Anne Kansiime anavyotengeneza pesa

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Kansiime Anne ni mchekeshaji kutoka Uganda ambae amesomea Sayansi ya saikolojia kwenye chuo kikuu cha Makerere Kampala Uganda ambako alianzia kuchekesha kama utani kusambaza video zake mitandaoni lakini kwa sasa anaingiza mamilioni baada ya kukubalika kwenye nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya.

Kupenyeza kwake kwenye soko la uchekeshaji nchini Kenya ni jambo ambalo hata yeye anasema hakulitegemea kwa kiasi hicho lakini sasa amezidi kuwa maarufu kutokana na show yake ya TV iitwayo 'Don't mess with Kansiime' inayoonekana CitizenTV Kenya ambapo amezidi kupokelewa na Wakenya wengi wakiwemo ambao hubaki kwenye maeneo ya starehe mjini kumtazama kila Jumatano huku wakisubiria foleni ya magari ipungue ndio warudi nyumbani.

Anne anasema baada ya mda mrefu wa kukubalika na watazamaji wake Youtube, kulimfanya siku moja apokee simu kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa CitizenTV Washira Waruru aliempa dili la kuanza kuonyesha show zake kwenye station hii.

Mbali na CitizenTV Kenya, kansiime pia ameangukia dili ya mamilioni ya hela kama balozi wa bidhaa za kampuni ya bima na pia ameonekana kwenye tangazo la kibishara la Old mutual kuhusu kuwekeza akiba kwa ajili ya siku za usoni hasa bima ya watoto kwa ajili ya masomo ya shule ya upili, madili yote hayo yakiwa ya Kenya.

Chanzo: MillardAyo
 
Mimi huwa ananikosha sana huyu dada
 
Naona binamu unawasaidia jf kumpa promo bibie,wametutenga sisi majobless kwa kiingilio kile walichoweka.
 
Kansiime namkubali!" .......... Anajua saaana. big up!

Grand PA
 
Anna ni mkorofi kiama, yani akiwa anaigiza anakuwa serious huyo, me nacheka sana.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…