Nimesoma kwa Umakini mkubwa thread yako kuhusu mikopo ya Elimu ya juu. Sijafurahishwa na motive yako! Utanisamehe! Mwalimu Nyerere,Baba wa Taifa,alikusomesha kipindi pato la Taifa likitegemea Mkonge,Kahawa,Pamba,Paretonk. Kwa uwiano wa pato la Taifa na mahitaji,fedha ilitosheleza usomeshwe bure bila harambee za mama au bibi zetu!
Leo,mapato ya nchi hayategemei sana mazao hayo,bali tuna migodi ya madini,makampuni ya mawasiliano,mikopo,grants,wasomi,uvuvi na mengineyo chungu tele!
Kama mwanasiasa mahiri,na mama,dada yetu,ungeanzia hapo kuhoji kulikoni tumekwamia wapi? Ninaamini una nia njema,ila kabla wake zetu,shangazi zetu hawajaanza kuchangia wazo lako,tueleze au tuelimishe tumekwamia wapi? Ukiwa kama kipepeo kuchagua uwa la kuanzia kurukia kwa sababu tu ya rangi au upepo umekusukumia hapo,jamii haitakuelewa vizuri.