Angola walitangaza zabuni na DP World ikashinda na sasa yasimamia kitengo cha makontena bandari ya Luanda

Makubaliano hayana msingi wa kisheria hayo mambo ya mda Serikali imeshasema yataonekana kwenye mkataba wa utekelezwaji Sasa shida Iko wapi?
Anyway, tuseme ni makubaliano, ni kwanini walikubaliana na hivyo vipengele? Ni vizuri sana?
 
Umetolea mfano wa Angola ila huo mkataba wao umeuona, kuusoma na kuuelewa?, Upo Kama huu wakwetu?
 
Baada ya kusoma heading tuu nikajua umeandika ujinga..

Waziri Mbarawa alisema zaidi ya makampuni 8 yalijitokeza na DP World ndio ikashinda Kwa vigezo Sasa huu upotoshaji unatoka wapi?
Mkataba wa Serikali ya Angola na DP world ni miaka 20.

Soma hapa: DP World signs 20-year concession agreement with Angola

Je, mkataba wa Serikali ya Tanzania na DP World ni miaka mingapi?

Pia tambua kuwa mkataba wa DP world na serikali ya Angola ni kuendesha shughuli za kitengo cha makontena tu na si bandari nzima au bandari zingine.
 
Vipengele vina shida gani?
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 

ChoiceVariable


Waitwa hapa kujibu masuali ya msingi.
 
Sasa kwetu Mwarabu anakuja na karatasi za kufungiwa vitumbua (Zitto, 2023) halafu Bunge letu linakaa na kuzijadili hizo karatasi.

Akili ya kuambiwa changan ya na zako (JK, 2013).

Tanzania kichwa cha Mwendawazimu (Mwinyi, 1993).
 
Ten

Tenda itangazwe TANePS kila mwenye GPSA aombe!!!!!
 
Uzushi huu achana nao
 
Sasa huyu mama kawapa bandari zote kwa 100%.
 
Naandika point wenzio wanasema wacha tukumbize ji kibatali letu kila wilaya tuwazibe midomo kina TL na wote wanapinga DP, hamna jinsi.. Ji moto linavyowaka kila wilaya wajinga wanalala usingizi wa pono.. wenye DP yao wanaendelea na maandalizi ya awali ya mwekezaji😁😁na wambia Siku ule moto ukiacha kuzungushwa.. Mtaamka...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…