Angalia jela hiyo ughaibuni

Angalia jela hiyo ughaibuni

Inaitwa Justice Center Leoben, iko Austria ni jengo ambalo lina mahakama pamoja na jela. Aliyeli -design architect anaitwa Josef Hohenssin likakamilika 2005.

Lina uwezo wa kuweka wafungwa 205 na limejaa wafungwa 205 lengo la kujengwa gereza zuri hivyo ni kusimamia Kwa vitendo na kuonyesha kwamba kila binadamu ana Haki Sawa, amezaliwa huru na anapaswa atendewe Kwa heshima.

View attachment 2957511View attachment 2957512
Nendeni Austria mkafanye uhalifu mfungwe huko ndio mtajua nini maana ya jela.
 
Inaitwa Justice Center Leoben, iko Austria ni jengo ambalo lina mahakama pamoja na jela. Aliyeli -design architect anaitwa Josef Hohenssin likakamilika 2005.

Lina uwezo wa kuweka wafungwa 205 na limejaa wafungwa 205 lengo la kujengwa gereza zuri hivyo ni kusimamia Kwa vitendo na kuonyesha kwamba kila binadamu ana Haki Sawa, amezaliwa huru na anapaswa atendewe Kwa heshima.

View attachment 2957511View attachment 2957512
unaitamaniee:Haram:
 
Huko netherland jela zilifungwa karibia zote,maana zilikosa wahalifu,wakazikarabati vizuri na kuzitafutia mpangaji,yaani kama jela zako zimejaa unakodisha jela moja huko na kuwaweka wafungwa wako kwa makubaliano, nchi ilisikitika kuwa askari magereza wanaenda kupoteza kazi (siyo vibarua) wengi walitamani magereza zao ziwe active,ila utamfunga nani? Kwa nini?
 
Jengo zuri ila huko ndani unakutana na watu wamepinda na kuna utawala wa muhalifu mwenye nguvu kifedha.
Ukiwa mzembe mzembe unakua mke wa mtu, movie nyingi tunazoangalia zina reflect uhalisia wa jela za huko .
 
Mkinipa uhakika wa kufungwa hapo na-overtake msafara wa rais nauchomekea kwa bodaboda.
 
Kwao jela sio sehemu ya mateso Bali kukubadilisha tabia na mwenendo wako ila huku kwetu jela ni sehemu ya kuadhibiwa.
 
Back
Top Bottom