Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Nikiwa mwanaCCM kindakindaki nimepokea kwa furaha lakini kwa tahadhari kubwa haya matokeo ya Uchaguzi mkuu uliofanyika 28 Oktoba 2020.
FURAHA
Ni wazi Chama Cha Mapinduzi kilijikita kwenye kunadi ilani yake ya uchaguzi. Ushindi huu umetokana na kuungwa mkono kwa ilani yake ambapo vyama vya upinzani hususani chama kikubwa cha upinzani walijikita kukosoa dhima nzima ya maendeleo na mafanikio ya rais aliyepo madarakani huku wakiwataka kuwaaminisha wapiga kura kwamba CCM haina tofauti na mkoloni ambaye naye alijenga miundombinu ya barabara na reli wakisahau kutofautisha malengo ya mkoloni kujenga miundombinu ilikuwa kufanikisha extraction ya resources kupeleka kunakohitajika.
TAHADHARI
Tunapokea matokeo haya kwa tahadhari kubwa hasa ikichukuliwa ushindi huu unapeleka chama changu cha CCM kutokuwa na mpinzani kabisa kwa miaka mitano ijayo. Nikikumbuka mwaka 2019 wapinzani walikosa nafasi nyingi uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji hivyo mwaka huu ingewezekana wapinzani wakajitutumua kupata kura nyingi na kupata viti kadhaa vya uwakilishi kwenye Bunge na Baraza la Uwakilishi.
Ukichukulia bado ndani ya CCM kuna minong'ono kuhusu taratibu zilivyokiukwa kuwapata wagombea mbalimbali wa nafasi za ubunge na udiwani huku waliopitishwa wengi wao walitumia rushwa kupata kura za wajumbe. Pamoja na ahadi za mgombea wa CCM kuwa waliocontest watulie watapata nafasi serikali ijayo lakini bado kuna wale wafuasi ambao wanaona kabisa kilichotendeka siyo sahihi na kuwaachia maumivu moyoni.
Tahadhari kubwa ichukuliwe hapo kwa sababu inawezekana waliochaguliwa wasiwe watendaji na wabunifu wa kutatua kero za wananchi hivyo kusababisha ombwe la uongozi. Mfano mzuri kwenye kata ninayoishi ambapo Diwani aliyemaliza muda wake ndiye aliyerudishwa kupitia kura za wajumbe huku wakijua kabisa hakuwa mtekelezaji wa ahadi na ilani zaidi ya kugubikwa na kashfa nyingi za aibu kwenye uongozi wake hivyo ushindi wake ni kuirudisha kero kubwa ya wananchi kwenye uongozi.
NINI KIFANYIKE
Matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2020 umeleta mtazamo tofauti sana kwenye jamii ya siasa nchini na wafuatiliaji wa siasa za Tanzania.
Inawezekana kabisa ni kauli ya wapigakura kuonyesha kukerwa na kuchoshwa na mwenendo wa siasa za upinzani nchini kujikita kupinga, kukosoa na kuhujumu juhudi za serikali iliyopo madarakani kuwaletea maendeleo wananchi.
Kupitia matamko ya upinzani Bungeni kwamba tunahitaji kufufua mashirika yaliyokufa kama ATC na imiliki ndege zake na hata kujenga miundombinu ya barabara, reli, madaraja, viwanja vya ndege na bandari. lakini ilipokuja serikali ya awamu ya tano ikaanza kutekeleza kwa nguvu zote miradi ya maendeleo huku ikianza kwa kubana matumizi na fedha hizo kupelekwa kugharimia miradi hiyo wimbo ukabadilika ukisema hayo yote siyo wananchi wanayohitaji bali health services and facilities.
Lakini wakasahau kwamba serikali imejenga mahospitali na vituo vya afya nchi nzima huku ikiboresha hospitali zilizopo na kuzipandisha hadhi. Haya yote yalikuwa katika agenda za wapinzani bila kuzingatia kwamba maendeleo yaliyohaidiwa yalikuwa yanaonekana kwa macho na hata uendelezwaji wa miradi ya maendeleo vilikuwa ni vitu vinavyoonekana na wapigakura.
Baadaye wapinzani waligeuza wimbo wakisema ubanwaji wa uhuru wa maoni ndiyo kikwazo kikubwa cha ustawi wa nchi yetu. Waliweza kutumia lugha lukuki hata za matusi kuishinikiza hoja hii kwenye jamii. Wanaharakati wa kijamii waligeuka kuwa wanaharakati wa kisiasa hasa wakiegemea sauti za upinzani ili kuiangusha serikali ya CCM kwenye uchaguzi huu mkuu uliopita.
Hayo yote yalikuwa yanatendeka kwa kisingizio cha kuwasemea wapigakura ambapo hata ziliendeshwa harakati kubwa ndani na nje hata kufikia kuomba nchi isipewe fedha za miradi ya maendeleo ambapo wafaidika ni wapigakura wanaosemewa na wapinzani wakisaidiwa na wanaharakati wa kijamii.
Sauti au maamuzi ya wananchi kwa usahihi kabisa tunayapata kupitia sanduku la kura. Kura hizi zimeleta taswira ya kukataliwa kwa harakati za wanasiasa za upinzani nchini.
Humu JamiiForums kuna wataalam mbalimbali na wachambuzi mahiri wa kisiasa, je ni wakati muafaka sasa kwa wanasiasa kujipanga na kuanza upya kujenga siasa makini zenye mwelekeo mbadala lakini chanya kwa maendeleo ya nchi yetu.
Wapinzani waliopo walijikweza kuwa ndiyo majibu ya kero zote za wapigakura hata ikafikia tukapata wanasiasa waliojiita wabunge wa kitaifa hivyo wakatelekeza majimbo yao na kuwa wasemaji wakuu wa vyama vyao bila kuzingatia agenda zilizowapeleka bungeni.
Tanzania bado inahitaji sana siasa za upinzani lakini ziwe na majibu taradadi kwa kero za nchi. Wanasiasa wajikite kwenye kuiendeleza nchi na jamii nzima wasiwe wanahujumu mikakati na miradi ya serikali kwa watu wake. Chama kinachoshinda madaraka huwa kinarithi mafanikio, matatizo na uhalisia wa nchi kwa minajili ya kusonga mbele.
Wapinzani walijijengea uadui na serikali hasa pale walipoanza kushambulia kwa lengo la kudhalilisha vyombo nyeti vya serikali kama.vile ulinzi na usalama, afya, rasilimali na kadhalika.
Swali kwenu wanabodi,
TUANZE KUJENGA UPYA SIASA MBADALA?

Upinzani usipofanya haya basi usahau kukamata dola:
NAWASILISHA. POVU RUKSA.
- Kushinikaza au kudai katiba mpya. Vyama vya upinzani vinatakiwa kuwa na umoja kwa ajili ya kudai katiba mpya. Katiba ya nchi hii ndiyo kikwazo namba moja cha upinzani kuendelea kusindikiza tu wenzao ccm kila uchaguzi hata pale inapoonekana kabisa wananchi wanataka mabadiliko kupitia vyama vya upinzani. Ningemuelewa sana zitto, Lissu na hata jasusi bobezi lisilojua kujieleza mbele ya kadamnasi (Membe) kama safari zao za ndani ya hii nchi na hata safari zao za kuzunguka ulaya na marekani wangekuwa wanatafuta support ya kuiwezesha katiba ya Tanzania kubadilishwa.
- Kujenga vyama vyao kuanzia ngazi za vitongoji/Vijiji/Mtaa (grassroot level) ili kupata mtaji wa wanachama wa kudumu na pia kuwawezesha sera za vyama vyao kuwafikia wananchi wengi kwa urahisi zaidi badala ya kusubiri siasa za mihemuko au uanaharakati ambazo huwa hazina uhalisia kabisa. Wawe na media kama magazeti ya vyama vyao, gazeti la upinzani, redio na hata television chanell kwa lengo la kupeleka sera zao kwa wananchi kwa urahisi badala ya kuwa na njia moja tu ya mikutano ya hadahara.
- Kufanya mabadiliko ya uongozi katika vyama vyao kwa lengo la kuondoa dhana potofu ya chama kuaonekana kama kinamilikiwa na mtu/watu wachache au kundi fulani katika jamii na hivyo kuleta taswira kwenye jamii kwamba hicho ni cha watu au jamii fulani.
- Kuwaandaa viongozi/wagombea mapema ili kuwapa muda wa kutosha kujua kero au shida za sehemu wanazoongoza/kugombea ili kutafuta njia bora za kutatua kero za sehemu husika ambazo ndizo zitaunda ilani ya uchaguzi wa vyama vyao.
- Kuandaa ilani za uchaguzi zinazoongelea kwa kina ni kitu gani wanataka kuwafanyaia watanzania na kwa namna gani, wapi, na ndani ya muda gani. (a detailed party election manifesto).
- Kuwa na vyanzo vya mapato: Wapinzani hasa hivi vyama vikubwa vya upinzani vinatakiwa kubuni na kuanzisha vyanzo vya mapato ili kuviwezesha vyama hivyo kujijenga badala ya kutegemea ruzuku toka serikalini tu.