SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Hii mada nilikuwa nataka niielezee kwa upana ila nadhani kwa ufupi itajitosheleza.
Timu za Simba na Yanga zimebeba mioyo ya asilimia kubwa ya Watanzania. Wote tunajua inayosemekana ni historia ya Yanga katika siasa za nchi hii. Sitaingia sana huko ila uthibitisho upo na ni mkubwa kuwa mpaka leo Yanga ni mtoto wa kipekee wa CCM na serikali zake.
Simba kwa upande mwingine ni mtoto wa kambo. Huyu mtoto ameonyesha tena na tena ujuaji na kujifanya kumzidi mwenzie maarifa na kutaka maendeleo ya haraka hali inayopelekea Yanga kujitutumua ili kubalance mzani wa ushindani.
Simba amepigwa pini au kuvutwa shati sana tu katika mazingira na vipindi mbalimbali pale walipoonekana wameshindikana na wanakaribia kumuacha kwa mbali toto pendwa.
Njia kuu inayoweza kutumika kucontrol maendeleo ya club ni kwa kupandikiza viongozi wasio na mapenzi ya kweli na timu, halafu viongozi hao kusajili wachezaji wasio na uwezo au kung'ang'ania wale ambao wanaweza kutumika kwa shughuli hizo.
Sitashangaa kama ghafla suala zima la ushiriki wa Simba katika CAF Super Cup kugubikwa na giza na sintofahamu. Watu fulani fulani kwa kutopendezwa kuona toto pendwa haingii katika mashindano hayo wanaweza kwa makusudi kurubuni vigezo muhimu vilivyowekwa na CAF.
Simba wasibweteke na support wanayopewaga na wakubwa fulani fulani. Watu hawa wanaweza kuwa ni wapenzi wa Simba ila siasa nchi hii ni kama dini, hivyo si vyema kuweka maslahi ya club yategemee weledi au fadhila za watu fulani ambao maslahi yao ya kisiasa yanaweza kuwafanya waihujumu timu.
Ni ngumu lakini inawezekana. Nadhani nitakuwa nimeeleweka.