Nime pewa nafasi na Mungu kuishi kwenye tawala za marais wote. Kuanzia Mwalimu, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magu na sasa Mama wa Kizimkazi, niseme tuu ukweli toka moyoni, sijawahi kumsikia rais alie toa hutuba mbovu kama ya huyu mama wa Kizimkazi.
Sijui kama labda hakuipitia kabla ya kuhutubia au alifanya vile akidhani ni hotuba konki.
Ati kifo ni kifo, ati wasi nipangie, mara mimi ni amiri jeshi mkuu, ni nani asie jua yeye ni amiri jeshi mkuu na rais wa nchi? Mara wame ota mikia, mara wengine walitoroka nchi wana hamu ya kutoroka tena.
Alisha wahi kutuambia katiba ni kijitabu, jana a a sema ana ongoza kwa mujibu wa katiba. Yaani jana hutuba yake ilikuwa vurugu vurugu.. Mungu tusaidie.