Mkuu niliogopa kumvunja moyo kijana maana nilitaka nimwambia kwa ufaulu ule ni aombe kwenda vyuo vya utabibu yaani Clinical Officers. Ila kwa ufaulu wa kidato cha 6 Science mwajka 2023 hata Div I zitaenda vyuo vya chini tu. Maana mwaka huu nina imani MD Muhimbili PCB watachukua point 3. Point 4 itbidi waweke na kigezo kingine kama A ya BAM ili kupunguza competition kwa kuondoa wale wanaopata BAM C,D,E. japo wanazo point kali. Enzi zetu kupata point 3 si mchezo kabisa, yaani ile Div I ya masomo kama PCB, PCBM, PGM, CBG, haikuwa mchezo kabisa.