jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Nichukue Fursa hii kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusukuma mbele gurudumu la maendeleo nchini Tanzania. Yapo mambo mengi yaliyobadilishwa naye katika kipindi kifupi kwa mustakabali wa Tanzania mbele ya Uso wa kidiplomasia.
Mengi ni mazuri na ni muendelezo na marekebisho wa awamu ya Tano.
ANGALIZO
Tunatarajia kuletewa marekebisho mbalimbali ya kisheria yanayogusa rasilimali zetu hususani katika eneo la nishati.
Ikumbukwe kuwa tulikuwa na sheria mbovu zilizokosa meno katika usimamizi wa rasilimali zetu za asili jambo lililopelekea tuje nasheria za umiliki wa rasilimali zetu za asili.
Tulitumia nguvu na mali nyingi ili kufanikisha suala hilo na hatimaye tukawa na sheria bora za udhibiti wa rasilimali hizo za asili.
Tunapoelekea kushangilia ufutaji wa mzigo wa kodi na tozo mbalimbali katika mafuta/nishati kamwe tusije KUCHOMEKEWA jambo bovu litakaloondoa milestone tuliyoifikia.yaani umiliki wa rasilimali zetu.
NASAHA KWA BUNGE
Tusome na kuelewa in details kile kitakachowasikishwa katika mapendekezo ya marekebisho ya sheria. Tukumbuke kuwa tunachokibadilisha kinaweza kubadilishwa pia lakini maamuzi ya leo yana athari ya kesho.
#CATEGORICAL#
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!