Angekuwa ndio Magufuli kapokea report ya CAG leo, naamini angefanya maamuzi haya ya kishujaa...

Angekuwa ndio Magufuli kapokea report ya CAG leo, naamini angefanya maamuzi haya ya kishujaa...

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Nawashangaa mnaomsifia Madam Samia kwa kumsimamisha DG wa TPA na kumpa onyo Jaffo.

Binafsi naamini Magufuli angekuwa hai leo, Angevunja bodi nzima ya TPA, DG angefukuzwa na sio kusimamishwa. Jaffo angetumbuliwa sababu alishaonywa mapema,angeteua mwanajeshi kuwa DG mpya wa TPA waziri mpya wa Tamisemi angeweza kuwa mkuchika au Mhagama

Sasa huyu mama ameanza kucheka na nyani mapema yote hii.

Ngoja tuone
 
Unayosema ni kweli kabisa. Usichojua ni kwamba JPM alikuwa mtawala na kaeaida ya watawala hutawala na kuchukua maamuzi kutegemeana na ameamkaje lakini SSH ni Kiongozi na mara zote Kiongozi huongoza kulingana na Sheria zinavyosema. Utamfukuzaje DG ilihali tuhuma hazijachunguzwa?
 
Hao wapigaji na wazembe wote ulio wataja waliteuliwa na nani? Unataka kuniambia aliye wateua alikurupuka? Au ndiyo business as usual?

Yaani unalitengeza tatizo, halafu baadae unakuja kulitatua mwenyewe kwa mbwembwe! ili tu upate umaarufu wa kisiasa! Au siyo!! Anyway, mwacheni mzee apumzike huko aliko.

Ni wakati sahihi sasa kama Taifa kupigania mifumo imara, badala ya watu imara.
 
Nawashangaa mnaomsifia Madam Samia kwa kumsimamisha DG wa TPA na kumpa onyo Jaffo.Binafsi naamini Magufuli angekuwa hai leo,Angevunja bodi nzima ya TPA,DG angefukuzwa na sio kusimamishwa.Jaffo angetumbuliwa sababu alishaonywa mapema,angeteua mwanajeshi kuwa DG mpya wa TPA.waziri mpya wa Tamisemi angeweza kuwa mkuchika au Mhagama.
Sasa huyu mama ameanza kucheka na nyani mapema yote hii..ngoja tuone
Rais mama samia si magufuli. muache kumu underrate kwenye maamuzi yake.
kila rais ana character yake.
ana style yake ya kufanya kazi.

kila kitu Magufuli Magufuli. No offence alikuwa ni mtu wa maamuzi.
lakin he is gone .. gone forever. tuache kutembelea kwenye kivuli chake.
 
CAG alikuwa anasoma taarifa kwa hofu....baadaye mama akamtia nguvu kuwa aseme kila kwa uwazi. Ripoti iliyopita ni 20% zilijibiwa, 40% hazijakamilika, lakini 40% nyingine hata haijulikani... Mama aliwaambia atalisimamia mwenyewe
 
Back
Top Bottom