Anguko la Millard Ayo liko karibu sana

Anguko la Millard Ayo liko karibu sana

Na tatizo la Bongo hata ukitoa ushauri wa premium standard; kama hutaambiwa 'si mwenzetu', utaambiwa una wivu.
Anyway! Tamaa zilimponza fisi.
 
Binafsi nilikuwa mpenzi mno wa hii blog, lakini toka mwaka Jana mwanzoni mpenzi yangu yalitoweka kabisa.

Kuna sababu kadhaa zilizopelekea kuichukia hii blog ambazo ni Pamoja na:

Habari zake Karibu zote amekuwa akiweka video badala ya kuandika hali inayopelekea bundle kuisha haraka sana

Pia Millard Ayo licha ya kutuwekea Video katika almost Kila habari anayoposti, robo ya hiyo Habari unakuta na video ya Tangazo la biashara ambalo ni video pia

Achilia mbali hilo hata Habari anazopost nyingi ni za Abunuasi yaani kufikirika kwa maisha ya mtanzania wa kawaida hazina msaada mathalani NYUMBANI ghari duniani - Simu ya Gharama zaidi na mengine mfano wa haya
Anguko ni lako wewe usio na bundle... Ulitaka yeye akununulie kifurushi? Pambana na umaskini wako na uache wivu
 
Jf yatosha kwingine panini?nikatafute shombo tu
 
Anaongeza Views Youtube ili mshiko uwe mrefu mkuu na pia kwenye video hizo anakula matangazo ya Vodacom/GSM.
 
Mleta hoja

Wewe sio target ya millard.... Alishamalizana na watu kama wewe... Anajiongeza
 
Mimi Tatizo langu na milad ayo ni : apple yake haifanyi kazi kwenye Iphone . Ni mpenzi wa ‘Nyumba’ na ‘simu’ ghali Zaidi Duniani
 
Niliwahi kusoma mahali Millard huyu alizawadiwa kimataifa kwa SBB alikuwa na viewers wengi internationally,nilishangaa mpaka Iran alikuwa nao wengi tu.sasa nashindwa kuelewa mjinga in yupi!!!
Waliomzawadia ni kina nani? Na je huko alikopata viewers wengi kwani hakuna wajinga pia? Umefanya research hao wanaofuatilia blog yake ni watu wa aina gani? Binafsi sifuatilii hiyo blog uchwara sababu 99% ya habari zake ni hovyo na copy and paste!
 
Matangazo ndiyo biashara yenyewe. Hii ni ishara kwamba kijana anapiga pesa balaa
 
Nilisha unstall siku nyingi kwenye simu baada ya kero hiyo kuzidi
 
Huwa anatoa maelezo yanayohusu tukio husika then anaweka video kwa uthibitishi zaidi.
Tuchape kazi tuache majungu!
 
unai

unaitwa msigwa(nahisi ndio jina la ukoo) alafu unasema mkoa wenu?wew ni mkimbizi tuu ndani mji wa mawe na milima.....muulize mzee wako akina Mnogelichuma ni akina nan wilaya ya iringa vijijini ukianzia Mgera/luganga,kiwele,mfyome,kilendu,village 4 nk
Hahahahha bhe mkwamisi, uli mdesi swella. Uveve mnyalukolo ve lidugulu lya whi?
 
Awali ya yote nakiri kabisa mimi ni mfatiliaji mkubwa sana wa millard Ayo.

Katika sakata linaloendelea kati ya wababe wa Fitna WCB vs Clouds nimejikuta nacheka tu baada ya kuona Millard naye amekata kupost habar za WCB ambazo 85% zilikua zinampa faida sana.
Hapo ndo nimeprove kumbe jamaa hamna kitu still anapangiwa cha kupost kwenye Media zake ambazo mimi na wewe tunajua kabisa ni zake binafsi.....tuendelee kuangalia nani ataibuka Mshindi japokuwa naona kama clouds wanatumia nguvu sana kupambana na WCB wakati wakina Chibu wamewapotezea kabisa Clouds.
 
Back
Top Bottom