Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Bado waliokosa mikopo wanahitaji elimu, wanahitaji kusoma ili wafanikishe mipango ya maisha yao. Kwahiyo tunapotoa madai yetu mengine tusisahau na hili. Asante
 
w
We want her and many more mothers like her to contribute only 1000. If a million of us contributes just one thousand shillings, that is one billion! How much can we take to schools with that amount? A lot isnt it?
 
Mama wazo lako zuri,tunashukuru maana sie wengine tunaosomesha hadi wadogo zetu kwa kweli awamu hii imekuwa mzigo mzito.
Mtu una vijana wawili wote wako chuo,no mkopo,yaani hadi kichwa kinauma.
Kuna jambo moja nimekutana nalo wakati nahangaika na mdogo wangu mmoja,hebu tusaidie kulifikisha huko ngazi za juu walifikirie upya.
Nakumbuka wakati akiweka jiwe la msingi la hosteli mpya UDSM,mh,Rais Magufuli alisema ni wakati wa vyuo vya serikali kuchukua idadi ya wanafunzi sawa na capacity yake,kwa kuwa vimekuwa vinachukua wanafunzi wachache tofauti na uwezo wake,matokeo yake wanafunzi wengi huenda vyuo binafsi ambavyo vimekuwa vingi bila sababu za msingi.
Katika masuala aliyowahi kuyasema Magufuli,hili lilinigusa sana.
Naomba ukipata nafasi uende kwa Rais ukamkumbushe kuhusu hilo,vyuo vya serikali viongeze udahili wa wanafunzi,ili watoto wengi wasome huko hata kama ni kwa kujilipia,walau ada za vyuo vya serikali ni nafuu.
Hili litazamwe hasa kwenye zile kozi vipaumbele vya taifa,vyuo vya govt vichukue watu wengi.Kozi kama za tiba,it's better wengi wakasoma huko maana ni expensive sana,ni nyeti sana,na wanahitajika sana wataalamu hao.
Mama unahamasisha vijana wa mitaani wajiendeleze vyuoni,uko sahihi,ila katika kuwapa moyo,tungepunguza masharti magumu kwao.Na wao wapewe mikopo,na wadahiliwe na vyuo vya serikali,maana sasa hivi vyuo hivyo havichukui vijana wanaojiendeleza ambao walimaliza zamani.Vinachukua from 2015 kuja mbele nadhani.Sasa mtu anajisomesha mwenyewe,hapewi mkopo,halafu analazimishwa akasome vyuo binafsi vyenye ada kubwa ilhali vyuo vya govt bado vina nafasi?ni bora angeruhusiwa kusoma govt institutions lakini kwa kujilipia,au hata na kozi fulani nyeti iwe hivyo ili kuwahamasisha vijana kusoma huko.
 
Yaani nipo ila sichangii mijadala mingi ndio maana sifahamiki kama nipo...
Piga kazi mother, hii issue ya wanafunzi kuhusu mikopo tutengeneze kitu ambacho kitakuwa na msaada kwa vizazi na vizazi kupitia hapa hapa JF, itapendeza kama wewe utatuongoza kwenye harambee ya kuchangia wanafunzi wetu. Mother wewe ni public figure
 
Wana jukwaa,

Kama nilivyoahidi kuanzisha mfuko wa kusaidia wanafunzi wa elimu ya juu kupata mikopo na kuendelea na masomo. Leo nimefanya mahojiano na waandishi kupitia tamko la waandishi (Press), naaambatanisha andiko langu. Kutakuwa na Kamati ndogo ya kuratibu mfuko baada ya taratibu za kisheria kukamilika. Hizi ni pamoja na kupata kibali cha kuchangisha na makubaliano mengine na wizara ya elimu, Bodi ya mikopo na baraza la mitihani.

Niombe maoni zaidi ya wanajukwaa jinsi bora ya kuendesha mfuko huu ili umfikiei kila mwanafunzi na kila raia mwenye nia ya kujiendeleza kielimu.

Hii ni ndoto yangu ya kuwa na Tanzania ya watu walioelimika, wenye upeo wa kielimu, kifikra na kijamii. Tunahitaji elimu sana ili kufikia Tanzania ya viwanda vyenye ushindani kimataifa. Ninaomba sana ushirikiano wenu.

Tamko halisi hili hapa:


Mfuko wa Mama Anna Mghwira wa Kusaidia wanafunzi wa vyuo vya Juu: (HESF) Anna Mghwira Higher Education Support Fund.



Arusha



Machi 6, 2017.



Elimu ni haki ya kila mtu. Ni chombo muhimu cha kuunganisha jamii, kuondoa matabaka na kuimarisha umoja wa jamii. Ni moja ya njia kuu za kuleta maendeleo. Ni kitu ambacho kila mwenye uhai anapaswa kukipata.



Ni kwa sababu hii tunafikiri kila mwanafunzi mwenye sifa ya kupata elimu na mwenye nia anaipata. Mfuko huu umeanzishwa kuziba pengo hili na kutoa njia mbadala ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Tunajua kuwa wanafunzi wapatao laki 5 humaliza elimu ya sekondari kila mwaka na kuhitaji kuingia vyuo vikuu.



Hata hivyo bodi ya mikopo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi wasiozidi laki 120, 000 tu. Wanaobaki ama hushindwa kuingia vyuo vikuu ama huchagua njia tofauti za maisha. Tunapenda na hawa nao waende vyuoni, wapate mikopo na wapate elimu wanayoihitaji na tunayoihitaji kama taifa. Tumeona kuna haja ya kuratibu juhudi hizi kupitia mfuko huu.



Juhudi za mtu mmoja mmoja kusaidia wanafunzi hazijatupatia matokeo chanya na ya wingi. Tumejaribu sisi wenyewe kwa njia mbalimbali na kwa viwango vidogo binafsi na kwa umoja wetu kujaribu kukabiliana na changamoto hii na kujikuta hatufikii malengo.

Lakini tukiungana kuchangia kidogo tunaweza kutoa fursa kwa wanafunzi wengi kupata elimu.



Awali wazo hili liliwekwa Jamii forum yenye wanachama takribani laki 4 (400,000). Hesabu za haraka zilionesha kuwa kama kila mwanachama wa mtandao huo angetoa shs 1,000.00 (elfu moja tu) tungekusanya kiasi cha Tshs milioni mia nne (400,000,000.00). hizi zingeweza kukopesha zaidi ya wanafunzi 150 kwa mwaka. Tutaweka utaratibu wa makundi mengine ya jamii kuongeza nguvu kwa idadi tofauti.



Kwa kuanzia mfuko utaendeshwa chini ya Taasisi ya ESTL ( Empower Society: TransformLives) yenye ofisi zake mjini Singida na jijini Dar Es Salaam. Tutakuwa na ofisi ndogo Arusha pia.



Tunafanya hivi pia kwa kuamini kuwa lengo la kuwa na Tanzania ya viwanda litaweza kufikiwa nchi ikiweza kuzalisha wataalamu wake wenye ujuzi mkubwa na mpana katika maeneo mengi tofauti tofauti.



Tutatangaza tarehe ya uzinduzi wa mfuko huu baadae mwezi huu.





Asanteni kwa kutika wito huu.


Asanteni
 
hao hao watoto unaopigania wapewe mikopo wakija kuanza kazi ya ualimu na kulipwa laki saba thena makato 15% unadhani wataishije na take home ya laki mbili?
 
Waooooh, hili wazo bonge la wazo

Maombi tuuu kisiruhusiwe chama chochote na kwa namna yoyote kulitumia hili wazo kama mtaji,

Na asitokee mtu yeyote atakayeruhusu kutumia kwa namna yeyote hili wazo kwa ubaguzi wowote
Ilankunda, asante. Tulinde sana hili jambo lisiingizwe siasa ya aina yoyote ile sipokuwa elimu ya juu, elimu kwa ujumla na mikopo ya elimu.
 
hao hao watoto unaopigania wapewe mikopo wakija kuanza kazi ya ualimu na kulipwa laki saba thena makato 15% unadhani wataishije na take home ya laki mbili?
Saint, hiyo ni agenda ya pili. Ya sasa wapate mikopo kwanza. wapate elimu, wapate ujuzi. Wakisha kuwa na hizi nyenzo wataweza kujisaidia kwa njia tofauti. Lengo la mfuko ni kutaka wasome kwanza.
 
Asante mama Mghwira
(1) Mfuko shughuli zake ziwe transparent, ielezwe wapi pesa inatoka, na shughuli zote za kutoa hizo pesa ziwe transparent

(2) Mfuko usiwe na upendeleo, vigezo viwekwe na wanaoqualify wapate usaidizi bila ubaguzi

(3) Mfuko ushirikiane na serikali, upatiwe msaada wa kibalozi huko nje ya nchi katika kuwatafuta wasamaria wema kuuchangia

(4)Mfuko uingie mkataba na wanufaika, kuwa hata wao baadae watakuja kusaidia kuutunisha kama wao walivyosaidiwa

(5)Mfuko uongee na viongozi wote wa dini, ziwepo sadaka maalum za waumini kuutunisha mfuko huu wa elimu

(6)Mfuko utatafute USSD code maalum kutoka TCRA ili watu waweze kuuchangia kupitia sms

(7) Mfuko utoe account yake, na uwashawishi watu walipie kwenye account hiyo kwa kukatwa asilimia 0.1 ya mshahara wao juu kwa juu na mabenki mishahara yao inapopitia na kuingizwa kwenye accont hiyo, hii inasaidia mtu asinotice makato hayo, lakini infact anakuwa anachangia!
 
Saint, hiyo ni agenda ya pili. Ya sasa wapate mikopo kwanza. wapate elimu, wapate ujuzi. Wakisha kuwa na hizi nyenzo wataweza kujisaidia kwa njia tofauti. Lengo la mfuko ni kutaka wasome kwanza.
Mama asante sana.

Nimeshakuelewa, nilijua kuwa kati ya lengo mojawapo ni kupigabia makato Makubwa ya bodi ya mikopo.
Ila kama hio sio mission mojawapo nimeelewa.

Tunakupenda.

Msalimie mwanao.
 
Naafiki mfuko uanzishwe. Niliahidi kupendekeza ninaoamini mnalandana kimawazo kuhusu Elimu. Kabla ya kupendekeza muundo,leo nikutajie hadharani angalao wawili tu. 1. Mh. Easter Bulaya. 2. Mzee wetu Reginald Mengi. 3........,4....... Hao wengine nitakupa baadaye.
Mimi ni scientist by profession,na ni Mtafiti. Nina tabia ya kutaka ukweli,na ni result-oriented person. Hutaka kuona utafiti ukianza ili kupata ukweli, utakaoakisi hali ya matokeo tunayotarajia. Ninaomba nipendekeze yafuatayo kwa uchache
1. Jamii ikupongeze kwa Juhudi zako.
2. Pata wanasheria,wasomi na wachumi (mnaoendana) kimtizamo,muchambue wazo hili kiutafiti,ili liweze kumerge na sera ya Taifa ya Elimu.
3. As a fund, iwe revolving kama ulivyosema,na ikibidi,itengenezewe mfumo fulani wa hisa (nina mfano) wa nchi iliyofanikiwa kivile.
Kwa leo niishie hapo Mama yetu. Mungu akutangulie.
 
Na sheria itungwe zisijekuliwa kama za maafa Kagera
 
Natamani elimu iwe ni lazima kuchangia, hatuwezi kuendelea kama tuna taifa la watu wajinga.
 
Nianze kwa ku-declare interest mimi si mwanachama wa aict wanzalendo wala sitegemei kujiunga na GHETTO lenu.Lakini ulifaa kabisa kupewa nafasi ya viti vya kuteuliwa kuliko yule first lady.Unamawazo mapana kwa mstakabali wa nchi hii.Tuliona Mh Mbatia alivyoufumua mustakabali wa Elimu Tanzania wewe ni Mama wa Shoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…