Uchaguzi 2020 Angalizo: Membe ni hatari kwa upinzani kuliko alivyokuwa Lowassa

Tatizo nu kuwa huko mbeleni anaweza akakosa vyote hata kufutika kwa ACT Tanzania.
ACT kwa sasa haiwezi futika nahata huko mbeleni haitafutika, kwa sababu ACT Kwa sasa iko Pemba basi tegemea haitofutika leo wala kesho.Labda Zitto na wazanzibar wakosane nahata wakikosana hakuna atakaefutika either iwe Zitto au ACT.
 
Bado hujaleta hoja za kushawishi wapinzani wamkatae Membe kwakuwa mtaji wa siasa ni watu na membe ana watu CCM ambao ata hama nao nakwenda nao upinzani.

Hao watu ndio watagombea na kuchagua ACT. Lakini ndio hao viongozi wataohama tena toka ACT kurudi nyyumbani na kuleta mtafaruku mkubwa kwa wapenzi halisi wa ACT. Kwa sababu wapenzi wa ACT watadhani kuwa wabunge/madiwani wao wananunuliwa na chama tawala, dhana ambayo ni sumu kwa ACT. Hili ndilo ninaloliogopa!
 
ACT kwa sasa haiwezi futika nahata huko mbeleni haitafutika, kwa sababu ACT Kwa sasa iko Pemba basi tegemea haitofutika leo wala kesho.Labda Zitto na wazanzibar wakosane nahata wakikosana hakuna atakaefutika either iwe Zitto au ACT.

CUF ilikuwa Pemba na ikafutika. Ogopa mamluki aka membe ambae ni Lipumba part 2.
 
Zito hawezi kua mjinga wa kuilinda chadema wakat ambao na yeye anahis atanufaika
Membe akienda Act Zito ataongeza Wabunge na Hatujui Chadema itapoteza kwa kias Gan ila Zito anaweza kua chama kikuu cha upinzan sababu zanzibar tayar Act Ina nguvu akimuunga Membe uku akipata hata wabunge kadhaa itakua poa Sana

Mnapo mtaka Zito ajiunge na chadema mjue Baada ya uchaguz ruzuku hawagaw [emoji849]
 
Tatizo kubwa sio kuwa presidential material, hilo sina ubishi nalo.

Tatizo kubwa kabisa ni baada ya uchaguzi UPINZANI UTAKUWA NA HALI GANI? Suala la upinzani si swala la muda mfupi ni lazima liwe na long term plan. Tafakari!
Nimekuelewa sana mkuu, siungi mkono swala la Membe kuingia upinzani, though natambua uwezo wake mkubwa kisiasa.
 
CUF ilikuwa Pemba na ikafutika. Ogopa mamluki aka membe ambae ni Lipumba part 2.
CUF imefutika Pemba kwa sababu CUF Pemba nimaalim Seif, lakini leo hata Maalim akienda NCCR bado Zitto atabaki na kuaminika na baadhi ya watu wa Kigoma, hata Zitto akiondoka ACT ataenda CDM au CCM huko kote wataendelea kumtukuza kwa sababu nimjengaji hoja mzuri na mchumi mzuri kuliko wanasiasa wengi walioko huko. Uzuri wa Zitto nimzuri majukwaan lakin pia nimzuri katika eneo lake la uchambuzi siasa hasa kiuchumi sema kingine ambacho sikipendi kwake nimlazimisha furusa hata pale isipotakiwa yeye hulazimisha tu.
 
Nimekuelewa sana mkuu, siungi mkono swala la Membe kuingia upinzani, though natambua uwezo wake mkubwa kisiasa.
Kijiunga upinzan sio tatizo tatizo nikuwa akijiunga upinzan atapewa nafasi gani,Kama anajiunga upinzan amnadi Lisu hakuna shida ,Kisha yeye agombee ubunge huko kusini.
 
Washirikiane tu waangalie namna gani kila chama kitanufaika na ushirikiano huo.
 
Nimekuelewa sana mkuu, siungi mkono swala la Membe kuingia upinzani, though natambua uwezo wake mkubwa kisiasa.
Huu uwezo wa kuja tu wakati wa uchaguzi huwa unanitia mashaka? Naomba unijulishe tu kwamba tangu membe aingie kwenye siasa (ubunge na uwaziri) ni lipi jambo ambalo amelifanya kwa taifa hili kiasi cha kutuaminisha kwamba ni presedential material? Wapiga kura wangapi huko mashinani wanamjua membe? Kama walivyo viongozi wengi wa CCM (hasa awamu zilizopita) membe pia ni mhanga wa kashifa za ufisadi!
 
Mkuu kapicha basi kajapo muamala 1 kati ya hiyo miamala ya kuua upinzani zaidi ya 2.4 tr zilizotumika.
 
Wote Membe na Zito sio watu wenye Nia njema na upinzani
 
Mleta mada una point

Nitawashangaa sana upinzani wakimpa membe.hio nafasi ya kugombea nitawashangaa sana

Ina maana hawakujifunza ya lowassa

Hivi Ni kweli kwamba wao Kama wao hawawezi kuleta mshawasha was uchaguzi bila mtu toka CCM

Nitawashangaa sana aisee na nitawadharau moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe ana watu sita waliopo CCM ambao hataki kuwataja.

Na ana maadui 11 ambao akiwa Rais watahama Nchi. Ngoja tuone hii picha itaisha namna gani .
 
Waende wote

CCM - Mh J P Magufuli
ACT - Mh Benard Membe
CHADEMA - Mh Tundu Lissu

Kiu yangu chama kitakachoshida kiwe na ushindi wa 60% na vyama vinavyofuatia viwe na Jumla ya 40% hapo tutakuwa na Serikali imara na upinzani ulio imara vile vile
I second you.
Waache wote hao waende kugombea kupitia vyama tofauti kisha tupate raisi bora kabisa.

Bila shaka Mh. JP Magufuli atashinda kwa kura nyingi tu.
 
I second you.
Waache wote hao waende kugombea kupitia vyama tofauti kisha tupate raisi bora kabisa.

Bila shaka Mh. JP Magufuli atashinda kwa kura nyingi tu.
Sina tatizo na ushindi wa Mh J P Magufuli ila kiu yangu ni kuona siasa za ushindani zikiendelea kwa kuwa na Bunge ambalo Wabunge wa Chama kimoja hawawezi kubadilisha Katiba bila kupata uungwaji mkono wa upande wa pili. Uwiano wa 3:2 utachochea sana maendeleo tofauti na kuwa na uwiano wa 9:1 kwa mfano.
 
Mleta mada kaja na conspiracy theory tu, lowasa aliitikisa CCM ipasavyo, kama siyo manuavre, basi CCM ingekuwa ni chama cha upinzani au kingekuwa kishapotea kwa sasa. Kwa aliyesoma kilichotokea 2015 ni wazi Membe ana nia dhahiri ya kuwania uraisi wa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…