Yaliyojiri katika hafla hiyo ya mapokezi ya ndege hii
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda: ''Wabunge wa Majimbo ya Kawe, Kibamba na Ubungo ni wezi wanaokula posho bungeni bila kufanya kazi kwa wananchi'' Asema mwaka 2015 walifanya makosa kuruhusu watu hawa kuwa wabunge.
''Wilaya ya Ubungo ina wabunge wawili na ina Meya wa Upinzani; nakuomba Mhe. Rais unisaidie niwajengee hospitali ya Wilaya wanaUbungo''
Naye Kaimu Balozi wa Marekani, Dkt. Inmi Patterson, akitumia lugha ya Kiswahili amewapongeza Watanzania na Shirika la ATCL kwa kununua ndege mpya ya pili aina ya Boeing B787-8. Asema, kukua kwa safari za anga kutakuza biashara na utalii.
Ufuatao ni mukhtasari wa sehemu ya hotuba fupi ya Rais Magufuli:
''Naambiwa hapa kuna Mabalozi na Wawakilishi zaidi ya 30. Waswahili wanasema ukitaka kwenda safari ndefu lazima uanze na fupi. Tulipoanza kufufua ATCL kwa kununua Bomberdier wengi walikejeli na wangine walidhani `tunabeep’. Ndege 7 tulizonunua zimewasili''
''Ndege nyingine 4 tulizonunua zitawasili kwa nyakati tofauti (Bombadier na Airbus). Ndege hizi zimeshushwa hapa na Watanzania, hadi Marekani inajulikana kuwa Watanzania wanafedha. Tembeeni kufua mbele''
''Hii inamaanisha Tanzania inaweza na Afrika inaweza''
''Najisikia raha kuwa Mwenyekiti wa CCM, nashangaa tumewezaje. Tumshukuru Mungu. Kwanini mandege haya hayakuja miaka ya nyuma? Makonda umeomba bilioni 1.5 kujenga hospitali Ubungo, nitazitoa. Waziri wa TAMISEMI tafuta fedha na hospitali ianze kujengwa Ubungo''
''Shukrani hizi zimuendee Mungu na Watanzania wote bila kujali dini na vyama vyao. Watanzania wamenunua ndege hizi kwa fedha za kodi zao, mpaka madudu haya yamekuja''
''Wameondoka kule Seattle, Marekani jana saa 3 usiku na kituo cha kwanza ni Tanzania''
''Hizi ndege zimenunuliwa kwa fedha za Serikali na sio ATCL, ninyi ATCL tumewaazima mfanye biashara. Waziri ameniambia hadi sasa wamekusanya kiasi cha dola milioni 14, nitakwenda kuzicheki kesho. Nawapongeza ATCL''
''ATCL wamepata cheti cha Ubora wa Huduma''
''Idadi ya wasafiri wa anga imeongezeka, nilikuwa Mpanda na wananchi waliomba ndege zianze kwenda, nimeambiwa safari zimeanza leo na ndege inaenda imejaa na inarudi imejaa''
''Baadhi ya maofisa wa ATCL wana lugha mbaya na nisingependa kusikia malalamiko tena''
''Tuendelee kujiamini na kutangaza mazuri ya Taifa letu. Tuongeze juhudi za kuchapa kazi na kulipa kodi''
''Sipendi kuwapotezea muda, leo ni siku ya sherehe na sio siku ya hotuba''
''Niko tayari kuzindua ndege hii yenye jina la Rubondo''