MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Kama ambavyo tunaona matangazo yanayotolewa na mabenki kushusha riba za mikopo kutokana na maelekezo ya BOT ili kuleta nafuu kwa wakopaji.
Hili la riba imekuwa ni juhudi binafsi za Mh Rais John Pombe Magufuli ambaye toka wakati wa kampeni alioneshwa kukerwa na riba za ajabu tulizonazo hapa nchini. Hivyo kuanza kutekeleza hili tunapaswa kiungwana kumpongeza mkuu wa nchi kama tunavyomkosoa pia akikosea.
Angalizo muhimu kwa BOT ni kuhakikisha system au njia inayotumika kukokotoa riba iwe standard kwa taasisi zote isipokuwa pale inapompa unafuu mkopaji.
Kukokotoa riba kwa kutumia straight line method ni mzigo maana makato hayapungui hadi muda wa mkopo unapofika mwisho wakati reducing balance inasaidia kuona unafuu kadri unavyolipa.
Asilimia kubwa ya wafanyakazi wana mikopo hivyo kushuka kwa riba kutaleta unafuu mkubwa sana wa maisha. Riba zilishafika 25% and above lakini kurudi hadi below 17% si punguzo dogo.
Mikopo nafuu ndio njia pekee ya kukomboa wananchi na kusaidia kuboost mzunguko wa pesa. Ni matarajio punguzo hili litawagusa pia wenye mikopo ili impact ya mabadiliko iwe kubwa na ya haraka zaidi.
Wafanyakazi wengi walichukua mikopo ili kupata basic needs na si uwekezaji hivyo riba kubwa kwa mishahara midogo imewageuza kuwa watumwa na kuchangia ufisadi hasa kwa maafisa wadogo.
Pongezi kwa BOT na Mh Rais kwa hatua hii kubwa itayogusa mifuko ya wananchi moja kwa moja kama utekelezaji wake utasimamiwa vizuri ili kuleta matokeo yanayotarajiwa.