radika
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 20,440
- 32,260
Si mara moja polisi kuhusishwa na matukio ya upotevu wa watu wanaowakamata pale wanapoondoka nao na kutoweka kwenye mazingira ya utata au kupotea moja kwa moja.
Kwa yaliyotokea kwa ndugu yatu Sativa (Edgar) ni muendelezo wa hatari iliyopo pindi ndugu zetu wanapokuwa katika mikono ya polisi, ndugu yetu anasema alipelekwa hadi Kituo cha Polisi Osterbay cha ajabu hapakuwa hata na taarifa zake hii ilikuwa na maana gani? Kumtoa uhai bila watu kujua? Ndugu wanamtafuta wameenda hadi kituo hicho cha polisi na hao polisi walikataa kumshikiria ndugu Sativa hii kutokana na kutomuingiza ktk rekodi ili iwe rahisi kumpoteza.
Polisi siyo sehemu salama tena ndugu zangu kila mmoja anapoona ndugu yake au Mtanzania kachukuliwa na polisi basi ajue kuna mawili, kumuona tena nudgu yake au kumpoteza moja kwa moja, kodi za Watanzania zinatumika vibaya sana!
Ukiona ndugu yako anaondoka na polisi itaneni muwe hata wa 4 au zaidi kuhakikisha anafika salama na hali ya afya yake mliyomuacha nayo na kuyajua majina ya polisi na vitambulisho vyao vya kazi msikubali waondoke nao peke yao itakula kwenu.
Polisi sio sehemu salama tena.
====
Pia soma: Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana