Pre GE2025 Anguko la CCM linazidi kuonekana chini ya utawala wa Awamu ya 6

Pre GE2025 Anguko la CCM linazidi kuonekana chini ya utawala wa Awamu ya 6

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
chama dola kongwe kimeishiwa mbinu zote walizozoea kutumia kama silaha, ambazo ni Bunge, Mahakama, Sheria za Uchu wa Kubaki Madarakani, Propaganda Mfu Amani ipo Tanzania n.k
  • 2024 September Mauaji yapigiwa kelele waziwazi mbele ya waziri wa mambo ya ndani Eng. Masauni ktk maziko ya mzee Ali Mohamed Kibao
  • 2024 Mahakama Kuu inajitutumua kuacha kutumiwa kama silaha ya vitisho na CCM- KESI YA TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa mitaa, vitongoji na vijiji pingamizi la serikali latupiliwa mbali
  • 2024 Agosti - Watu wa nyikani Ngorongoro wajiunga ktk wingi wao kama jamii ya kiMaasai, serikali ya CCM yasalimu amri Kabudi na Lukuvi waenda kuomba msamaha
  • 2024 Agosti serikali ya CCM yatumia chakula kama silaha ya kivita kwa kuweka mageti barabarani kuzuia chakula kisifike Ngorongoro
  • 2024 kuelekea Siku ya Vijana Duniani tarehe 12 Agosti 2024 jijini Mbeya wafuasi 500 wa CHADEMA wasukumwa mahabusu na kutishiwa kufunguliwa kesi,
  • 2023 November CCM yatumia bunge lake la chama kimoja Dodoma kama silaha ya ugandamizi, kwa kupuuza kuweka viraka vya sheria ya uchaguzi Tume Huru ya Uchaguzi INEC isiweze kusimamia uchaguzi wa November 2024
  • 2023 Tundu Lissu na CHADEMA Kanda ya kaskazini wazuiwa kuingia Ngorongoro Loliondo na kufunguliwa kesi, ambazo serikali imeshindwa kuendlea na kesi
Tuache kujidanganya ccm ni taasisi imara sana ingawa ina mapungufu yake kwenye mambo kadhaa ila imeviacha mbali sana hivi vyama vingine huo ndio ukweli, 2025 ccm itashinda kwa kishindo sioni wa kuisumbua ccm kwa sasa
 
Katika uchaguzi ujao katika Mkoa wa Dsalaam hakuna mbunge yeyote atakayepenya isipokuwa tu kama Mhe. Zungu atagombea yeye atapenya. Wengine wote ni chali.
 
Kama ni kusubiria anguko la chama dola, na kuhakikishia utasubiri sana kwasababu CCM sio tuu ni chama cha siasa, ni chama dola, ni dola!. CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
P
CCM itaanguka ikishindwa kubadilika ikaendelea kuishi zama za giza watu wameshatoka huko CCM ibadilishe siasa zake lakini ikiendelea kutegemea kugawa kanga na vitenge na kofia kupata kura itaondoka system itafika kipindi itachoka kubeba chama mzee Mda haujawai kudanganya hata kama sio leo ila time itafika
 
Chama dola kongwe kimeishiwa mbinu zote walizozoea kutumia kama silaha, ambazo ni Bunge, Mahakama, Sheria za Uchu wa Kubaki Madarakani, Propaganda Mfu Amani ipo Tanzania n.k
  • 2024 September Mauaji yapigiwa kelele waziwazi mbele ya waziri wa mambo ya ndani Eng. Masauni ktk maziko ya mzee Ali Mohamed Kibao
  • 2024 Mahakama Kuu inajitutumua kuacha kutumiwa kama silaha ya vitisho na CCM- KESI YA TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa mitaa, vitongoji na vijiji pingamizi la serikali latupiliwa mbali
  • 2024 Agosti - Watu wa nyikani Ngorongoro wajiunga ktk wingi wao kama jamii ya kiMaasai, serikali ya CCM yasalimu amri Kabudi na Lukuvi waenda kuomba msamaha
  • 2024 Agosti serikali ya CCM yatumia chakula kama silaha ya kivita kwa kuweka mageti barabarani kuzuia chakula kisifike Ngorongoro
  • 2024 kuelekea Siku ya Vijana Duniani tarehe 12 Agosti 2024 jijini Mbeya wafuasi 500 wa CHADEMA wasukumwa mahabusu na kutishiwa kufunguliwa kesi,
  • 2023 November CCM yatumia bunge lake la chama kimoja Dodoma kama silaha ya ugandamizi, kwa kupuuza kuweka viraka vya sheria ya uchaguzi Tume Huru ya Uchaguzi INEC isiweze kusimamia uchaguzi wa November 2024
  • 2023 Tundu Lissu na CHADEMA Kanda ya kaskazini wazuiwa kuingia Ngorongoro Loliondo na kufunguliwa kesi, ambazo serikali imeshindwa kuendlea na kesi
Infact,
chama cha siasa Tawala, kupitia kwenye hiyo misukosuko michache sana kati ya mingi iliyopitia na katika yote na ikavuka salama,

kinakua kimekomaa vizuri zaid, kimeimarika zaid katika kupitia miongoni mwa hali nyingine zozote ngumu,

na kwahivyo huo ni msingi wa kujizatiti zaid mamlakani bila kutetereshwa na mbilingembilinge zozote zile, kwasabb uzoefu, nguvu , mbinu na uwezo wa kukabiliana nazo ni mkubwa mno...🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu wabariki viongozi wote Tanzania
 
CCM itaanguka ikishindwa kubadilika ikaendelea kuishi zama za giza watu wameshatoka huko CCM ibadilishe siasa zake lakini ikiendelea kutegemea kugawa kanga na vitenge na kofia kupata kura itaondoka system itafika kipindi itachoka kubeba chama mzee Mda haujawai kudanganya hata kama sio leo ila time itafika
ingekua haizalishi, haiandai wala haiwapi watoto na vijana mafunzo ya kiutawala na kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye chama na Serikali, hoja yako ingalikua na maana,

but naona nilichosema ni kinyume chake sasa, na hivyo hakuna kitisho wala hatari ati siku ingine CCM inaweza kutoka madarakani Tanzania

kwasabb hakuna mbadala nje ya CCM bali mbadala wa CCM upo ndani ya CCM yenyewe 🐒
 
Let's assume you are right kuwa this is the right time, ili CCM iondoke ni lazima kwanza wa kuchukua nafasi yake apatikane ndipo CCM ifungeshe!, jee mtu huyo yupo?.
Kwa maoni yangu bado hayupo hivyo CCM bado ipo sana tuu!, hizi kelele zote za sasa ni hasira tuu baada ya muda zitapoa na hili nalo litapita!.
P
Hayupo Kwa kuwa bado wanataka kuendelea kutawala. Madaraka ni matamu. Kuanzia kwenye ubalozi wa nyumba 10 balozi huwa anaamini kuwa hakuna kama yeye atakayekuwa balozi. Siyo AJABU KWA CCM KUAMINI KUWA hakuna MWENYE UWEZO WA kutawala zaidi ya mwanachama wa CCM. Lakini hii HOJA SIYO YA KWELI KWA SABABU ZIFUATAZO;
1. CCM imekuwa ikiteua viongozi wa upinzani kuwapa madaraka MAKUBWA , Mfano Kafulila alitokea upinzani, marehemu ANNA MUGHWIRA aliteuliwa kuwa mkuu wa MKOA mpaka KIFO kilipomkuta.. LEO HII PROF.KITILA MKUMBO NI WAZIRI na alitokea UPINZANI.
2. NCHI hii Ina wasomi wengi sana wenye milengo tofauti na mambo ya CCM. Hawa watu Wana upeo mkubwa sana wa kiuongozi na kiutawala. Maana kutawala ni kuonesha njia .CCM hawakuanza kutawala Bali NI TANU na ASP Tanganyika na Zanzibar kila mmoja.. HIVYO SIYO KWELI kwamba CHADEMA AU ACT akiingia madarakani hawezi kutawala. hivi vyama vina watu wasomi sana.
3.Tanzania ni nchi ya mfumo wa VYAMA vingi( MULTIPARTISM) system.. mfumo huu unaamini kuwa nchi inaweza kutawaliwa na vyama tofauti.ndiyo maana mbunge wa CHADEMA au CCM wanalipwa na Kodi za watanganyika au wazanzibar.
3. Walio CCM Wamethibitisha wazi kuwa mambo yamewaendea kombo.
Rushwa, kila Kona, mwl haendi kusimamia mitihani bila rushwa,
Upendeleo wa Hali ya juu maofisini . Nipo serikalini nayaona haya, sipo serikalini Kwa kuwa nilipendelewa Nina kila alichonacho msomi wa Tanzania na upevu wa ufaham wangu ni mkubwa sana kuhusu nchi hii. Tunajitoa faham na kuona kila KITU kipo sawa lkn Kwa kweli CCM itasababisha damu ya watanzania wengi kumwagika.
4. Tume ya UCHAGUZI SIYO HURU . Mtendaji wa kata ni mwakilishi wa mkurugenzi, ndiye msimamizi wa uchaguzi kata Kwa nafasi yake huku akiwajibika moja Kwa moja Kwa mkurugenzi wa wilaya. Mkurugenzi mteuliwa wa rais. Wakuu wote wa time ya UCHAGUZI ni watu wa CCM. HIZI NDIZO SABABU KUU KWANINI CCM INAAMINI HAMNA ZAIDI YAKE.
 
Hakuna marefu yasiyo na ncha
Kila lenye sura lazima lina kisogo
Kila lenye mwanzo..

RIP - CCM.
Kuzaliwa 05/02/1977
Kufa....... 2025.
 
Umeshasoma mara ngapi neno anguko la CCM limefika?

Kuanzia magazetini miaka hiyo ya Kikwete. Na leo unasoma neno lile lile.
Anguko halitokani na kusoma bali dalili na viashiria sahihi.Ukiwa mzee dalili za kufa kwako zitakua wazi zaidi kulingana na viashiria vinavyojitokeza.na kadri miaka inavyoenda ndivyo na viashiria vinazidi kuongezeka.fanya tathmin utaona toka kikwete hadi sasa kumeshaongezeka viashiria vingapi alafu utaona jinsi ambavyo kifo ki karibu.
 
Tuache kujidanganya ccm ni taasisi imara sana ingawa ina mapungufu yake kwenye mambo kadhaa ila imeviacha mbali sana hivi vyama vingine huo ndio ukweli, 2025 ccm itashinda kwa kishindo sioni wa kuisumbua ccm kwa sasa
Imeviacha vyama vingine kwa weledi na haki au kwakubebwa na vyombo vya dola na tume ya uchaguzi.toa sifa kwa usawa ili tulianganishe kwa haki.
 
Back
Top Bottom