Anguko la Makonda

Mkuu, nakubaliana na wewe 100% kwamba huenda Makonda akarudi, na pengine akapewa madaraka makubwa zaidi. Lakini kuondolewa kwake ni kama a wake up call: kwamba cheo ni dhamana na kinaweza kukuponyoka wakati wowote. Haswa cheo cha kuteuliwa na Mkuu wa nchi.

Mabega yake yalitaka kufikia maskio yake. Ni kama mtu aliyepewa madaraka makubwa bila maelekezo (job description. Matokeo yake, akawa anajiingiza kila sehemu kama nywele. Mara anataka kushughulikia suala la wakina mama waliotelekezwa na wazazi wenzao, Mara suala la mirathi, mara suala la migogoro ya ardhi n.k. Mwisho wake akaanza kugombana Mawaziri husika wenye dhamana ya hayo mambo. Nadhani alinza kuhisi kwamba D' Salaam ni Jamhuri ya peke yake.

Ndio maana, ilipofikia wakati wa kumtosa, wahusika hawakufikiria hata sekunde moja.

A slap on the wrist ni nzuri sana. Inakukumbusha kwamba cheo ni dhamana na kwamba everyone is replaceable.

D' Salaam iliwahi kuwa na mkuu wa mkoa; mtoto wa mjini, na member wa club ya Saigon (Marehem Ditopile). Kwa masikitiko makubwa, mwisho wake haukuwa mzuri baada ya kumpiga risasi na kumfumuwa kichwa kondakta wa daladala. Power is contagious. Mungu bado anampenda Makonda. Natumaini akipewa madara mapya atajua jukumu lake na atajifunza kuwa humble.
 
Nimekutana naye mara kadhaa kule masaki mwisho jirani na police post.

Kwenye uwanja ule wa mpira yupo naye anapiga tizi...umeona peach ile walivyoitengeneza.

In short mwana fungu lipo mambo yake yanakwenda kama kawaida tu.

Ova
Ila kanenepa sana bila mpango, kwenye ule majengo wa ghorofa 8 unaoendelea kujrngwa ni wa kwake? Kila siku naikuta Range Rover Autobiography imepaki, lete maneno.
 
Sasa huyu kitu gani kitakacho mtisha wakati amekuwa akijaza mchanga malori hapo Kawe. Konda wa daladalá. Mama yake amekuwa akienda kumwangilia chuoni wakati ndala zake zimekatika.
He never hide his past, he often reveal his past proudly.
 
Thubutu

Makonda hana uwezo wa Kufika hata Robo yangu

Exposure
Namzidi sana

Mali
I have almost €2Milion

Elimu
PhD

Yeye ana Kipi?
Au kwakuwa tunatumia majina fake
Ungee kaa kimya bila kutaka how worth are you, comment hii usinge iona, kama €2 million ndio uwezo wako, usishangae Makonda anaweza kukuzidi uwezo .
 
Pesa atazitoa wapi? Au kamshahara ka ukuu wa mkoa
Huyo jamaa ni haramia, amedhurumu sana pesa matajili na kuwapira magari.

Asingekuwa mtotopendwa wa cage one leo huyo Bashite alipaswa kuwa chakula ya Takukuru muda mrefu tu.
 
Huyu mtu hawezi kurudi tena, naomba uniamini. Zero brain ameshindwa kuutumia vizuri ukaribu wake na JPM.
Ametumia vibaya ukaribu wake na Jiwe kuwapora matajiri magari, fedha kwa kisingizio cha "dawa za kulevya" au kwa kisingizio kuwa "Mzee amenituma anataka hela".

Mwaka 2019 aliwadanganya GSM wale wafadhili wa Yanga kuwa Jiwe anataka ajengewe nyumba. Kweli GSM wakamuamini na wakajenga. Baada ya hapo GSM wakawa wanataka Jiwe mwenyewe akazindue nyumba hiyo lakini Bashite akawa anawapotezea. Ndipo kwa namna yao wakamfikia Jiwe na mchezo ndipo ulipoharibika kwa vile Jiwe hakumtuma Bashite. Atabakia tu kutumia hela alizo dhulumu.

Kuporomoka kwa Makonda kumeenda sawa na Mayor Benjamin Sitta na DED wa Kinindoni Aron Kajurumjuli. Utatu wao ilikuwa unapiga hela za miradi ya Coco, Machinjio na Stendi
 
Kuna watu wanatamani Makonda arudishwe ili waweze kuendelea kulalamikia huu utawala,k una watu huku kulalamika washazoea.
 
Anaishi + anakula bata tu
Bora watu sahivi wamchunie tu
Hajapoteza kitu

Ova
Kwani kuna wangapi wanaokula bata zaidi yake, tunachoangalia ni yeye kutokuwa na uwezo tena wa kutumia madaraka ya umma kwa manufaa yake binafsi.
 
Mungu halipi mbali wewe alitamba sana kipindi chake utazani hajawahi kuwa otingo wa magari ya mzee mabina kipindi hicho RIP hayati mabina
 
Your sarcasm knows no bound!
But how can it be sarcasm?

Those were actual actions undertaken by the individual, and they appeared to have pleased the sit of power at the time.

So he was rewarded for his efforts at that time by being appointed District Commissioner.

Prior to those actions, few people knew there existed a person by the name of Paul Christian Makonda.

Enter John Pombe Magufuli, and for quite different reasons, Makonda's fortunes changed drastically for the better!
 
Mungu halipi mbali wewe alitamba sana kipindi chake utazani hajawahi kuwa otingo wa magari ya mzee mabina kipindi hicho RIP hayati mabina
Eeenh Heee, Mabina na kipistol chake kuwatishia wananchi wenye hasira!

Kweli CCM imepitia parefu. Sijui kuna mangapi ambayo bado haijatuonyesha!
 
10. Aliwahi kulitukana bunge hadi likamkalisha kikao cha kuliomba samahani.
11. Aliwahi kumtukana Askofu Gwaji hadi akaitwa Bashite.
12. Aliwahi kumfukuzisha kazi Nape hadi akanyooshewa mguu wa kuku na wana TISS.
13. Aliwahi kuwakusanya wanawake wote wa Dar waliotelekezwa na waliowatunga mimba hadi wakataja aliyewahi kuwa PM.
14. Aliwahi kufukuzia Dar es Salaam nzima gesi ya kuua vidudu vya corona hadi rais akakasirika.
15. Aliwahi ....... nk nk. hadi wajumbe wakamfyanyizia mambo yao.
 
We kijana huyo ndio katibu mkuu ajaye wa ccm , huna habari ?
 

So Makonda aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na JPM au KIKWETE. Hivi nyie watu mnataka kutuambia hamna yajifichayo. Niwaambie Siri moja. Ukiona mtu anamuda wa kumuattack mtu ambaye hana hata uhusiano naye , hasa behind ya keypad, jua tu huyo mtu Ana matatizo Makubwa sana kuliko anayemwandika. Nafsi yake inatafuta faraja katika kuwaandika wengine hata asiowajua.
 
Inaonekana huijui CCM wewe...wanajua kulindana hao

Huku na kule utashangaa siku jamaa anapewa hata ubalozi wa Malawi
 

Mkuu umesema wewe una PHD na exposure na hela ya mboga. Umewezaje pata muda wa kumuandika mtu ambaye Ana maisha yake. Au mfanyakazi Wako wa ndani asiyena „. Exposure“ kaiba simu yako. Mana mwenye hela plus PHD huo muda wa kuandika kitu kisichoakisi ongezeko la Hizo noti usingeupata. Muonye mfanyakazi wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…