Kwa miaka kadhaa ndugu Nyani Ngabu au( a boy from USA [emoji631] ) kama anavyojiita mwenyewe amekuwa ni mtu maarufu humu jukwaani haswa kwa mbwembwe zake za kuongea kiingereza cha ndani zaidi kiasi kwamba kama kiingereza chako ni cha kuunga unga huwezi kumuelewa kamwe vitu anavyoviandika .
Kwa miaka hiyo kama mtu ukizungumzia kuhusu JF ilikuwa si rahisi kutomjua huyu mtu ila kadri siku zinavyozidi kwenda umaarufu wake unazidi kufifia kama moto wa nyasi .
Ngabu alikuwa anaongoza kwa messages nyingi humu jukwaani lakini kwa sasa ameshapinduliwa tayali na ameachwa mbali sana
View attachment 511524
Pia kwa upande wa likes ameachwa mbali saaana ,kwenye upande wa likes yeye ni mtu wa 18 na muda sio mrefu atatupwa kwenye wale watu 20 wanaoongoza kwa kuwa na likes nyingi
Namba moja inashikiliwa na Bitoz akifuatiwa na Jimenna ,Shunie ,Mussolin5 na Quigley
View attachment 511525
View attachment 511528
Ni kazi kubwa sana waliyofanya hawa makapuku kufagia fagia kwa kweli ,maana ukiangalia wana messages chache ila likes nyingi sana
Bila shaka baada ya miezi kama sita mpaka miaka miwili na nusu umaarufu wa Ngabu utakuwa ni wakaida sana kama 10% tu basi hasa kwa wale wageni ndio hawatamjua kabisaa .
Bye bye Nyani Ngabu wakati wako umeshaisha tayali.