Angekuwepo Magufuli, bei ya cement isingefikia Tsh 28000/= kanda ya ziwa

Angekuwepo Magufuli, bei ya cement isingefikia Tsh 28000/= kanda ya ziwa

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,480
Reaction score
7,443
Kanda ya ziwa Victoria inafanyiwa harassment ya kisiasa sana.

Maisha yapo juu hususani bei ya cement. Kwa miaka nenda rudi bei ya cement ni tatizk kubwa kanda ya ziwa. Leo hii imefikia Tsh 28000/=

Hii yote ni kwa sababu gharama za usafirishaji kwa kutumia malori ni kubwa ndio maana bei ni kubwa Kanda ya ziwa.

Lakini angekuwepo hayati JPM mradi wa treni ya Sgr ungekuwa umekamilika. Gharama za usafirishani wa cement zingepungua na kanda ya ziwa bei isingefikia Tsh 28000/=
 
Alikuwa na Kiwanda cha cement? Huyo si ndio alipoingia tu madarakani na ule ulimbukeni wake wa madaraka mafuta ya kula na sukari zikapanda ghafla? Amesahau yeye ndio alianza kumsumbua Dangote na Kiwanda chake cha cement?
 
Alikuwa na Kiwanda cha cement? Huyo si ndio alipoingia tu madarakani na ule ulimbukeni wake wa madaraka mafuta ya kula na sukari zikapanda ghafla? Amesahau yeye ndio alianza kumsumbua Dangite na Kiwanda chake cha cement?
We unajibu mada kwa kuwa na chuki na mtu. Ishu ya sukari zilikuwa njama za mafisadi na alidhibiti. Ulitaka Dongete awekeze kibwege kama ilivyofanyika Bulyanhulu?
 
Hili nalo nijambo la kulifikilia. Tusikumbatie Kesi Zisizo na faida kwa taifa huku wananchi wanataabika na ugumu wa maisha kutokana na upandaji wa bei za bidhaa kiholela.Ambapo pesa hizo za uendeshaji wa kesi zisizo na faida zingeweza kutengwa kama ruzuku kwa wananchi wake ili kupunguza gharama za maisha zinazokana na bei za bidhaa kupanda kiholela...
 
We unajibu mada kwa kuwa na chuki na mtu. Ishu ya sukari zilikuwa njama za mafisadi na alidhibiti. Ulitaka Dongete awekeze kibwege kama ilivyofanyika Bulyanhulu?
Huyo jamaa huwa ana Magufuli sickness na hajawahi kuona watu wengine wana uwezo zaidi ya watu wa Chadema yaani assessment zake zipo kichana zaidi badala ya mtu anayetawala chama.
 
Kanda ya ziwa Victoria inafanyiwa harassment ya kisiasa sana.

Maisha yapo juu hususani bei ya cement. Kwa miaka nenda rudi bei ya cement ni tatizk kubwa kanda ya ziwa. Leo hii imefikia Tsh 28000/=

Hii yote ni kwa sababu gharama za usafirishaji kwa kutumia malori ni kubwa ndio maana bei ni kubwa Kanda ya ziwa.

Lakini angekuwepo hayati JPM mradi wa treni ya Sgr ungekuwa umekamilika. Gharama za usafirishani wa cement zingepungua na kanda ya ziwa bei isingefikia Tsh 28000/=
Alikuwepo Sukari ikafikia 5800 2018
Alikuwepo bando ya bati nyeupe ilipanda kutoka 200k mpaka 460000 2019.
Alikuwepo Mbolea ilipanda kutoka 50 UREA hadi 65000.
Alikuwepo nondo ilipanda kutoka 13000 mpaka 23000 2018.
Alikuwepo Cement kanda ya Ziwa ilipanda kutoka 15000 mpaka 17000.

Msiwe wepesi wa kusahau.
 
Huyo mleta uzi ni mjinga, anadhani tunasahau kwa kiwango hicho. Nikisikia mtu anasema tu angekuwepo Magufuli, najua alijaa kwenye propaganda za utawala wake.
 
Hii yote ni kwa sababu gharama za usafirishaji kwa kutumia malori ni kubwa ndio maana bei ni kubwa Kanda ya ziwa.
Wahandisi na wanasayansi waingie kazini kutengeneza mbadala wa materials ya cement. Materials hayo yawe yanapatikana huko huko kanda ya ziwa.

Furusa hiyo kwa wanasayansi na wahandisi wetu.
 
Back
Top Bottom