Achilia mbali "chama dola", hata dola yenyewe huanguka na kupotea kabisa...
Dola ya Rumi, Dola ya Misri ya kale chini ya Farao zilizowahi kuwa na nguvu sana duniani, zilianguka na kupotea hadi leo....
Mwisho wa jambo lolote haupimwi wala kuangaliwa kwa namna unavyoangalia wewe kwa kuwa unaona ukubwa wake, nguvu zake na uwezo wake kwa macho yako tu ya damu na nyama...
Mwisho wa kitu au jambo hupimwa kwa kuangalia majira na ishara za nyakati....
Watu wa Sodoma na Gomorra waliangamia wote kwa sbb ya ujinga wao wa kutosoma ishara za nyakati na majira. Walikuwa wanajiona wako fresh, wana kila kitu, nguvu na mapesa ya kula maraha. Bahati mbaya ni kuwa walikuwa wajinga kama walivyo CCM leo....!
Kizazi cha Nuhu (Noah) kilichoangamizwa na mafuriko ya maji (gharika) ya Mungu kilikuwa na kila kitu, kilijiona kina akili na nguvu nyingi, lakini kikaangamia chote kwa sababu ya ujinga wa kushindwa kuzielewa ishara za nyakati na majira kama walivyo CCM....
Ishara za nyakati na majira, zinathibitisha mwisho wa CCM umefika haijalishi mnajiona mna nguvu kiasi gani maana hazitawasaidia kwa kuwa MAJIRA na NYAKATI zina nguvu zaidi ya hizo zenu
Kumbuka kanuni hii muhimu ya asili: Kwamba, hakuna kilicho na mwanzo kikakosa kuwa na mwisho wake....!!