Angalizo kwa BOT baada ya riba za mikopo kuanza kushuka

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Kama ambavyo tunaona matangazo yanayotolewa na mabenki kushusha riba za mikopo kutokana na maelekezo ya BOT ili kuleta nafuu kwa wakopaji.

Hili la riba imekuwa ni juhudi binafsi za Mh Rais John Pombe Magufuli ambaye toka wakati wa kampeni alioneshwa kukerwa na riba za ajabu tulizonazo hapa nchini. Hivyo kuanza kutekeleza hili tunapaswa kiungwana kumpongeza mkuu wa nchi kama tunavyomkosoa pia akikosea.

Angalizo muhimu kwa BOT ni kuhakikisha system au njia inayotumika kukokotoa riba iwe standard kwa taasisi zote isipokuwa pale inapompa unafuu mkopaji.

Kukokotoa riba kwa kutumia straight line method ni mzigo maana makato hayapungui hadi muda wa mkopo unapofika mwisho wakati reducing balance inasaidia kuona unafuu kadri unavyolipa.

Asilimia kubwa ya wafanyakazi wana mikopo hivyo kushuka kwa riba kutaleta unafuu mkubwa sana wa maisha. Riba zilishafika 25% and above lakini kurudi hadi below 17% si punguzo dogo.

Mikopo nafuu ndio njia pekee ya kukomboa wananchi na kusaidia kuboost mzunguko wa pesa. Ni matarajio punguzo hili litawagusa pia wenye mikopo ili impact ya mabadiliko iwe kubwa na ya haraka zaidi.

Wafanyakazi wengi walichukua mikopo ili kupata basic needs na si uwekezaji hivyo riba kubwa kwa mishahara midogo imewageuza kuwa watumwa na kuchangia ufisadi hasa kwa maafisa wadogo.

Pongezi kwa BOT na Mh Rais kwa hatua hii kubwa itayogusa mifuko ya wananchi moja kwa moja kama utekelezaji wake utasimamiwa vizuri ili kuleta matokeo yanayotarajiwa.
 
Safi sana mleta hoja ana hoja nzuri...hongera Mheshmiwa Rais Dr. JPM na serikali ya awamu ya tano kwa kuliona ili tatizo la riba kubwa kwa mikopo hususani kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa kipato cha chini
 
Mimi nashauri JF waweke sticky thread maalum kwa ajili ya pongezi kwa Magufuli ili wapenda kupongeza muwe mnajimwaga huko 24 hours kupongeza.

Ni upuuzi kudhani kila mtu ana akili ndogo kama yako.

 
Mleta mda Najua Upo Vema kwenye mambo ya Uhasibu na Uchumi....hongera sana sana
Natamani Serikali Ilifanyie haraka hili Tangazo,Hoja yako hasa Kutumia Formula/Kikokotozi/Mfumo wa Aina moja kwa mabank ambayo ni Reducing Balance ili kuleta Unafuu kwa Mkopaji....ikiwezekana Hili Suala lianze Mapema/Haraka Iwezekanavyo!
Big up MTAZAMO!
 
Hajui lolote huyo, riba bafo ni kubwa sana, nadhani tatizo la Wabongo wengi ni exposure hamjui duniani bank za wenzetu zinatowa vipi huduma hasa riba zao.

Islamic bank wameonesha mfano hai ni vitu vinawezekana kukopesha bila kutoza riba mzigo.
 
Hakuna lolote la kumpongeza Rais na Serikali kwenye hili jambo..

Ni maagizo mangapi yanatolewa na Rais au Serikali kwa Taasisi au makundi ya watu mbalimbali na HAYATEKELEZWI..??

Mfano bei ya sukari, mbona maagizo kibao yameshatolewa kwa bidhaa hii bei iwe sio zaidi ya 2200/kg na mbona ipo juu zaidi mpaka 3000/kg??

Ni hivi. .
Mabenki wameona hali halisi ya Uchumi ulivyo ndio maana yameamua kushusha viwango vya RIBA kwenye mikopo.

Banks zinajiendesha kwa faida kupitia MIKOPO na si zaidi ya hapo..

Wameona kuendelea kung'ang'ania riba kubwa za 25%+ kwa hali ya Uchumi uliodorora wa Tanzania, Benki zitakuja ku collapse kabisa..

Hali ya Benki nyingi ni mbaya..mbaya kweli kweli na they had no alternative except kupunguza riba kwa wakopaji..

Kushuka kwa Riba za Banks ni " Economic Variables" ndio main determinant factor na sio maombi ya Rais au BOT.

Toa sifa panapostahili na sio kusifia UONGO, eti juhudi za Mh Rais..
NO.
 
hapa ndo unajua uongo wa mabenki watu wanatoka kwenye riba ya reducing wanakuambia wameshusha kumbe ipo pale pale ila kwasababu wanatumia flat rate inakufanya uone riba ndogo machoni, halafu riba kushuka sio ombi la raisi wala maneno ya mtu ni economic variables ndo zinaamua, deposit inchi maskini ni very expensive pia gharama za kuendesha biashara zipo juu sana ndo maana riba zipo juu. Hii shuka riba ina ulaghai mkubwa ndani yake maana inashuka machoni kwa mteja na wala si kwenye mkopo
 
ni kweli apongezwe.
ila tusisahau kurudi hapa tena kumpongeza atakapo print notes mpya kwa wingi.
dalili zi wazi!
 
Hajui lolote huyo, riba bafo ni kubwa sana, nadhani tatizo la Wabongo wengi ni exposure hamjui duniani bank za wenzetu zinatowa vipi huduma hasa riba zao.

Islamic bank wameonesha mfano hai ni vitu vinawezekana kukopesha bila kutoza riba mzigo.
Islamic banking unawapa hisa kwenye biadhara yako uliyoanzisha kwa mkopo wao dhamana Mali zako na faida ya Kila mwaka mnagawana na benki kwa ratio ya share ukipiga hesabu riba yaani faida mnayogawana Ni kubwa kuliko riba ndio maana wengi hawachangamkii.Riba Ni faida mnayogawana sema jina ndio tofauti.Lakini Ni riba
 
Peleka ULumumba wako huko. Hoja yako ni nzuri tatizo umeingiza siasa. Rais hana mamlaka ya kuzipangia benki riba... wadanganye wenzako CCM, not others! Rais anajua operating costs za mabenki? acha kumpamba!
 

Mkuu hili linalofanyika na mabank kupunguza riba halitasaidia , kupunguza riba kuendane na serikali kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara, kupunguza riba huku biashara nyingi zimefungwa inamsaidia nani?
 
Kama ni juhudi Za Raisi basi hili swala lipo kisiasa zaidi kuliko uhalisia.

Mabenki yangejikita kutangaza mikopo mipya kwa riba ndogo ningewaelewa.

Hizi zingine ni mbwembwe tu za kufurahisha kiti.
 
Hakuna cha declining interesting wala flat rate interesting vyote ni uwizi tu tatizo letu akili zinawaza kupata mkopo kwanza na sio kujua wewe utalipa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…