Angalizo kwa wanaotaka kuja kutafuta ajira Afrika Kusini

Angalizo kwa wanaotaka kuja kutafuta ajira Afrika Kusini

steve_shemej

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,175
Reaction score
1,588
Natumai wazima wote leo nilikuwa natamani tushee Jambo moja na watanzania wenzangu mnaohitaji kuja kutafuta ajira huku SA

Ukweli ni kwamba ajira huenda zikawepo ila siyo kwa watanzania

Huenda hujanielewa watanzania huku hatuaminiki, ni vigumu mtu kukuamini kukupa kazi wengi "wezi' hali iliyopelekea kupunguza imani juu yetu

Huku unaweza kukuta wabongo 200 ila walioajiriwa hawazidi 40 wengi wezi Hawa hujiita "26" Hawa ni wabaya hawamwangalii wa kumuibia na waliobaki wamejiajiri kama kuuza matunda nk

Tatizo letu kubwa tunakuja SA kuja kutafuta ajira tukiwa hatuna msingi tukija tunashtukia kuwa hakuna ajira

Wenzetu Wasomali, Ethiopians, Nigerians huwa wanakuja huku na mitaji yao hata ukiwaona Wasomali wameshikwa huko Tanzania pale wanakuwa wamejipanga wanahela wakija huku wanafungua biashara wanatoboa pia wanasaidiana na kiukweli wana hela ila kwa watanzania ni kinyume

Ushawahi sikia vurugu dhidi ya watanzania? Natives wa huku huwa hawamchukii mtu asiye na mafanikio na wabongo hatuna chochote ndiyo maana hawatufanyii vurugu kama kwa wanaijeria na wengine

Wabongo huku tunauana miezi miwili ilyopita Johannesburg watanzania wamemuua mtanzania mwenzao kisa Randi 8000 sasa imagine

Nia na madhumuni ya uzi huu wewe unaetaka kuja huku jipange uwe na mtaji huku sasa hivi ajira kwa wabongo hamna brothers wa miaka ya 90s Washa tuharibia CV pamoja na watoto wa Dar Hawa huja SA kufata life style tu hawana malengo ndiyo wanaofanya watanzania woote huku tuonekane wazurulaji pia ndiyo wanaongoza kwa kuuana Kisha kusafirisha maiti kurudi Dar

NB: Kila mtu anabahati yake kana unakuja njoo ujaribu bahati yako ila jipange kisaikolojia
 
Mfano kwa kuanzia uwe Na mtaji wa shilingi ngapi za kitanzania ukija huko ili angalau mambo yaende?

Biashara gani maeneo yapi au miji ipi unaweza kutoboa kirahisi?

Kama una elimu mfano diploma au digrii ni specialization zipi ambazo kupata ajira ni rahisi?

Saidia mkuu, nafikiri wengi tutafaidika
 
Duh.... mie toka shemej angu arudi toka nje na hela mbuzi sijapata tena mzuka aisee...hapana
Pole yake aisee,😀 yaani watu tunaamini ukitoka nje huko ni rahisi kutoboa kumbe huko pia wanatamani kutoka waje huku kwetu( yaani nao wana struggle tu). Naamini mapambano popote tu ndani ama nje unaweza kutoboa muhimu ni ubunifu.🤔
 
Pole yake aisee,😀 yaani watu tunaamini ukitoka nje huko ni rahisi kutoboa kumbe huko pia wanatamani kutoka waje huku kwetu( yaani nao wana struggle tu). Naamini mapambano popote tu ndani ama nje unaweza kutoboa muhimu ni ubunifu.🤔
Haswa...alirudi na 3m...leo hii ukimpa 20k anakushukuruje
 
Mfano kwa kuanzia uwe Na mtaji wa shilling ngapi za kitanzania ukija huko ili angalau mambo yaende?

Biashara gani maeneo yapi au miji ipi unaweza kutoboa kirahisi?

Kama una elimu mfano diploma au digrii ni specialization zipi ambazo kupata ajira ni rahisi?

Saidia mkuu, nafikiri wengi tutafaidika
Ishu watakuamini wakupe hiyo ajira kama mambo yenyewe ndio yapo hivyo
 
Back
Top Bottom