Ushauri ni kuwa,
kwanza kozi baada ya lenta zinatakiwa ziongezeke ili kupata slope kubwa ya bati kuzuia bati kuoza haraka na kuvuja.
Pili inabidi kuwe na vent kwenye ukuta wa juu kuweka mzunguko wa hewa na kulinda gypsum board isivimbe au kuharibika mapema.
Tatu ongeza upana wa kibaraza na canopy yake ili nyumba ionekane ni kubwa unaweza kudhani una sebule mbili, moja ya ndani nyingine ya nje.
Nne upande ambao hauonekani kushoto inaonekana hakuna canopy lakini kutakuwa na dirisha, sasa mvua itasumbua kuingia ndani kama hakuna kikinga mvua upande huo.
Tano, kibongobongo bila grill work madirishani usalama ni mdogo.
Sita zungusha boundary ya tiles au Tangastone kulinda msingi wa nyumba dhidi ya mimea ambayo mizizi yake itapenya na kudhoofisha msingi. Pia inongeza convinience kutembea nyuma ya nyumba kuifanyia usafi, ukaguzi na ukarabati.