

Ndiyo maana niliongoza platoon iliyokuwa na wanajeshi 32 huku mimi ni kiwa ofisa wao hivyo jumla ya wanajeshi 33 tulivamia kituo cha taifa cha ZBC nami nikatoa tangazo la serikali kupinduliwa...

Tulikuwa tumekubaliana na kambi zingine za Kitwe, Mufulira n.k nao waingie ktk sehemu nyeti za utawala wa kiserikali ktk majimbo ili kukamilisha mapinduzi hayo...

Wananchi walijitokeza kwa wingi mtaani kufurahia tangazo la mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo wenzetu tuliokubaliana kuikamilisha kazi hivyo kote nchini walitugeuka.

Akatumwa askari mmoja mwandamizi atushawishi kuwa mapinduzi yetu hayakufanikiwa.

Nilikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha Central police nikafungiwa katika mahabusu upande wa wanawake, na wale mahabusu wote wanawake kwanza walihamishwa.

Wakaja wanajeshi wa idara ya utambuzi, maofisa wa usalama wa taifa na wa vyombo vingine kunihoji kwa muda wa wiki moja ktk selo hiyo ya wanawake.

Baada ya hapo walinipakiza ktk helicopter tukaelekea katika kambi nilitotokea iliyopo kilometa 500 kutoka Lusaka. Wakafanya upekuzi katika ofisi nikiyokuwa natumia kambini na katika nyumba niliyokuwa naishi kambini.

Wakanirejesha Lusaka hata hivyo usiku ulikuwa umeanza kuingia hivyo rubani wa helicopter akazima mawasiliano yote na kutua eneo mojawapo kwani rubani alitoa taarifa ya kuwa helicopter haina uwezo wa kusafiri usiku wa giza kufika Lusaka. Walizima mawasiliano ili kama kuna njama za wenzangu kuja kuniokoa zisifanikiwe.

Alfajiri na mapema tukamalizia safari yetu kwa usafiri wa barabara hii yote ikiwa ni njia ya medani, kwa waliopanga nami kufanya mapinduzi wasijue nilipo wala nini kimetokea kwangu mimi.

Mahojiano yakaendelea mjini Lusaka ktk nyumba maalum (safe house) kujaribu kupata habari zote za Mapinduzi na wahusika wote katika njama hii ya kupindua nchi.

Walitumia koleo / pliers kutoa meno yangu kavukavu bila ganzi, lakini situwasaliti wala kutaja wenzangu waliotayarisha jaribio la kuangusha serikali.

Baada ya kunisulubu hivyo, wakanirudisha kwa kificho kituo kikuu cha Polisi huku nikiwa na maumivu makali. Wakanipandisha ghorofani, watu wa Idara ya Usalama na wale wa Idara ya Utambuzi jeshini wakapanga mipango watawaambia nini raia hata polisi na wanajeshi watakaoniona.

Hivyo basi wakanivua nguo zote tukiwa ghorofani na kuzitupa kupitia dirishani. Kutoka juu ghorofani wakanitelemsha mzobemzobe mbiombio uchi wa mnyama nikiwa mtupu, kisha wale wote walikuwapo kituo kikuu cha Polisi wakanishangaa si polisi, raia na waandishi wa habari hata wapita njia wakabaki wanajiuliza kulikoni..

Watu wa Idara na Vyombo wakasema huyu ni kichaa aliyewehuka siku nyingi kabla ya mapinduzi, faili lipo jeshini na kwa vile alikunya sana Pombe na bangi ndiyo maana akatimka kwenda, kutangaza mapinduzi yale.


Baada ya miezi miwili nikastaafishwa jeshi kwa sababu za 'kiafya' yaani ugonjwa wa akili. Hata hivyo vyombo vya usalama vikamwambia rais pamoja na hii hadaa tuliyoitengeneza ukweli watu wanataka na wanaamini mabadiliko ya kuleta vyama vingi vya kisiasa. Hivyo ni bora rais aanzishe mchakato wa mabadiliko ya katiiba kuruhusu na kuafiki kwa moyo mkunjufu vyama vingi, demokrasia na uchaguzi huru kupitia tume huru ya uchaguzi.

Hivyo mwaka 1991 mchakato wa vyama vingi na katiba mpya vikapitishwa na bunge la Zambia kwa usimamizi wa karibu wa rais Kenneth Kaunda.

Mapinduzi yale yaliyoshindwa hata hivyo yalileta jambo chanya kuwa watu wanataka mfumo wa vyama vingi, yalionesha kuwa ukiritimba wa chama dola kongwe cha UNIP na rais nguvu yao ya ushawishi wa chama kimoja umepungua na wajitayarishe kuwa chama cha upinzani.

Kwa ujasiri wa Luteni Mwamba Luchembe kuongoza jaribio la mapinduzi , sasa anahesabika kama baba wa mabadiliko / reforms za kupatikana katiba mpya na demokrasia ya vyama vingi nchini Zambia.

Katika mitaala vya masomo ya uraia / civic Luteni Mwamba Luchembe anatokea ktk vitabu mashuleni kuwa alikuwa chachu ya mabadiliko yaliyoleta vyama vingi kuruhusiwa nchini Zambia.

Mbali ya watoto wa shule kusomeshwa mchango wake Luteni Mwamba Luchembe kuleta mabadiliko, sasa katika Makumbusho ya Taifa mjini Lusaka na makumbusho ya majimbo mbalimbali nchini Zambia picha yake ipo miongoni mwa watu waliotoa mchango kwa taifa la Zambia hadi kufikia lililopo sasa.

Rais Frederick Chiluba aliposhinda uchaguzi wa vyama vingi kupitia chama cha upinzani alimrejesha Luteni Mwamba Luchembe kazini na kumpa cheo mserereko hadi kuwa Captain kisha kumstaafisha kwa kumpatia pensheni stahiki ya cheo alichofikia.

Source :
 
Shida yote hiyo ya nini kuangalia Citizen TV ya Kenya.??

Kwani nchini kwao kuna nini wanachotuzidi? Kama ni demokrasia na katiba nzuri wanayo, lakini hawana tofauti na kinachotokea kwetu.

Utekaji upo, uuaji upo na bado siyo rahisi kwa mtu yeyote kugombea urais wa Kenya. Lazima utoke kwenye circles zenye nguvu ya hela na kabila maarufu
Angalao wana freedom of speech
 
Hii debate aisee inakufanya uone jinsi tulivyo na viongozi wabovu sana
 
29 October 2025

No Election in Tanzania 2025, It Is A Coronation

The Next 7 Days Could Change Tanzania Forever- Here's Why


View: https://m.youtube.com/watch?v=heb8BeuSUcs

 


TOKA MAKTABA :

27 July 2025
Gauteng, Republic of South Africa

KULINDALI MAFANIKIO YA VYAMA VYA UKOMBOZI BAADA YA UHURU, VINAENDANA NA HAJA YA VYAMA HIVYO KUBAKI MADARAKANI

Kigogo wa CCM waziri mkuu mstaafu komradi Mizengo Kayanda Peter Pinda ameongoza msafara mzito kwenda kuhudhuria mkutano wa vyama vilivyoleta ukombozi / uhuru ambavyo kwa sasa viko chini ya tishio la kuondolewa madarakani baada ya kushindwa kutatua matatizo yanayokumba raia katika nchi zao

African National Congress (ANC) itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kilele cha Vyama vya Ukombozi 2025 katika Hoteli ya Radison Blu, Kempton Park kuanzia leo tarehe 25 hadi 28 Julai 2025 chini ya mada: "Kulinda Mafanikio ya Ukombozi, Kuendeleza Maendeleo Jumuishi ya Kijamii na Kiuchumi, Kuimarisha Mshikamano wa Afrika."

Mkutano huu muhimu unathibitisha misingi ya kiitikadi ya vyama sita vya ukombozi Kusini mwa Afrika - ANC, MPLA, SWAPO, FRELIMO, ZANU-PF na CCM - na jukumu lao la kihistoria katika kupata uhuru, utu na maendeleo katika eneo lote la Kusini mwa Afrika.

Pia Kongamano linalenga kusisitiza umuhimu wa harakati hizi kuwa katika mpangilio unaotambua mabadiliko ya mazingira ya kisiasa na kimataifa yanayobadilika haraka.

Vyama vya ukombozi vya Kusini mwa Afrika vilibadilisha hali ya kisiasa ya eneo hilo, kupinga utawala wa kikoloni na ubaguzi wa rangi, na kukaribisha utawala unaozingatia watu.

Tangu uhuru, vuguvugu hizi zimetekeleza sera muhimu kuhusu mageuzi ya ardhi, elimu, makazi, miundombinu na ulinzi wa kijamii.

Hata hivyo, mafanikio haya sasa yanakabiliwa kumegeka kutokana shinikizo jipya la mataifa ya kibeberu, migogoro ya kiuchumi, na majaribio ya kuingiliwa na ukoloni mamboleo.

Mkutano huu unatoa jukwaa moja la kukabiliana na matishio haya na kujumuisha majibu ya kimaendeleo ya kikanda yanayokitwa katika Pan-Africanism (Umajimuhi wa Kiafrika), internationalism na multilateralism.

Mkutano huo ni uingiliaji wa kimkakati katika uanzishaji upya wa mpango kazi (framework), kuimarisha mshikamano wa ndani ya chama, na kurekebisha harakati za ukombozi na matarajio ya kijamii na kiuchumi ya kizazi kipya.

ANC inaamini kwamba uhai wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni wa urithi wa ukombozi wa Kusini mwa Afrika unahitaji kuchunguzwa kwa uaminifu, ukweli, kujifunza kwa pamoja na umoja unaoweza kutekelezeka.
Mkutano huo utaendeleza mifumo ya ushirikiano kati ya vyama, ushirikiano wa kikanda, ushirikishwaji wa vijana, na utawala huru wa rasilimali.

Kupitia kuthibitisha tena maadili ya pamoja na kuimarisha ushirikiano, Kongamano la Vyama la Ukombozi 2025 utapanga njia mpya ya kusonga mbele, ambayo inalinda mafanikio ya zamani huku ikijenga mustakabali wa Afrika wenye haki, jumuishi na unaojiamulia.

Vyombo vya habari vinashauriwa kuzingatia yafuatayo:
Wajumbe wameanza kuwasili leo, Alhamisi, tarehe 24 Julai 2025 na Wakuu wengi wa Wajumbe watawasili kesho Ijumaa, tarehe 25 Julai 2025. Watatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Reginald Tambo, Wanaowasili Kimataifa,.

Wakuu wa Ujumbe :

  • Cde. Mizengo Kayanza Pinda, Head of Delegation, CCM, Tanzania
  • Cde. Chakil Aboobacar, Katibu Mkuu, FRELIMO, Msumbiji
  • Cde. Mara Baptista Quiosa, Naibu Rais, MPLA
  • Cde. Sophia Shaningwa, Katibu Mkuu, SWAPO
  • Cde. Obert Mpofu, Katibu Mkuu wa ZANU-PF
  • Cde. Liu Jianchao, Kamati Kuu ya CPC (IDCPC), Chama cha Kikomunisti cha China (CPC)
  • Cde. Mohamed Yeslem Beisat, Mkuu wa Ujumbe, Polisario Front
  • Cde. Jibril Rajoub, Katibu Mkuu, Harakati ya Ukombozi wa Kitaifa ya Palestina - FATAH
  • Cde. Solly Phetoe, Katibu Mkuu wa COSATU
  • Cde. Solly Afrika Mapaila, Katibu Mkuu, SACP
  • Cde. Mike Soko, Katibu Mkuu wa SANCO
  • Cde. Apa Poe, Katibu Mkuu, PAC
The African National Congress (ANC) will host the 2025 Liberation Movements Summit at the Radison Blu Hotel, Kempton Park from the 25th to 28th of July 2025 under the theme: “Defending the Liberation Gains, Advancing Integrated Socio-Economic Development, Strengthening Solidarity for a Better Africa.”
Source : https://www.anc1912.org.za/liberati...ng-the-gains-confronting-the-future-together/
 
KULINDALI MAFANIKIO YA VYAMA VYA UKOMBOZI BAADA YA UHURU, VINAENDANA NA HAJA YA VYAMA HIVYO KUBAKI MADARAKANI
Toka maktaba :

Mahojiano na Prof. P.A.N Mihanjo kuhusu hali ya kisiasa nchini.

Prof. Eginald P.A.N. Mihanjo. PhD, MA in History, BA (Hon.) Educ. (UDSM) amewahi kuwa Kaimu Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu, Mhadhiri mwandamizi ndani na nje ya nchi, Mkurugenzi wa mafunzo wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC kinachotoa mafunzo ya usalama -stratejia- ulinzi, mhadhiri Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Msumbiji Foreign Relation Kurasini.. pia ni mtaalamu wa Usalama, Ulinzi, Usuluhishi wa Migogoro kimataifa na kikanda ..

 
Back
Top Bottom