Anna Mghwira: Tuendeleze mjadala wa Mikopo ya Elimu ya Juu na tuchukue hatua

Mama anzisha harambee hapa hapa JF tunatosha kufanikisha hili jambo.
Tuanze tu, maana tayari wanafunzi kadhaa waliotangazwa kurudishwa nyumbani kwa kukosa ada ama sifa walikuwa zaidi ya elfu kumi (10,000) wengi sana hawa kuwapoteza bilaujuzi wala sifa za kitaaluma. Hiki kijiwe cha JF kikianza tunaweza kukusanya zaidi ya m400 kwa mchango wa elfu moja tu. Tuwaombe moderators wa jukwaa watusaidie...tuweke akaunti ya kutuma. Ili ikiwezekana mhula mpya unapoanza tuwe na kitu cha kuwapa walengwa. Itakuwa thawabu kubwa kwa nchi yetu, kumsaidia mtu kujisaidia. Asante sana kwa maoni haya.
 
Kididimo,

Asante kwa maoni yako. Nitajaribu kuwasiliana na hao uliowataja, hata mimininaafiki mapendekezo yako. Kwa kuanzia tuna kamati ndogo Arusha inayoratibu hatua za mwanzo. Tutaendelea nayo. Kuna mapendekezo JF ianze ili hatua za mwanzo za uchangiaji zianze na wanafunzi wenye sifa kupata mkopo waanze mwezi huu mwishoni vyuo vitakapofunguliwa. Hili linatoa nafasi ya kuharakisha hatua hizi. Kamati ikamilishe majukmu yake, ...baada ya michango na kuwapa wahusika wachache , utafiti uanze ili kutoa picha pana ya tatizo. kwa sasa ninafahamu / nimetafiti kidogo na kujua kuwa zaidi ya wanafunzi laki 400 hawana mikopo. Hawa ni wa daraja la 1&2. Wanafunzi takribani wote wa daraja la 3 na 4 wameachwa nje kabisa, hawajulikani walipo na wanachofanya.

Mtaji wetu nama moja wa kufikia nchi yaviwanda niwatumishi wenye ujuzi. Ninaamini lengo la viwanda hivi nipamoja na kutoa ajira nyingi na bora kwa watanzania kwanza. Kwa hiyo tuna kila sababu ya kutaka wawe na ujuzi wa kila aina. Hili pia litaangaliwa na utafiti huu. Tuanzie hapa. Asante
 

Mhe Lowassa katika manifesto yake ya kutaka kuingia Ikulu alikuwa na agenda yake muhimu sana kwa taifa 1. Elimu 2. Elimu 3. Elimu na kuahidi kuwa watoto wa taifa la Tanzania watasoma bure kuanzia chekechea(nursery) mpaka chuo kikuu bure na wale wote waliosomeshwa kwa mikopo watasamehewa, kwani ni kodi iliwasomesha! Watanzania walichagua mwenye faslisafa ya kuwa watoto watasoma bure kutoka nursery mpaka kidato cha nne(form four). Kule kuomba mchango kutoka kwa wahisani na wabunge kuchanga wakati Watanzania walichagua kusoma mpaka kidato cha nne unaudhi na kusumbua raia wema wakati wanafurahi walichochagua. Let them wait mpaka next election 2020 ili tuone Watanzania wanataka nini! Please tumechagua wenyewe na tunafurahia as 2020 siyo mbali.
 
Gamba la Nyoka,

Asante sana kwa maoni yako. Yote yatazingatiwa.

Tutakuwa na bima pia kwa mfuko mzima na kwa mikopo itakayotolewa. Wataalamu wa fedha na bima watausaidia mfuko kujua njia bora za kujiendesha.

Asante sana
 
Hatuwapi tunawakopesha wote wenye sifa, tutafute wanasheria wazuri waandae mkatamba ambao hauna riba, tuanze na hiyo elfu moja kuanzia April mosi. Nb nasikia na wewe ni mwanasheria hivyo tusaidie
 
Asante. Naomba uwaombe Moderators waiweke hii thread kama "Sticky Thread" kwa vile ni endelevu,na tunahitaji kuchangia pia. Pia mimi,niko tayari kuanza uchangiaji,ila tuone njia nzuri ya kutumia ID zetu humu JF! Wengi siyo verified users na huenda hawatahitaji kuwa exposed publicly. Nina nia njema. Ubarikiwe mama yetu.
 
Kuna vitu vingi vya kurekebisha nchi hii ambavyo vinaingiliana. So the best approach ni kuangalia udahili, quality of education, ajira Na source of financing yaani kodi , utendaji kazi ,rushwa etc
 
Hatuwapi tunawakopesha wote wenye sifa, tutafute wanasheria wazuri waandae mkatamba ambao hauna riba, tuanze na hiyo elfu moja kuanzia April mosi. Nb nasikia na wewe ni mwanasheria hivyo tusaidie
Ndio, si kuwapa ni kuwakopesha kwa riba ndogo kwa sababu ya udhaifu wa fedha yetu...Kamati itaamua lakini asiliia 2% inaweza kufidia pengo hili na ili kuufanya uwe endelevu (revolving) kukopesha wengine kwa kipindi chote cha uhai na uhitaji wa huduma hii.
 
Asante nitaongea na uongozi wa JF. Tayari akaunt ipo lakini kuna taratibu chache za kurekebisha, tuanze.
 
Mother inabidi tufanye harambee iongozwe na PM kwa ajili ya mfuko wetu, mapendekezo mkopo wa shule 5% na wa member wa JF ni 8%, anza kuandika katiba
 
Waooooh, hili wazo bonge la wazo

Maombi tuuu kisiruhusiwe chama chochote na kwa namna yoyote kulitumia hili wazo kama mtaji,

Na asitokee mtu yeyote atakayeruhusu kutumia kwa namna yeyote hili wazo kwa ubaguzi wowote
Press tayari, sasa tunapanga uzinduzi rasmi. Tayri wanafunzi waliokosa mikopo wanajitikeza na kueleza keri zao mbalimbali.
 
Tuhakikishe
Tatizo Swahili land mama. Watajichanga wenye machungu lakini kufikiwa bado ni kitendawili.

Na hivi hali ya mitaani ilivyo...

Naunga mkono hoja, kama siasa na maslahi binafsi hazitojumuishwa.

Tuhakikishe hazitaingia
 

Elimu ni ukombozi wa mtu mmoja mmoja na jamii. sidhani na siamini serikali haitaki watu wapate elimu, lakini changamoto za uratibu zinaweza kutoa matokeo hasi. Sisi tutoe mchangowetu.
 
Kididimo, mkwamo wa rasilimali upo ndio maana tunaongea hivi. Kama kujadili kutawapa wanafunzi mikopo kesho kutwa vyuo vikifunguliwa,basi tuanze huomjadala, lakini kama mijadala mingi haijazaa matunda, tuchange wakati tunajadili ili michango ipungue, na kodi ya mali asiliilipie elimu yetu,
 
Vijana wa Lumumba kwenye huu Uzi huwezi kuwaona wanasubiri michango ikishakusanywa utawaona wakipanga utaratibu wa kugawa.majambazi wakubwa CCM
Waterloo,
Tumesema tusiingize siasa, lakini wewe unaingiza siasa kwa mategemeo kuwa wengine hawatafanya hivyo, itawezekana kweli? Kama hatutaki siasa kwenye jambo lolote tusishutumu mtu wala kikundi mbacho hakijaleta siasa. Anayeleta siasa, atajitoa mwenyewe kwenye kundi.
 

Kampeni ni nia mkuu. Lakini unapofika kazini mambo mengi. Tz maskini sana. Na unaposema utoe mkopo huu. Ujue na mwakani lazima utoe. Rais kazi yake ni kuonyesha dhamiri ya kufanya. Sisi ndo tumsaidie. Hawezi toa hela mfukoni. Nchi ina watu 50,mill na ushee. Embu tumia akili ukioanisha na maisha yako. Angalia kabla hujafikia stage fulani lakini ngoma yenyewe inachangamoto. Unawaza ada. Usiku nyumba inaungua. Unawaza nyumba. Mkwe anafariki. Nk. Nk so kabla ya kuandika pumba tufikirie mana sasa hata mbwa atatuzidi kwa vitu na hoja za kichekechea kisa majina ya kificho.
 
Naam, ndio lengo. Tukifanikiwa kuchangisha kwa miaka 5 mfululizo, tunaweza tusichange tena milele, ilimradi mfuko uendeshwe kwa uadilifu.

Piga kazi mother, hii issue ya wanafunzi kuhusu mikopo tutengeneze kitu ambacho kitakuwa na msaada kwa vizazi na vizazi kupitia hapa hapa JF, itapendeza kama wewe utatuongoza kwenye harambee ya kuchangia wanafunzi wetu. Mother wewe ni public figure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…