Anguko la Diamond ni sawa na "Mr nice"

Anguko la Diamond ni sawa na "Mr nice"

Habari zenu wakuu.
Kwa jinsi upepo unavyovuma sina budi kusema kwamba huyu kijanaa mwenzetu kutoka tandale anaelekea kuanguakia pua kama ilivyotokea kwa msanii mwenzake Mr nice( Lucas mkenda),sababu kubwa itakayofanya huyu kijana wetu aanguke mshindo mkubwa ni kulewa sifa kiasi kwamba anatumia umaarufu wake kutoa nyimbo ambazo hazina viwango.
Kitu kingine ni kwamba inaonekana huyu bwana mdogo anatumia nguvu na ukubwa wa timu yake kusambaza nyimbo ambazo ziko chini ya kiwango kitu ambacho ni makosa makubwa kwasababu sisi ambao hatuna timu au hatuko kwenye timu yake ni rahisi sana kuona ubovu wa nyimbo zake kwasababu tunatumia akili zetu kuchambua tofauti na members wa timu yake ambao hutumia mihemko.
Kitu kingine anachofanya huyu kijana ambacho sio kizuri ni kutumia nguvu kubwa kwenye video ili kuficha ubovu wa audio kitu ambacho kwa upande mwingine kinapelekea kuwanyima haki ya kusikiliza mziki mzuri wale wasiotizama video zake.
Mwisho.
Diamond alikuja vizuri sana lakini huko anakoenda kuna giza nene lisiloelezeka, kwani kwa hizi nyimbo zake mbili mpya za yeye na Neyo na rich mavoko zinaashiria kwamba graph yake inashuka kwa kasi.
Namshauri aangalie sana management aliyonayo kwa sasa maana naona huyu "Salam" anafanya umbeya zaidi kuliko kazi anazotakiwa kufanya,pia ikiwezekana siku moja moja afanye nyimbo zake kwenye studio nyingine siyo kila siku "WASAFI RECORD"maana naamini hawawezi kujua kila kitu,pia aache kufanya vitu kwa mazoeya.
Naona wachawi povu linawatokaa
 
Mi sipo kishabiki zaidi! Labda tu tuseme ukwl Hiv onana ya diamond ft Mr flaver ni sawa na merry u alioaimba na neyo? Mi naendelea kusisitiza wasanii wetu watashuka viwango kw ajili ya matim ukwl ndo huo! Tim hazina msaada kw msanii kw sababu hazina ushaur wanapokea chochote wanachopewa hilo ni tattizo kubwa!! Diamond ni msanii mzuri Sna! Lakin kwnye hii sehem ya nyimbo ya rich kiwango ni kidogo Sana. Ni mara 100 ile nyimbo ya watora ya yule mzimbabwe alifanya vizur sna!! Kiukwl nyimbo hii kama kaitunga mwenyewe HAPA AMETEREZA...! Bak na timu zako tunaepnda wasanii wetu tunasemaga ukwl! Hii nyimbo haieleweki mkuu!
 
Umesema nikuletee ushahidi wa copy & paste iliyofanywa na WCB nimekuletea.

Jay z akiliwa jicho na wewe utakuwa tayari kuliwa jicho??
Hakuna uhusiano wa kuliwa jicho na ku copy muzic...kwani ndugu we darasa la ngapi?sikutegemea unaweza fananisha ivo vitu viwili....afu unapozungumzia copy n paste ujue ht maana yake...mi sioni copy n paste hapo...rangi hazifanani,vitanda havifanani...arrangement ya items ktk izo scene hazifanani...copy n paste maana yake kila kitu kina kua vile vile hakuna mabadiliko bt hapo kuna mabadiliko makubwa...sema ka copy idea ila sio copy n paste...ukiweka paste unabadili maana...
 
Hvi management ya domo imeshindwa kubuni video kabisaa??? maana ile ya kwanza tulisema bahati mbaya akarudia tena na psquare kaja karudia tena na mavoko hv shida ni nn? kwann hatak kuumiza kichwa kutoa video yake mwenyewe?
 
Mi sipo kishabiki zaidi! Labda tu tuseme ukwl Hiv onana ya diamond ft Mr flaver ni sawa na merry u alioaimba na neyo? Mi naendelea kusisitiza wasanii wetu watashuka viwango kw ajili ya matim ukwl ndo huo! Tim hazina msaada kw msanii kw sababu hazina ushaur wanapokea chochote wanachopewa hilo ni tattizo kubwa!! Diamond ni msanii mzuri Sna! Lakin kwnye hii sehem ya nyimbo ya rich kiwango ni kidogo Sana. Ni mara 100 ile nyimbo ya watora ya yule mzimbabwe alifanya vizur sna!! Kiukwl nyimbo hii kama kaitunga mwenyewe HAPA AMETEREZA...! Bak na timu zako tunaepnda wasanii wetu tunasemaga ukwl! Hii nyimbo haieleweki mkuu!
Mkuu ningejua ulipe ningekupa offer ya lunch
 
Tatizo haya matimu ndo chanzo cha wasanii kuelekea kubaya kiukwl kabisa!! Unajua mm huwa napnda nyimbo na huwa sina taratibu za kupnda mtu!! Anapofanya vizur msanii yeyote yule anastahil pongez, pia unapoona mtu anaelekea kusiko c vyema kukumbatia u team!! Jamaa kaelezea vizuri sna kuwa uwezo wa jamaa utashuka kama sipokua makini na wakumuangusha ni miteam isiyo ya maana! Diamond haimba kama zamani, hana hisia za kimuziki kama zamani! Ww tim ukisikia nyimbo tu ya diamond bac hata akiwa hajafanya vizur unatoa pongez! Tuache ushabiki wakati mwingine tujue kabisa hawa vijana wetu kuna wakati wanateleza kw hiyo lazima usema ukwl! Na ndivyo kesho atalekebisha tatizo! Diamond ni binadam so kuna wakati anakosea pia, tuache matim tushabikia muziki kuitangaza Tanzania!
Asante sana mkuu,umeongea points sana.
Ila hawa watu hawatakuelewa.
 
Kwanza tambua ya kuwa wimbo wa mwisho wa diamond kutoa ni salome so ungeanza kumjudge kuanzia hapo kurudi nyuma kuhusu kufananisha kushuka kwa diamond(kitu ambacho sikweli) na kushuka kwa mr.nice hebu jaribu kujiuliza mr.nice alikuwa on top kwa muda gani na diamond yupo on top kwa muda gani then angalia anayoyafanya diamond akiwa on top na aliyofanya mr.nice wakati akiwa on top halafu pia cheki management ya mond na ya mr.nice ilivyokuwa (sijui kama alikuwa nayo) enzi hizo ukisha linganisha vyote hivyo sasa utakuwa unajua kushuka kwa mr.nice na kushuka kwa diamond ni tofauti
Nimalizie kwa kusema huu msemo unao itwa "diamond huu ni mwaka wake wa mwisho" nilianza kuuskia tangia mwaka 2012 lakini kila mwaka unao kuja unakuwa mkubwa kuliko ulio pita
 
Tatizo hawa team mondi hawataki kusikia wakiambiwa ukweli, ila ngoja tuwaeleze tu wasiposikia basi watajua wenyewe.
Ukweli upi? Wewe si wa kwanza kupiga hizo ramli; hebu pitia hii habari ya mwaka 2013:
Leo Diamond Platnumz kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, ameamua kufunguka kwa undani kuhusiana na shutuma zinazoelekezwa kwake kuanzia kudaiwa kutumia waganga wa kienjeji kuosha nyota yake na scandal zingine. Kuhusiana na mganga anayedai kuwa atamshusha Diamond baada ya kumtelekeza Diamond amesema:
Wakati wewe unaota anguko lake kuna wengine walienda mbele ya TV na kuapa kwamba watamshusha... unaenda mwaka wa nne sasa!! Lakini vile vile ukipitia hapa JF; threads sawa na zako zipo 10 kidogo na ingekuwa kuota ndo kutokea; huyu jamaa asingekuwepo leo hii!!! Lakini vile vile ukipitia hapa JF; wapiga ramli sawa na wewe wapo kwa miaka kadhaa sasa; kwa uchache tu, hawa hapa:
Wakuu sishabikii ,ila I predict nyimbo zote zinazokuja za Diamond Platnumz hazitahit tena,Katoa wimbo unaitwa Kitorondo,
NB:ASIMDHARAU ALIKIBA WOTE WANAFANANA TU
Kama wewe ni mfuatiliaji wa muziki piga hesabu mwenyewe tangia kutoka kwa Kintorondo hadi leo! Mwingine huyu hapa:
Naam na hili ndilo anguko rasmi la msanii diamond
BELIEVE IT OR NOT…..HII NDO CROWD ILIYOKUWEPO KWENYE SHOW YA DIAMOND JIJINI MWANZA-TANZANIA SIKU YA JANA TAREHE 14-2-2013……. Intresting!.......Ukumbi unaitwa Gold-Crest.......Photo Credit FORTUNATUS MKARE
Ni zaidi ya miaka 3 imepita sasa tangu hiyo ramli ipigwe! Mganga wa kienyeji mwingine huyu hapa:
Anguko la Diamond limefika,hana baraka za baba, kwa hiyo hawezi kusonga mbele hata kama taifa zima litamuombea, DIAMOND KAMUANGUKIE BABA YAKO, OR ELSE YOU'RE GONE AWAY.
Miaka miwili imepita tangu jamaa achukue kuku mweupe na paka mwenye chongo kufanikisha ramli! Akaja huyu nae:
Anguko la Diamond Platnumz
Kama wewe ni mfuatiliaji wa trend ya muziki hapa nchini utagundu hivi karibuni heshima ya diamond kimuziki imeshuka sana ila kinachoweka juu ni tetesi na magazeti na ni habari zisizohusiana na muziki,
Mwaka umekatika lakini ndo kwanza anazidi kupiga shows kwenye nchi ambazo hakuna Mtanzania hata mmoja amewahi kufanya shows!
 
Ukweli upi? Wewe si wa kwanza kupiga hizo ramli; hebu pitia hii habari ya mwaka 2013:Wakati wewe unaota anguko lake kuna wengine walienda mbele ya TV na kuapa kwamba watamshusha... unaenda mwaka wa nne sasa!! Lakini vile vile ukipitia hapa JF; threads sawa na zako zipo 10 kidogo na ingekuwa kuota ndo kutokea; huyu jamaa asingekuwepo leo hii!!!
Mkuu maona umeamua kuumua na kumzika kabisa huyu mpiga ramli hawezi kurudi tena humu
 
Hiyo avatar nimeitoa hapa kijijini kwetu.
Waelekeze jinsi ya kulima maharagwe, karanga, njegere ili waweze kupunguza vitambi. Si kula nyama na samaki kunasaidia. kwetu hatuli nyama na samaki ila hivyo vitu vimefanya watoto wasiwe na hiyo hali.
 
Huyo jamas ni hater , hajui hata anachokiongea
Nachokiongea ni hiki:

Copy
1479900393482.png

Paste
1479900417413.png
 
Back
Top Bottom