Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Katika kina mama nao heshimu michango yao kwa jamii kama viongozi basi wewe ni namba 1, hoja nzuri ila utekelezaji kwa sasa ni mgumu kama watu wanafikia hatua wanatafuna hadi hela za wahanga wa tetemeko na kuanza kuleta kauli za kibabe kamwe hatutafika.
 
NI WAZO NZURI MAMA. MIKAKATI IANZE KWANI WAADHIRIKA NI WENGI NA NI WATOTO WA MASIKINI.
KWANZA FANYA PRESS CONFERENCE NA WAANDISHI WA HABARI, THEN IFUATE FUNDRISING.
ATAKAYEFIKIRI HILI NI SUALA LA KISIASA MUNGU AMSHUSHE CHINI.
 
Kimsingi siamini kama viongozi wanania njema kuhusu elimu na sioni tatizo liko wapi? mfano NSSF, LAPF, PSPF, PPF, GEPF n.k hawa badala ya kujenga majengo ambayo hayana wapangaji, kila mfuko ukatoa billions 50 zikapatikana billions 250 na kila mmoja akapata million 6 jumla ya wanafunzi 41,667 hawa wote waliyokosa wangepata na tatizo likapungua hata kama siyo kuisha kabisa.
 
Nina wasiwasi na serikali hii kma kweli ina dhamira ya dhati kuinua elimu na kuwasaidia watoto wa masikini. Nakumbuka kwenye kampeni mjini Tabora mjomba alisema hakuna mtoto atakayekosa mkopo. Sasa sijui kma mjomba anakumbuka. Kwenye majukwaa wanasema hii ni serikali ya wanyonge na maskini, Lkn kwenye utekelezaji ni tofauti kabisa. Huu umaskini wetu ndo viongozi wanajivunia.
Waache wakina mama waamuwe wao,
Mboma unaanza kuwapandikiza chuki zisizo za msingi??
Wamesha liona hilo, ukiendelea kufanya hayo kaanzishe taasisi yako

Toka ulijue hilo ulichukua hatua gani??

Mama anaijua siasa zaidi ya unavofikiria, lakini kaweka kando utumbo wooote uhusuo siasa kaamua kuja kuwasaidia vijana kwa staili hii.
Uzuri hata wale mliopanga foleni kumpigia kura bwana yule mliynadi kwa utajiri wake mtanufaika na mama huyu.
Cha ajabu ni mshindi namba tatu wa uraisi anayeonyesha dhamira ya kweli kumsaidia kijana asiyejiweza,

Mama kaamua kutupa utumbo woooote uhusuo siasa kaja kwa utekelezaji zaidi,

Upinzani si ugomvi, anaonyesha namna upinzani safi unavyopaswa kuwa
Ni kulijenga taifa na si kulibomoa ili upate pa kuongelea.

Mama tuko pamoja, naamini yote utakayoyasikia humu ni kuhusu vijisiasa ambavyo nadhani umevizoea, na pengine una uzoefu navyo zaidi na zaidi ya wengi watakavyovileta humu ndani
 
kuchanga tutachanga ila unakumbuka hela ya tetemeko mama yangu ?
Kwani umeambiwa utaichangia serikali ya sehemu fulani??

Hii inaingia kwenye chombo kitakachoundwa na nyie akina mama na usimamizi ni wenu nyinyi wenyewe bodi ya mikopo wataombwa kutoa uzoefu pale utakapohitajika
 
Pesa ya rambirambi wanajua walichokifanya na hii ni laana hta mbele ya Mwenyezi Mungu, bila haya watu wanafanya mambo ya shetani
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa huyu mama na chombo chake kitakachoundwa watazishambulia pesa zao??

Muwache siasa za kijinga kwenye hiki kitu.
Hafu waacheni akina mama wathubutu wao wenyewe, nyinyi si mko bize na kesi na kupotezea baadhi ya vijana.

Usijifanye unajua mambo kuliko mama aliyeanzisha hiki kitu, huenda anavifahamu zaidi ya unavofikiria hivyo vyooote unavyoropoka
 
Mama yangu umetoa wazo zuri,nachelea kusema watu wanaweza kuchukulia unataka kujijenga kisiasa na kumbuka ulikuwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi.
Kumbuka serikali iliyopo madarakani ilisema watapewa mikopo wale tu waliosoma shule za serikali kwa maana ya kuwa waliosoma private wazazi wao wana uwezo!!!???
Uangalie usije kuwa unataka kuichonganisha serikali na wananchi wake maana tunatofautiana uelewa.
Ili kutoingia kwenye mgogoro,ningeshauri uanzie huko huko serikalini kwa kuwaomba wakukubarie wazo lako.
Naamini,watanzania wengi watakuunga mkono na si wanawake tu kama uluvyoainisha.
Watoto wamebaguliwa, kuna watoto wa watanzania na walipa kodi ndo wanafaidi kodi za wazazi wao!!!!
Hili huwa linatia hasira kama sio kusikitisha....
Hongera mama kwa kuja na hili wazo,simama nali,komaa nalo mpaka uone matunda yake.
Haya ndio mawazo ambayo huwa tunayategemea swhemu kama jf
 
Mama uko vzr sana upstairs. Hivi kwa nini Selikali haichoti hizi hekima zako???
 
Mama Mghwira

Nadhani tungeanza kuwa kujiuliza kwanza, ni kwa nini hii serikali imeshindwa kusomesha vijana wa taifa ili.

Inawezekana vipi pesa za kusomesha vijana zikakosekana lakini:

1. Pesa za Bombadier zikasepo
2. Pesa za kulipia Boeing zikawepo
3. Pesa za kujengea Chato Airport zikawepo
4. Pesa za kuamishia serikili Dodoma zikawepo
5. etc

Naamini kabisa hii serikali inayo pesa za kutosha za kulipia vijana wenye vigezo, ila tatizo ni kwamba, kipaumbele cha serikali sio kuwa na wasomi wengi wa Higher Education. Kipaumbele ni kuwa na vijana wengi walioishia darasa la 7 au Form 4, ndio maana huku ndiko serikali imeweka nguvu zake na msisitizo
 
Akhsante sana mama,hoja ya msingi kabisa. Mimi niliwahi kupata wazo kwa ajili ya kuchangia elimu kwa watoto wetu.
Kama serikali inashindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili,basi tuweke taratibu,sheria au kanuni ambazo zitalazimisha halmashauri husika ambapo mwanafunzi anatoka kuhakikisha mwanafunzi huyo anasomeshwa nao. Na hili kuna Halmashauri wanafanya tayari. Pia kama tunaweza kuchangia sherehe mbalimbali ( mpaka arobaini ya mtoto) na kupatikana mamilioni,kwa nini tusichangishane kwa hawa watoto ambao wamekosa mikopo? Utengenezwe utaratibu tu hata wa kutoa asimilia fulani za michango ya sherehe kwa ajili ya kusaidia hawa vijana. Hili kimsingi ni jukumu la serikali,lakini kama pamoja na kelele zote zilizokwisha pigwa kuhusu wanafunzi wote wenye sifa za kupewa mikopo wapewe,bado wahusika hawaonyeshi kujali. Sasa tuache kuwasaidia vijana wetu kusoma kisa tu si jukumu letu ni la serikali au tuwasaidie ili kujenga Tanzania bora ya kesho.
Kipindi cha nyuma kadri tunavosikia stori kulikuwa na tatizo mtoto anafaulu kwenda sekondari lakini alikosa nafasi kwa upungudu wa shule husika!!!

Sekta binafsi ilipoliingilia kati , imefikia hatua kila mtoto anayehitaji sasa kwenda shule sekondari anaenda tena bila shida.


Sasa kwa wazo kama hili hili, mama ameliona akawaazaaa akatoka na jibu hili,
Ameamua kuanzisha chombo cha binafsi cha kutoa mikopo kwa vijana watakao kuwa na sifa za kupata mikopo hiyo,
Uwekezaji katika eneo hili mama kaiona kama fursa na itafika hatua kutokee bodi za mikopo binafsi, kuwe na uchaguzi mtu kuamua kwenda kuchukua mkopo atakapo basi.


Hili ni bonge la wazo jamani mama Anna tumekuelewa.
 
Mama Mghwira

Nadhani tungeanza kuwa kujiuliza kwanza, ni kwa nini hii serikali imeshindwa kusomesha vijana wa taifa ili.

Inawezekana vipi pesa za kusomesha vijana zikakosekana lakini:

1. Pesa za Bombadier zikasepo
2. Pesa za kulipia Boeing zikawepo
3. Pesa za kujengea Chato Airport zikawepo
4. Pesa za kuamishia serikili Dodoma zikawepo
5. etc

Naamini kabisa hii serikali inayo pesa za kutosha za kulipia vijana wenye vigezo, ila tatizo ni kwamba, kipaumbele cha serikali sio kuwa na wasomi wengi wa Higher Education. Kipaumbele ni kuwa na vijana wengi walioishia darasa la 7 au Form 4, ndio maana huku ndiko serikali imeweka nguvu zake na msisitizo
We have problem with priorities !
 
Serikali ya sasa haina nia kabisa ya kumsaidia mtoto wa kimaskini na kila siku serikali inazidi kujenga chuki na wanaichi wake, mfano mdogo tu hayo makato ya asilimia 15% kama mrejesho ya mkopo wa elimu ya juu kwa mnufaika ambaye kajiliwa ilikuwa kama utani ila tayali wamelitimiza mwezi huu sasa unajiuliza hivi kweli hii serikali ina huruma na watu wake

Yani Kijana alipewa mkopo kwa kigezo cha kuwa hajiwezi kiuchumi, sasa leo kapata ajira kaanza kurejesha asilimia 8 na mshahara wake bado serikali haikulizika ikamua ongeza asilimia saba nyingine na kufikia asilimia 15% kweli si uonevu huu uyu unayemfanyia hivi ni mtoto wa kimaskini ambaye ulipatia mkopo

Mfano mtumishi wa umma ambaye salary yake ni 716,000 kama basic salary ukikata makato yote bima ya afya, kodi nk alafu uyu mtumishi awe anamkopo katika tasisi za kibenki kabaki na salary ya moja ya tatu tu, basi kwa ongozeko la makato ya bodi ya mkopo kutoka asilimia 8 mpaka asili 15 % uyu mtumishi mshahara wake haufiki laki mbili

Sasa kwa mtindo huu kweli Kuna uzalendo hapo
 
NI WAZO NZURI MAMA. MIKAKATI IANZE KWANI WAADHIRIKA NI WENGI NA NI WATOTO WA MASIKINI.
KWANZA FANYA PRESS CONFERENCE NA WAANDISHI WA HABARI, THEN IFUATE FUNDRISING.
ATAKAYEFIKIRI HILI NI SUALA LA KISIASA MUNGU AMSHUSHE CHINI.
Waooooh, hili wazo bonge la wazo

Maombi tuuu kisiruhusiwe chama chochote na kwa namna yoyote kulitumia hili wazo kama mtaji,

Na asitokee mtu yeyote atakayeruhusu kutumia kwa namna yeyote hili wazo kwa ubaguzi wowote
 
Tunaomba CAG akague kwanza pesa za tetemeko ili tupate nguvu ya kuichangia tena pesa zetu hii serikali tajiri
 
Tatizo Swahili land mama. Watajichanga wenye machungu lakini kufikiwa bado ni kitendawili.

Na hivi hali ya mitaani ilivyo...

Naunga mkono hoja, kama siasa na maslahi binafsi hazitojumuishwa.
 
ni initiative nzuri sana mama. Mtanzania yeyote mwenye nia njema hana budi kuunga mkono.

nijiongeze hata hivyo kwa kusema kuwa wakati tukiendelea kujipanga kwa mkakati aliouanzisha Mama Mgwhwira, sambamba na hilo kuna umuhimu wa pia ku-address kiini (root cause) cha tatizo. why watoto wetu hawa hawajapata mikopo in the first place?

miaka ya huko nyuma tuliona mikopo ilikuwa inatosha vizuri tu - imagine hadi wanafunzi hewa walikuwa wanapata! sasa hivi tunaamini suala la wanafunzi hewa ni historia, so idadi ya wahitaji (logically) inatakiwa ipungue proportionally.

kwa hiyo katika kutatua kiini cha tatizo tuanze na swali....iliwezekana vipi just a year or so ago lakini the same cannot be done today? tuanzie hapa. let's go to the bottom of it but without interfering with this good initiative from Mama Mghwira.
 
Kwanini umeomba radhi kwa kuandika mtandaoni ?

Kingine , Nakuhakikishia mpango wowote wa kuleta neema kwa wanafunzi nje ya mipango ya serikali hii hautakubaliwa na mamlaka kwa sababu ya uoga , lengo kuu la ccm ni kuhakikisha wanafunzi wanakosa mikopo ili waendelee kuwa mbumbumbu , wasije wakapata akili wakaanza kuongoza mapambano ya ukombozi wa nchi yao .
 
Nimesoma kwa Umakini mkubwa thread yako kuhusu mikopo ya Elimu ya juu. Sijafurahishwa na motive yako! Utanisamehe! Mwalimu Nyerere,Baba wa Taifa,alikusomesha kipindi pato la Taifa likitegemea Mkonge,Kahawa,Pamba,Paretonk. Kwa uwiano wa pato la Taifa na mahitaji,fedha ilitosheleza usomeshwe bure bila harambee za mama au bibi zetu!
Leo,mapato ya nchi hayategemei sana mazao hayo,bali tuna migodi ya madini,makampuni ya mawasiliano,mikopo,grants,wasomi,uvuvi na mengineyo chungu tele!
Kama mwanasiasa mahiri,na mama,dada yetu,ungeanzia hapo kuhoji kulikoni tumekwamia wapi? Ninaamini una nia njema,ila kabla wake zetu,shangazi zetu hawajaanza kuchangia wazo lako,tueleze au tuelimishe tumekwamia wapi? Ukiwa kama kipepeo kuchagua uwa la kuanzia kurukia kwa sababu tu ya rangi au upepo umekusukumia hapo,jamii haitakuelewa vizuri.
 
Back
Top Bottom