macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 29,500
- 61,451
Unapewa mamelekezo ya kijinga na yenye chuki namna hii na wewe unayakubali? Nadhani hapa badala ya kumsafisha Ndugai amezidi kuonyesha kuwa alikuwa hafai hata kidogo.Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi.
Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor). Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege.
Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .
Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi?
Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.
View attachment 3435096
Mrithi wake ana roho nzuri?magu alikuwa anaendesha nch km familia yake.yule dingi alikuwa na roho mbaya arifu
Absolutely 💯Unapewa mamelekezo ya kijinga na yenye chuki namna hii na wewe unayakubali? Nadhani hapa badala ya kumsafisha Ndugai amezidi kuonyesha kuwa alikuwa hafai hata kidogo.
Kabisa alikubali kumtumikia kafiri alipwe ujiraUnapewa mamelekezo ya kijinga na yenye chuki namna hii na wewe unayakubali? Nadhani hapa badala ya kumsafisha Ndugai amezidi kuonyesha kuwa alikuwa hafai hata kidogo.
Ni kwanini wanakubali kupewa maelekezo? Mtu mpumbavu akikupa maelekezo na wewe ukayakubali basi wewe ndiyo tatizo kuliko hata yule aliyekupa. Yaani upewe maelekezo kabisa mweke fulani ndani umsingizie kesi ya uongo na wewe unakubali? Mbona kazi za kufanya ziko nyingi sana? Kwani ni lazima uwe mbunge au kiongozi?Bunge la letu ni kibogoyo, linaishi kwa maelekezo. Hata pale kisutu yaleyale tu.
🤣🤣🤣 Mfumo ni mkubwa kuliko mtu yeyote.Ni kwanini wanakubali kupewa maelekezo? Mtu mpumbavu akikupa maelekezo na wewe ukayakubali basi wewe ndiyo tatizo kuliko hata yule aliyekupa. Yaani upewe maelekezo kabisa mweke fulani ndani umsingizie kesi ya uongo na wewe unakubali? Mbona kazi za kufanya ziko nyingi sana? Kwani ni lazima uwe mbunge au kiongozi?