Angalizo: Makonda akiendeleza siasa kwenye maandalizi ya Taifa Stars atawagawa watanzania

Angalizo: Makonda akiendeleza siasa kwenye maandalizi ya Taifa Stars atawagawa watanzania

Heshima kwenu wanajamvi.
Natoa tahadhari kwa TFF na watanzania kwa ujumla kuwa makini na propaganda za kisiasa zinazofanywa na mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda kila anapozungumzia maandalizi ya mchezo wa Taifa Stars dhididi ya Uganda.

Makonda anatumia nafasi aliyopewa ya mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kumsifia rais na serikali badals ya kuwahamasisha watanzania kuisapoti timu ya taifa.

Natoa angalizo kwa TFF kuacha kuwateua wanasiasa kwenye masuala ya mpira kwani kunawagawa watanzania badala ya kuwaunganisha.

Kama kuna jambo ambalo TFF wamekosea katika kampeni zetu za kuleta ushindi kisoka kwa timu zetu ni kumhusisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kampeni hizi....Ni kosa la kimkakati...Nilikuwa na mawazo ya kwenda kuiangalia Stars na baadhi ya michezo ya AFCON, nimeamua kutokwenda...TFF wamefanya jambo la ajabu kabisa...Suala la Taifa Stars ni la nchi na wala siyo la mkoa wa Dar es Salaam...anayepaswa kuwaa mbele katika hili ni Waziri anayehusika na michezo na siyo huyo mwingine...Sina tatizo na kijana wetu huyo ni mchapakazi mzuri, na ana mipango mizuri, lakini ana udhaifu pia.kuna masuala mengine inabidi aone kwamba hayamhusu...Ni kama lile la utekaji wa Mo...alitaka kujitokeza kuwa mseamaji wa suala nyeti kama lile wakati Waziri wa Mambo ya Ndani yupo...Ni bahati tu kuwa hakuendelea zaidi kulizungumzia lile...sasa hawa TFF wanamhusisha tena na soka...Yeye ahusike na masuala ya Dar es Salaam na siyo ya kitaifa...upo wakati akiwa ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amekwenda mpirani alivaa T shirt ya Simba kwenye mchezo uliohusisha pia Yanga ambayo nayo ni ya Dar es salaam...You can just imagine....nawashauri TFF wawe makini na masuala ya Taifa Stars, wawe makini mno...Nionavyo tayari baadhi ya watu wanachukizwa na mambo ya TFF kuhusu kampeni...Taifa Stars inakosa support pasipo maana kabisa...anyway ..niachie hapa..wako ambao hawatanielewa...Lakini kwangu mimi nilichoweka hapa ni fact...
 
Nasikitika kuwa uganda wanaweza wakacheza kisembe kwakuwa wao ata wakifungwa sio shida coz wameshafuzu tayar.

Sent using Jamii Forums mobile app
Thubutu, kwa taarifa yako tu hakuna kipindi nchi hii ina maafisa Wa shirikisho la mpira Wa miguu Africa na duniani kama kipindi hiki cha kuelekea mechi ya Mazuzu Fc Vs Uganda.


Sasa nyie pangeni matokeo mpigwe adhabu moja matata ambayo hamtakaa muisahau katika kipindi chenu cha uhai wenu.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuiombee tu timu yetu ya Taifa ishinde na kufuzu hiyo afcon. Ingawa natambua huo ushindi iwapo utapatikana, tutaambiwa ni kwa sababu ya mafanikio ya mtu fulani pasipo kuwapa heshima wanaostahili (wachezaji na benchi la ufundi). Kila kitu tunatanguliza siasa tu na siyo uzalendo.
Binafsi sikupenda huyo jamaa ashiriki kwenye haya mambo kabisa. Naona inanikera kidogo. Ingawa nilipenda Timu yetu ifanikiwe.

Uganda wameshaqualify, labda wanaweza kutulegezea kidogo, tukapata hata goli moja, na sisi tuingie..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima kwenu wanajamvi.
Natoa tahadhari kwa TFF na watanzania kwa ujumla kuwa makini na propaganda za kisiasa zinazofanywa na mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda kila anapozungumzia maandalizi ya mchezo wa Taifa Stars dhididi ya Uganda.

Makonda anatumia nafasi aliyopewa ya mwenyekiti wa kamati ya maandalizi kumsifia rais na serikali badals ya kuwahamasisha watanzania kuisapoti timu ya taifa.

Natoa angalizo kwa TFF kuacha kuwateua wanasiasa kwenye masuala ya mpira kwani kunawagawa watanzania badala ya kuwaunganisha.
Rais ni raia namba moja, taswira ya nchi, mkuu wa dola na serikali, unataka asifiwe nani? Hakuna mbadala wa rais. Ingekuwa tunao marais zaidi ya mmoja, basi tungemuhoji Makonda, "kwanini unamsifia mmoja wengine husifii?" Kwahiyo kuwa mpole akiingia wa kwako naye tutasifia.
 
viongozi wetu wanajifanya hawaoni kwamba bashite anachukiwa na vijana waliowengi. yaan yeye akiwakusanya bongo movie amaccm wachache wanahisi anaungwa mkono na makund yote, you are wrong!!

tuukubali ukweli makonda hana uwezo wa kuunganisha watu!! ana makando kando meng yanayoweza kuwagawa watu wasikubali kile anachokipeleka!!

mwishon tuu katumhukiza uongo wa mchana kweupe et vinywaji vyote vitakua nusu bei , yaan maji bia wine na vingne ving. hata iwe bia tuu bado haiwez kuwa kweli hilo tuu kwa wenye akili timamu linatisha kumdharau. siku nyingine tuweke watu wenye kukubalika makundi yote
 
Kulikuwa hakuna sababu ya msingi makondakta kuwa kwenye kamati hiyo, shida tumekuwa vipofu wa siasa vumbi, tunaona kila kitu ni sahihi kukitafutia kiki, bila kuangalia madhara yake.
 
Back
Top Bottom