Anna Abdallah naye ni fisadi?

Anna Abdallah naye ni fisadi?

Huyo mgawaji na mfanya biashara aliebahatika kwa msekwa hana mpya kabisa, tena akae kando atuanchie nchi yetu, kama hakula vya kutosha enzi yake basi mwambieni nimesema kuwa hakuna nafasi hiyo tena kwa generation yetu.....
 
Sorry guys to bring this up. Hiyo list ya wanaume inatisha, this can tell us what kind of person this Bibi is! Amewapanga kweli kweli
 
Kamalaya hako kamwanamke ka-Anna Abdallah Mhavile Kawawa Msekwa..............nasikia hata kuna tuvijana nato tunajilia kidogokidogo, kanavikamatia tu!!!!

Mmsamehe bibi wa watu.Akiwa kijana alipoteza muda na wanaume mbalimbali sasa amezeeka atafanya nini??? Kwenye list ongeza mholazi aliyezaa naye mtoto wakiume.
 
Anna Abdallah ana historia ndefu ya utumishi serikalini (ukuu wa wilaya, mkoa n.k) na uongozi wa kisiasa (ubunge, waziri wa uhamishaji makao makuu, waziri wa ujenzi, waziri wa afya, uenyekiti wa u.w.t n.k.). Sijamsikia mtu akimkosoa kuhusu utendaji wake humo bali watu ambao inadaiwa alitembea nao, zaa nao na kuolewa nao! Yaani kweli kipimo cha ufanisi katika uongozi wake ni watu aliotembea nao? Kweli sisi ni misogynists!
 
Katika miaka ya elfu mia tisa na sabini mama huyu alikuwa mkuu wa wilaya ya Magu huko Mwanza. Niliwahi kuambiwa kuwa wakati huo alitoa maamuzi fulani ambayo yaliwafanya wanyantuzu wamshikie vibuyu usiku na kumnyanyua kutoka chumbani kwake akiwa amelala na kumtupa kwenye viwanja vya hadharani bila yeye kujitambua. Kutokana na kufanyiwa kitendo kile ndipo Nyerere akamliwaza kwa kumpandisha cheo na kuwa mkuu wa mkoa mmoja huko kusini. Nashangaa kuwa tangu wakati huo hadi miaka hii ya elfu mbili bado anategemea kuwa watu wanaishi kwa fadhila na kutishana.
 
Ndiyo hiki ninachokizungumzia. Innuendos-alitoa maamuzi fulani ( kwani kutokukubalika kwa maamuzi na sehemu ya jamii kuna maana kuwa ni mabovu?), ushirikina-( wanyantuzu walimfanya mabaya), upendeleo ( Nyerere alimpandisha cheo kwa sababu ya huruma!). Hivi kweli Nyerere alishindwa kumhamisha kwa cheo kile kile hadi ampandishe cheo? Tunamlaumu kwa kutoa vitisho wakati ninavyoelewa mimi ni kuwa yeye ndiye aliyekataa kutishika na kuhukumiwa kwa jumla! Huyu mama alikuwa waziri wa ujenzi mbona sijasikia scandal zake kutoka huko? Kuwa alijiuzia nyumba au alichukua kidogo kwenye miradi hasa tukiangalia kuwa wenzake wamekumbwa na hayo. Huyu mama alikuwa waziri wa Afya mbona hamtuambii alifanya kibaya gani huko? Tunabaki kumhukumu kwa mambo yake binafsi. Kama alitembea na wote hao, ni uamuzi wake kama mtu mzima na a hao aliotembea nao. Tuache character assasination na tuangalie utendaji.
 
Chama cha ccm kina mafisadi akiwemo uliyemtaja!
Walichota mabilioni yetu na hawataki kuwakamata mafisadi ndani ya chama kwani ni kweli kuwa...ccm ni chama cha mafisadi!
 
Anna Abdallah ana historia ndefu ya utumishi serikalini (ukuu wa wilaya, mkoa n.k) na uongozi wa kisiasa (ubunge, waziri wa uhamishaji makao makuu, waziri wa ujenzi, waziri wa afya, uenyekiti wa u.w.t n.k.). Sijamsikia mtu akimkosoa kuhusu utendaji wake humo bali watu ambao inadaiwa alitembea nao, zaa nao na kuolewa nao! Yaani kweli kipimo cha ufanisi katika uongozi wake ni watu aliotembea nao? Kweli sisi ni misogynists!

Mkuu, inawezekana uko sawa.

Au sio sawa.

Kabla ya soo la Richmond, Lowassa aliwahi kukosolewa katika historia yake ya Uwaziri? Na ile miaka, sijui kumi ya AG Chenge, aliwahi kukosolewa kikazi, kabla hajageuka mbogo na kuwa blatantly malfeasant in the later years? Waziri Mkapa aliwahi kukosolewa wakati wote ule yuko surrogate wa Nyerere? Kanali Kikwete wa Wizara ya Nishati kesha wahi kukosolewa enzi zile? Na Mramba wa the '80s and '90s na Director General Mkulo wa NPF, na Waziri wa Utalii, Meghji na mafisadi wengi tu wa leo walio kuwa former "Mr and Mrs clean"?

What's the point? Wote hawa, Fundi, walizawadiwa vyeo vya juu baada ya rekodi zao za huko nyuma zisizo julikana, na wakaja kuonyesha incompetence kubwa kuliko. Kama walikuwa incompetent miaka ya baadae, what should stop me from wondering whether they were just as mafeasant and incompetent in their early careers when nobody said anything negative about them?

Nadhani, Fundi Mchundo, Tanzania hakuna rekodi, utandawazi, kuchunguzana chunguza kikazi, wala performance review za kila mwaka. Ukishapata kazi umepata, labda uharibu vibaya mno. Kiufupi, hakuna unoko. Mafaili ya viongozi wengi hayana madoa. Ni vigumu kujua performance ya mtu Tanzania kwa kutegemea kusikia public criticism. Hatujuia mazuri wala mabaya. Kwa hiyo, kama hujasikia mtu kawa criticized I would not assume anything, positive or negative.

Nani anaweza kuniambia perfomance record ya Foreign Minister Kikwete kwa miaka kumi ya kuongoza ile wizara, na kwenda nyuma toka 1988 Mwinyi alipo mteu deputy Energy minister? Amewekwa namba 11 katika list of shame kwa kusaini SAMAX na Kahama Mining, lakini zaidi ya lalamiko kwamba FFU waliondoa raia sehemu za machimbo aliyotia saini Kanali Kikwete, hakuna details za malfeasance yake. Nani ana faili la Kikwete la Foreign Affairs au Nishati miaka hiyo? Authoritative criticism, sio "dataz" za watu wasio na credibility. Sijaona mimi. Who the heck knows anything about our leaders anyway? Ha ha aaaa...It's a shame.

And then, think about this. Amidst all this total and absolute mystery and darkness due to absence of public records, tunalaumu Wanavijiji kwamba wanawapa kura mafisadi na watu incompetent kwa asilimia 80%. Tunasema ni wajinga sisi, ndivyo tulivyo. Extremely unfair and a total misconception of the details here. What the heck do we know?

Na hili la Anna Abdallah kutembea tembea na Wanaume, kama lipo, ni kweli Fundi, halipimi ufanisi wa mtu. Lakini, labda utakubaliana na mimi kwamba angekuwa yuko nchi za watu, mwanasiasa kama Abdallah watu wangesha mmaindi long time ago. Kwa nini? Wakina Anna Abdallah ni mfano mbaya wa maadili ya jamii.

Ndio maana kila siku nabishana na marafiki zangu kwamba, tusiwe wepesi kusema social values zetu za Kiafrika ni bora kulilo tamaduni za magharibi japo zimebobea kwenye decadence ya kila aina, ikiwemo usenge, pornography industry, high crime rates, divorce rate kubwa, teen sex, pamoja na watoto wanao ua walimu na wenzao madarasani, yote hayo.

Lakini, niambie Fundi, Governor Eliot Spitzer wa New York angejiuzulu kama angekuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanzania amekutwa na ki skandali eti cha ku cheat kwenye hoteli? (Sorry to get a little bit off topic).
 
Ndiyo hiki ninachokizungumzia. Innuendos-alitoa maamuzi fulani ( kwani kutokukubalika kwa maamuzi na sehemu ya jamii kuna maana kuwa ni mabovu?), ushirikina-( wanyantuzu walimfanya mabaya), upendeleo ( Nyerere alimpandisha cheo kwa sababu ya huruma!). Hivi kweli Nyerere alishindwa kumhamisha kwa cheo kile kile hadi ampandishe cheo? Tunamlaumu kwa kutoa vitisho wakati ninavyoelewa mimi ni kuwa yeye ndiye aliyekataa kutishika na kuhukumiwa kwa jumla! Huyu mama alikuwa waziri wa ujenzi mbona sijasikia scandal zake kutoka huko? Kuwa alijiuzia nyumba au alichukua kidogo kwenye miradi hasa tukiangalia kuwa wenzake wamekumbwa na hayo. Huyu mama alikuwa waziri wa Afya mbona hamtuambii alifanya kibaya gani huko? Tunabaki kumhukumu kwa mambo yake binafsi. Kama alitembea na wote hao, ni uamuzi wake kama mtu mzima na a hao aliotembea nao. Tuache character assasination na tuangalie utendaji.

Miaka hiyo ya sabini kulikuwa na purukushani sana aa watu kuhamishiwa kwenye vijiji vya ujamaa. Familia nyingi zilikuwa hazikubaliani na hatua hiyo ya kuhamishwa haraka haraka. Mama huyu mojawapo ya maamuzi yake yaliyomtia matatizoni na wanyantuzu yalihusu zoezi hilo hilo la kuhamisha watu kwenda vijijini harakaharaka. Sijui ni kigezo gani kilichotumiwa na Nyerere kumpandisha cheo mara moja kutoka ukuu wa wilaya hadi ukuu wa mkoa baada ya tafrani hiyo. Wakati huo mama yule alikuwa ameamua kumwaga manyanga kuachana na siasa. Kama mwenzangu unajuwa undani zaidi nifahamishe tu kwani ni muda mrefu umepita na wala swala hilo halikuwa la muhimu sana hadi yeye mwenyewe alipoamua kuturudisha katika siasa za enzi hizo za kutishana. Tukio hilo lililomkuta mama yule pale Magu mimi nalijua binafsi kwa vile nililishuhudia kwa macho yangu makavu ningali mdogo wakati huo; kama na wewe unalifahamu tukio lile vizuri zaidi, basi ni jambo jema kusahihishana tu.

Hata hivyo utakapopata nafasi ya kuongea naye, muulize experience yake kuhusu Magu katika kipindi kati ya mwaka 1973 hadi 1976 hivi. Baada ya kuwa amepata nafasi ya kuwa na nafasi nyingi za kulitumikia taifa hili huu ndio muda wake wa kuonyesha mapenzi yake kwa taifa badala ya kuendeleza mfumo wa kizamani kulindana na kufadhiliana.
 
Kuhani!
Governor Eliot angekuwa ufaransa angepeta. Angekuwa uingereza angetemwa. Angekuwa bongo angeonekana shujaa.

Wote hao uliowataja kwa namna moja au nyingine rekodi zao zimengaliwa (ingawa mara nyingi kupuuzwa). Lowassa ameanza kulalamikiwa toka alipokuwa AICC. Shutuma za kujilimbikizia mali hazikuanza na Richmond. Kikwete utendaji wake akiwa waziri wa nishati nako kumejadiliwa. Kwa nini tusifanye hivyo kwa huyu mama badala ya kukazania masuala ya ngono? Kwa nini badala ya kuipinga hoja yake kwa hoja tunang'ang'ania hayo hayo? Hicho ndicho ninachokipinga, Mkuu. Kila mara kukimbilia kwenye masuala ya chupi anapohusishwa mwanamke! hatuwatendei haki.
 
Vipi kama rekodi Tanzania hakuna?
 
Sijui ni kigezo gani kilichotumiwa na Nyerere kumpandisha cheo mara moja kutoka ukuu wa wilaya hadi ukuu wa mkoa baada ya tafrani hiyo. Wakati huo mama yule alikuwa ameamua kumwaga manyanga kuachana na siasa. Kama mwenzangu unajuwa undani zaidi nifahamishe tu kwani ni muda mrefu umepita na wala swala hilo halikuwa la muhimu sana hadi yeye mwenyewe alipoamua kuturudisha katika siasa za enzi hizo za kutishana. Tukio hilo lililomkuta mama yule pale Magu mimi nalijua binafsi kwa vile nililishuhudia kwa macho yangu makavu ningali mdogo wakati huo; kama na wewe unalifahamu tukio lile vizuri zaidi, basi ni jambo jema kusahihishana tu.

Unataka kutuambia uliwashuhudia wanyantuzu wakimtoa nje ya nyumba yake akiwa mtupu na kumfanya yanayodaiwa? Basi mwenzetu mkali!
 
Sijui kwa undani kuhusu tabia ya Abdallah. Lakini assuming it is true, Mama ni moto chini, niulize hivi:

Mwanamke ambae analala na Wakubwa na anaibuka na vyeo kila kukicha, ni fair ama sio fair kuuliza, je huyu Mama ana qualifations?

Au hiyo ni misogyny?
 
mpaka sasa kwa upande wangu nachukua ccm wote ni mafisadi untill proven otherwise.
ukiangalia vitendo vya wana ccm ni rahisi mno kuwaweka wote kwenye kundi la ufisadi kisha tukaanza kumtoa mmoja mmoja kuliko kufanya kinyume chake.
kwa nini nasema wote mafisadi? kwa sababu kama hawajahusika moja kwa moja na ufisadi, basi wanawaficha mafisadi, au wanawafurahia mafisadi ama kuwatetea.
 
Well said Gaijin,Tuko pamoja!
Huwezi kusema kuna ufisadi halafu ukiambiwa uusafishe unageuka na kusema haupo!
Kweli zama hizi za mawasiliano zimekuwa mwiba kwa serikali.'Unajua ccm bado hawajui hilo!
Zamani aliyekuwa akisikika ni mawlimu peke yake kwenye redio zetu mkulima kwa kupitia RTD!
Na viongozi wanaongea wanalotaka tu!
Hakuna wa kuwakamata kwa kauli zao!
Sasa naona hawa viongozi wana double standards!
Wakiwa bungeni wanasema hiki,wakiwa ndani ya chama story ni nyingine..Na wakiwa nje ya bunge na chama stori ni nyingine...Kauli za kisiasa tu!
Hawajui kabisa wamebanwa pabaya!
Waje tu na hiyo Plan B kama nilivyowaeleza!
 
Sijui kwa undani kuhusu tabia ya Abdallah. Lakini assuming it is true, Mama ni moto chini, niulize hivi:

Mwanamke ambae analala na Wakubwa na anaibuka na vyeo kila kukicha, ni fair ama sio fair kuuliza, je huyu Mama ana qualifations?

Au hiyo ni misogyny?

Hata kama amelala na hao wakubwa na yeye akiwa mkubwa? Mlitaka atembee na dereva wake? Ameolewa na Msekwa akiwa waziri. Kuhoji qualifications zake ni halali. Kuinsinuate kuwa alipendelewa kwa sababu alitembea na wakubwa ni misogyny!
 
Back
Top Bottom