Mpira hauko kama unavyofikiri na ndio maana best loser Ivory Coast kawa bingwa Afcon. Simba isijivunie kuwafunga wydad kwa vile wameshuka kiwango ila yanga ndio ijivunie kuwafunga CRB? Sasa CRB wana maajabu gani kuwazidi wydad?Simba sina matumaini nayo kwasababu
1. Mpira dhidi ya Asec simba alicheza mpira mbovu saana Taifa, Asec angekuwa na moto Simba angechapwa goli nyingi, na kama Simba nae angekuwa na moto, angemtandika Asec hata bao 5. Hili group timu zote zina uwezo wa Wastani, hakuna atakayeingia nusu fainal kwa uwezo.
2. Dhidi ha Wydad hii ilionesha ni namna gani Wydad alivyoishiwa mpira, kiwango kimeshuka, Simba akashinda, Simba akajiona ana timu ilhali bado timu haipo.
3. Simba haina mfungaji, hakuna mtu ambaye anayeweza kusumbua defence ya Jwaneng pale kati, sijui akili gani ilitumika kumuacha Baleke. Jwaneng wakichanga karata zao vizuri, kwa perfomance hii ya Simba, kwa perfomance hii ya Simba mechi zake za hivi karibuni, siioni Simba ikichukua matokeo mazuri mbele ya Jwaneng.
Wydad au simba unaowaona wabovu wanaweza kuitoa yanga wakikutana robo.