Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Baada ya Chadema kutangaza maandamano kupinga kutekwa na kuuwawa kwa Wanachama wao na Watanzania kulitokea ka tension kadogo.
Tension hii ilipata msisimko baada ya Viongozi wa dini kuanza kukemea.
Kwa kuwa tuhuma hizi zilikihusu Chama cha Mapinduzi na vyombo vya Serikali yake hasa Polisi na TISS ilihitajika kauli thabiti na yenye hekima kutoka Chama cha Mapinduzi.
Tuseme ukweli Press aliyoifanya Comred Emmanuel Nchimi ilituliza sana mioyo ya watanzania ingawa haikuwapa majibu juu ya mustakabali ya haki yao kuu ya kuishi!
Nchimbi kama Mwanasiasa aliyelelewa na wazee wenye exposure hekima na busara aliongea vizuri sana na kwa sehemu kubwa kuweza kutuliza tension ya Wananchi.
Kituko kilikuja kutokea jana. Kusema kweli Mwenyekiti jana ametia petrol na kiberiti kwenye moto alioweza kuuzima kidogo Comrade Nchimbi.
Mbaya zaidi kanunua ugomvi na wakubwa ambao ndiyo wanamlisha na kuendesha miradi yake mingi kwa misaada na mikopo yao.
Nimefuatilia maoni ya wananchi kwa jana na leo, mitaani na kwenye mitandao. Kusema ukweli Mwenyekiti wetu jana aliharibu sana.
Wananchi wanatoa maoni bila kificho tena kwa account zenye majina yao kulaaani maneno yake ya jana.
Swali nililojiuliza ni kuwa, baada ya Comrade Nchimbi kuzungumza vizuri siku ile na kutuliza upepo. Kulikuwa na haja ya yeye jana kuzungumza maneno yale aliyozungumza?
Ushauri wangu kwake,
" Gombana na Nchi za Magharibi ukiwa na internal support na kamwe usianzishe ugomvi na Magharibi ukiwa hohehahe kwenye internal support "