Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Mikopo inatolewa kwa watoto waliosoma shule za Kata tu, huo ndiyo msimamo wa Serikali hii na ndiyo kigezo kikuu
na hao waliosoma kata na wenyewe hawapewi mpaka wawe hawana wazazi au walemavu.
elimu imekuwa biashara watoto wamaskini kupata elimu ni shida
 
Mungu akutangulie na ufanikiwe kwenye wazo lako.
Maana elimu ni msingi wa ukuaji wataifa,
binafsi Mimi ni muathirika kwa watu waliokosa mkopo mwaka jana.
maisha ni magumu mpaka unatamani kuahirisha mwaka
 
Natafuta, hii tunachangishana sisi raia na tunaikopeshea watoto wetu kwa riba ndogo ya mabadiliko ya fedha (devaluation of the Tshs)
Sasa kwa wazo hili, mwaka huu nitajiandikisha tena chuo kikuu. Nitakutembelea.
 
NI WAZO JENGEFU MAMA. KUNA WANAFUNZI WENGI WAMERUDI NYUMBANI WAMESHINDWA KULIPA ADA KWA KUKOSA MKOPO BODI YA MIKOPO.
SIFAHAM NCHI INAANDAA NINI? HATA HIVYO VIWANDA AU NDEGE ZITAENDESHWA NA NANI KAMA WASOMI WANASHINDWA KUSOMA!
ITISHA KUNGAMANO ILI TUANZIE HAPO.
 
Wazo zuri saana.
Jamani hili jambo lazima liangaliwe kwa jicho la pekee kwa maana wototo machuoni wanahali mbaya sn
Tunataka kutengeneza wataalam wa aina gani
Watoto machuoni wana hali ngumu, wazazi nyumbani ambao ni wakulima hali sio nzuri kuwahudumia watoto wachuo..ali haki ya nyumban pesa mtaani hakuna
Watoto wakike mpaka inafikia kurubunika kiurahisi
 
Kimsingi siamini kama viongozi wanania njema kuhusu elimu na sioni tatizo liko wapi? mfano NSSF, LAPF, PSPF, PPF, GEPF n.k hawa badala ya kujenga majengo ambayo hayana wapangaji, kila mfuko ukatoa billions 50 zikapatikana billions 250 na kila mmoja akapata million 6 jumla ya wanafunzi 41,667 hawa wote waliyokosa wangepata na tatizo likapungua hata kama siyo kuisha kabisa.

Ni kweli tunaweza kabisa kulimaliza tatizo hili...Tuweke mikakati mizuri, tutafika na Mungu atutangulie. Atusaidie kuona uhitaji huu tu.
 
Kipindi cha nyuma kadri tunavosikia stori kulikuwa na tatizo mtoto anafaulu kwenda sekondari lakini alikosa nafasi kwa upungudu wa shule husika!!!

Sekta binafsi ilipoliingilia kati , imefikia hatua kila mtoto anayehitaji sasa kwenda shule sekondari anaenda tena bila shida.


Sasa kwa wazo kama hili hili, mama ameliona akawaazaaa akatoka na jibu hili,
Ameamua kuanzisha chombo cha binafsi cha kutoa mikopo kwa vijana watakao kuwa na sifa za kupata mikopo hiyo,
Uwekezaji katika eneo hili mama kaiona kama fursa na itafika hatua kutokee bodi za mikopo binafsi, kuwe na uchaguzi mtu kuamua kwenda kuchukua mkopo atakapo basi.


Hili ni bonge la wazo jamani mama Anna tumekuelewa.
Asante, tunalifanyia kazi tulete utaratibu. Asante.
 
Wazo zuri lakini litazuiwa ili uwekwe utaratibu mzuri wa kuchangia na CCM ndio watakuwa wasimamizi wa ugawaji wa hizo fedha .
Hii si ya chama chochote. Tufike mahali tuangalie uhalisia wa kila jambo. elimu ni suala nyeti, tukicheza nalo tunapoteza kizazi. Tutadaiwa sana.
 
Maisha ni magumu, kodi tunalipa lakini viongozi hawana priorities. Unanunuaje ndege huna dawa. Unajengaje airport chato huna hela za mikopo ya elimu ya juu. Ishu kubwa ni prioritie na wananchi tukiona serikali iko kinyume na sisi nani atasaidia? Nchi jirani wanapambana na baa la njaa sisi bei hazishikiki na haturuhusiwi kusema kitu. Unadhani mtu mwenye machungu moyoni kiasi hicho atachanga?
Tuchange tu, tusaidie watoto wetu.
 
UHuru wa mawazo na maoni. Mwihso wa siku tjitahidi kumpa kila mtu hifadhi yake kijamii na kielimu. Ndilo lengo la jambo hili. Asante
 
Ndio chombo kinaundwa na kina mama kwa ajili ya watoto wao wote. Tumbo jalala, huokota vyote. Kuwa mama ni kubeba yote ya kwako na ya wenzako. tukisimama vizuri tutawasaidia sana vijana wetu.
 
Tu
Mama Mghwira

Nadhani tungeanza kuwa kujiuliza kwanza, ni kwa nini hii serikali imeshindwa kusomesha vijana wa taifa ili.

Inawezekana vipi pesa za kusomesha vijana zikakosekana lakini:

1. Pesa za Bombadier zikasepo
2. Pesa za kulipia Boeing zikawepo
3. Pesa za kujengea Chato Airport zikawepo
4. Pesa za kuamishia serikili Dodoma zikawepo
5. etc

Naamini kabisa hii serikali inayo pesa za kutosha za kulipia vijana wenye vigezo, ila tatizo ni kwamba, kipaumbele cha serikali sio kuwa na wasomi wengi wa Higher Education. Kipaumbele ni kuwa na vijana wengi walioishia darasa la 7 au Form 4, ndio maana huku ndiko serikali imeweka nguvu zake na msisitizo
lichukulie kama suala la kijamii, tuchange kuwachangia waliokosa mikopo. Tutimize wajibu wetu kama raia.
 
Alright! This sounds positive!

Then, naamini tayari una watu ambao wanafanya analysis na kuweka mipango ya mawazo ambayo unayapata hapa...

Weka mpango kazi mezani ili ukishaanza utekelezaji inakuwa ni rahisi kuwaeleza watu ambao humu hawapo lakini tunaamini watakuwa na moyo wa kuinua Elima kama wewe.

Uwe na safari njema.

You have our support...!
Amen!
 
Mikopo inatolewa kwa watoto waliosoma shule za Kata tu, huo ndiyo msimamo wa Serikali hii na ndiyo kigezo kikuu
wewe hivi unadhani waliokosa mkopo wote wamesoma private schools?.hebu kabla hujaropoka jaribu kufanya uchunguzi hata upate data za juu juu tuu#mimi ni mmoja wa wahanga takriban 30k
 
Mawazo mazuri mama..ubarikiwe sana kutukumbuka wanao tulioko vyuoni natumetoka katika familia za wasakatonge tukitegemea baraka za heslb.Hope they'll be a positive result that will be able to cover even the small number of students who are victim.[HASHTAG]#formeamonmywayhome[/HASHTAG] UE next week 1.8mil where will my streetfish vendor mother will get??
 
Tuchange tu, tusaidie watoto wetu.
Utachanga vipi hali unalipa kodi kubwa, maisha magumu unadhani serikali ingeweka maisha bora kwa wananchi wake kungekuwa na ulazima wa wanafunzi kupewa mikopo? Jibu ni hapana maana wazazi wengi wangemudu kulipia watoto wao ada. Unaingia gharama za kuwapeleka kidato cha sita jeshi kuwalisha na kuwavika halafu huna hela za kuwapa mkopo.Atleast wangekuwa basi wanaenda kulima ili chakula kipatikane hivi mchakamchaka wa miezi sita ndo unamfanya mtu kuwa mzalendo.
Nyie mlio katika nafasi za juu tusaidie kuondoa huu mzigo kwa wananchi, serikali iwajibike wananchi watawajibika bila hata kuweka hamasa. Mimi naona leo airport inajengwa chato, watu wameiba mali za umma na tunaambiwa makaburi hayafukuliwi hivi kweli nitakuwa na moyo wa uzalendo hata kama nimegharamikiwa kwenda jeshi kwa mujibu wa sheria?
Je ni mafisadi wangapi tunao walipitia jeshi?
Pili, serikali inaona haraka gani kuhamia dodoma na sio kusomesha wanafunzi wa elimu ya juu. katika kizazi hichi cha teknolojia watu sio lazima wafike ofisini physically kupata huduma, mambo yote ni kwenye mitandao je kipi kilikuwa muhimu Elimu kwa watoto au kuhamia Dodoma.
Naomba tena nyie weny nafasi ya kuishauri serikali wakumbusheni vipaumbele vyetu. Wananchi tunaumia hela zinavyotumika visivyo
 
Back
Top Bottom