Angalizo: The state nyie ndio mtakaolaumiwa nchi yetu ikiyumba

Angalizo: The state nyie ndio mtakaolaumiwa nchi yetu ikiyumba

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Kelele zimeanza kusikika mapema kabisa kuhusu deni la Taifa! Hadi sasa ndani ya miezi michache ya Mama tena tisa tu tayari trillion 10 na zaidi ya nusu ya mkopo huo ukielekea visiwani Zanzibar wakati bado kuna miradi mikubwa ya bara kama stiglers na Bwawa la umeme haijakamilika Hadi sasa.

Inawezekana kabisa serekali ya Mama haina uhakika wa kuendelea tena kuwepo madarakani hapo 2025 ndio maana kaamua kutumia turufu ya uraisi wake kukopa mikopo mikubwa ili ajenge kwao Bila kujali madhara ya mikopo hiyo kwa Taifa letu.

Historia haidanganyi Ethiopia iliwahi kukopa mikopo mikubwa Kama hii tena kwa pupa kama tunavofanya hapa kwetu matokeo yake ni kibano kwa raia wake kwa zigo la kodi lisilobebeka hadi ikafikia hatua nchi haikaliki hadi sasa!

Wananchi wamekua wakimbizi wa Kodi na ugumu wa maisha!! Hilo ni onyo kwetu kama hali ikiendelea kuwa hivi basi tunaenda shimoni.

The state Kuna haja ya kutumia mamlaka yenu kwa serekali iliyopo kabla mambo hayajaharibika!!mkikaa kimya na kuendelea kuwachekea Hawa viongozi na chama chao mkasahau viapo vyenu mjue mtalaumiwa baadae na wananchi!

Viashiria vyote vinaonyesha kabisa kia kuna hofu ya kukimbizana na muda wa madaraka kwa Mama ,ndio maana anakopa kwa fujo ili atimize matamanio yake kwa muda mfupi.

Kama mnamacho na masikio basi fanyeni Jambo mapema kabla mambo hayajaharibika zaidi!!!
 
Punguza hasira kunywa maji mengi. Then uje tujadili hoja kwa utulivu
Hasira za nini,weka hiyo mikopo mbona mimi nimeweka?

Tuonyeshe til.ya kujenga uwanja pemba kwenye mchanganuo hapa chini.

Screenshot_20211228-190058.png


Screenshot_20211228-190007.png


Screenshot_20211228-190207.png
 
The state Kuna haja ya kutumia mamlaka yenu kwa serekali iliyopo kabla mambo hayajaharibika!!
Hivi unaongelea deep state ya nchi gani?
Hapa kwetu wamejazwa vijana wa hovyo ambao wengi wao wana unasaba na hawa hawa viongozi.

Nchi hii tumepigwa na kitu kizito akilini
 
Hili koti zito sana inapendeza kulivua sasa na kulitundika kwenye 🌲
 
Mimi ni mnyaki wa kumasai.

Sijawahi kuona mijitu mibaguzi kama sisi wa Bara.

Mnajua ni haki ngapi za mgawo wa kiitifaki Zanzibar wamedhulumiwa?

Kama ni kuimarisha Muungano kuna tatizo gani tukiwa na miradi ya kimkakati kuongeza makusanyo ya serikali? Au mnataka kuvitawala visiwa vile kwa kuhakikisha wanakuwa maskini wa kutupwa?

Acheni gubu, wivu na uvivu
 
Back
Top Bottom