Anne Kansiime anavyotengeneza pesa

Anne Kansiime anavyotengeneza pesa

Kwikwikwi anavyomtishia sasa kama anampiga na style zake sijui ndo kung fu mwenyew, kavaa na gloves kabisa hahaha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

I have been heard rumors that you are involving your feeling with someone going by the name nani sijui, ahhha demu akaogopa et akasema ana delete namba yake sasa sijui aki delet ndo kamuacha au vp dar hatar sana
 
Kansiime Anne ni mchekeshaji kutoka Uganda ambae amesomea Sayansi ya saikolojia kwenye chuo kikuu cha Makerere Kampala Uganda ambako alianzia kuchekesha kama utani kusambaza video zake mitandaoni lakini kwa sasa anaingiza mamilioni baada ya kukubalika kwenye nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya.

Kupenyeza kwake kwenye soko la uchekeshaji nchini Kenya ni jambo ambalo hata yeye anasema hakulitegemea kwa kiasi hicho lakini sasa amezidi kuwa maarufu kutokana na show yake ya TV iitwayo 'Don’t mess with Kansiime' inayoonekana CitizenTV Kenya ambapo amezidi kupokelewa na Wakenya wengi wakiwemo ambao hubaki kwenye maeneo ya starehe mjini kumtazama kila Jumatano huku wakisubiria foleni ya magari ipungue ndio warudi nyumbani.

Anne anasema baada ya mda mrefu wa kukubalika na watazamaji wake Youtube, kulimfanya siku moja apokee simu kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa CitizenTV Washira Waruru aliempa dili la kuanza kuonyesha show zake kwenye station hii.

Mbali na CitizenTV Kenya, kansiime pia ameangukia dili ya mamilioni ya hela kama balozi wa bidhaa za kampuni ya bima na pia ameonekana kwenye tangazo la kibishara la Old mutual kuhusu kuwekeza akiba kwa ajili ya siku za usoni hasa bima ya watoto kwa ajili ya masomo ya shule ya upili, madili yote hayo yakiwa ya Kenya.

Chanzo: MillardAyo
mkuu kwa kula ban duu ....Una beef na mods nin?
 
Back
Top Bottom