Uchaguzi 2020 Anguko la Upinzani Tanzania. Tuanze upya

Uchaguzi 2020 Anguko la Upinzani Tanzania. Tuanze upya

Nadhani hawa wapinzani uchwara walijisahau wakadhani vismart phone na vikompyuta vyao ndivyo vinapiga kura hapa mtandaoni. Wenzao wanamtaji wa wanachama huko uraiani wao wanajifanya kuwekeza kwenye mitandao ya kijamii ambayo ambayo bibi na babu zao huko vijijni Mpitimbi na maneromango hawaijui. Ndio maana nawambia kama wasipo rudi kwa wananchi mashinani na kwenye mtaa wakadhani chama kinajengwa kwenye mitandao wataendelea kuchezea vitasa vya ccm tu!
 
Magufuli ameshaongea na kuahidi mara nyingi kwamba muda wake ukiisha wa kukaa madarakani kwa mujibu wa sheria hatozidisha hata dk 5, ataondoka na katika kulionyesha hili kwa mfano wafuatilie wafuatao:
Juma Mkamia alianzisha hoja ya Magufuli kuongezewa muda madarakani, nadhani unajua aliko.
Ally Kessy aliikoleza hoja ya Magufuli kuongezewa muda wa kukaa madarakani, nadhani unajua aliko
Kangi Lugola akamfananisha Magufuli na yesu, nadhani unajua aliko.
Hoja ya Magufuli kung'ang'ania madarakani nadhani mnaikuza na kuishikilia kwa kuwa hamna hoja tena zenye mashiko mnazoweza kuja nazo kumpinga so nikuja na uzushi. Bado mnashangaa kwa nini wananchi wamewakataa? Basi hamjifunzi
Hata Kagame alisema hataongeza muda wa kukaa madarakani. Museven pia alisema hivyo hivyo. Kwa haya matukio yanayoendelea nchini tujiandae kwa lolote
 
Wanatakiwa wawe imara tu Lakin wamejifungia ndani loo
Haiwezekani kuwa imara bila support ya umma. Hivi kwa hali ya kawaida mtu kama Lissu amethubutu kuja kugombea urais pamoja na kushambuliwa kwa risasi zaidi ya kumi na sita, Mbowe pamoja na shuruba zote alizopitia ikiwa ni pamoja na kuwekwa ndani zaidi ya miezi mitatu, biashara zake kuhujumiwa na yeye binafsi kishambuliwa bado amesimama imara na kushiriki uchaguzi.
Unataka wawe imara kiasi gani?
Na wao ni binadamu kuna kipindi wanashindwa hasa pale wanapokosa support ya wananchi hasa wapenda mabadiliko. Nadhani tuwape moyo kwa jinsi walivyojitahidi kupambana pamoja na ukandamizaji wa hali ya juu wanaopitia na sio kuwabeza na kuwakatisha tamaa
 
Haiwezekani kuwa imara bila support ya umma. Hivi kwa hali ya kawaida mtu kama Lissu amethubutu kuja kugombea urais pamoja na kushambuliwa kwa risasi zaidi ya kumi na sita, Mbowe pamoja na shuruba zote alizopitia ikiwa ni pamoja na kuwekwa ndani zaidi ya miezi mitatu, biashara zake kuhujumiwa na yeye binafsi kishambuliwa bado amesimama imara na kushiriki uchaguzi.
Unataka wawe imara kiasi gani?
Na wao ni binadamu kuna kipindi wanashindwa hasa pale wanapokosa support ya wananchi hasa wapenda mabadiliko. Nadhani tuwape moyo kwa jinsi walivyojitahidi kupambana pamoja na ukandamizaji wa hali ya juu wanaopitia na sio kuwabeza na kuwakatisha tamaa
Basi wangetoa hata tamko wamekaa kimya tu kweli najua wamejitahidi sana na kujitoa
 
Kwa kifupi ni dhuluma.

Hata Trump haweze kushinda kwa asilimia 99
 
Upinzani gani wakupinga kila jambo zuri,kwa jinsi walivyo nisahihi wafutike kabisa.
Kwanza kunamambo mengi waliyofanya mpaka wakapoteza matumaini kwa watanzania wengi.

1)Taifa lilipopata msiba wa Maige na Mkapa R.I.P walitumia mudawao kukebehi na kukashifu misiba hii ya viongozi wetu.

2)Baada ya Kenya,Rwanda,Zambia,Malawi kufunga mipaka wakidai Tanzania tuna Corona JPM nae alifunga mipaka walimbeza sana,cha ajabu na wao waliungana na misimamo ya hayo mataifa kunyanyapaa taifa lao la Tanzania.

3)wakati JPM akihimiza njiambalimbali za kupambana na Corona na kijifunza kuishi na Corona,hawajamaa walibeza waziwazi tena kwasauti pana,walisambaza video na takwimu feki kuwapa watanzania hofu.

4)walisambaza picha kubeza nyumba za udongo vijijini kuwa na umeme.

5)awataki kusikia miradi mizuri ya taifa kama sgr,bwawa la kufua umeme,vivuko,barabara,umeme mpaka vijijini n,k.

6)taifa likipata janga dogo tu mfano kama mafuriko,jamaa wanatumia janga ilo kuinanga serikali na taifa kwaujumla.

kwa tabia hizi na zingine nyingi,sioni umuhimu wa kuwa na upinzani wa namna hii Tanzania.
 
John Pombe Magufuli - Kura 12,516,252

Tundu Antipas Lissu - Kura 1,933,271

John Pombe Joseph Magufuli amechaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

ITV

Imeisha hiyo!!!!
 
Hayo mambo yamewagombanisha na wapigakura.

Inaonesha hawapo tayari kujifunza, kinaweza kuinuka chama makini ambacho kikawa na fikra mbadala wa kuipeleka agenda ya maendeleo ya kiuchumi kiushindani ili chama tawala kipate mshindani wa kweli
 
Yaani mmekosa hata aibu! loooh! Hasbiallah!
Mkuu ukisoma kwa makini utaelewa nini nimemaanisha.

Kikubwa ni upinzani kujitathmini kama wapo sahihi njia na mbinu wanazotumia au wajikite kwenye kudeal na maendeleo ya nchi na watu wake
 
tatizo mnadhani upinzani ni kina mbowe, zitto na viongozi wengine waandamizi. think twice.

upinzani ni sisi mnaotupiga risasi za moto wakati tupo mikono mitupu. yaani ipo siku mtatia akili mbona. endeleeni tu na upuuzi wenu.
 
Tuanze hapa
Screenshot_20201031-055833_1.jpg
 
Back
Top Bottom