Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi.

Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor). Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege.

Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi?

Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.

View attachment 3435096
Unapewa mamelekezo ya kijinga na yenye chuki namna hii na wewe unayakubali? Nadhani hapa badala ya kumsafisha Ndugai amezidi kuonyesha kuwa alikuwa hafai hata kidogo.
 
Bunge la letu ni kibogoyo, linaishi kwa maelekezo. Hata pale kisutu yaleyale tu.
Ni kwanini wanakubali kupewa maelekezo? Mtu mpumbavu akikupa maelekezo na wewe ukayakubali basi wewe ndiyo tatizo kuliko hata yule aliyekupa. Yaani upewe maelekezo kabisa mweke fulani ndani umsingizie kesi ya uongo na wewe unakubali? Mbona kazi za kufanya ziko nyingi sana? Kwani ni lazima uwe mbunge au kiongozi?
 
Ni kwanini wanakubali kupewa maelekezo? Mtu mpumbavu akikupa maelekezo na wewe ukayakubali basi wewe ndiyo tatizo kuliko hata yule aliyekupa. Yaani upewe maelekezo kabisa mweke fulani ndani umsingizie kesi ya uongo na wewe unakubali? Mbona kazi za kufanya ziko nyingi sana? Kwani ni lazima uwe mbunge au kiongozi?
🤣🤣🤣 Mfumo ni mkubwa kuliko mtu yeyote.
 
Visa vya wakubwa ni vingi sana. Ndiyo maana tupaswa kuwaheshimu sana
 
Process za kulikopesha bunge zikoje.

Kwa maneno tuu,
 
Back
Top Bottom