Annunaki created Man: Binadamu tunaoishi sasa tulitengenezwa (tuliumbwa) na Annunaki

Ni kweli kabisa.
 
Nimesoma hadi nikaogopa mpaka nikawaza haya mambo yalitokeaje? Inaonekana hao viumbe walokuwa against Mungu nao walikuwa na nguvu maana nao waliweza kujaribu kufanya alichofanya MUngu dah.
 
Hongera sana ndugu, haya majibu yameshiba na yanajitosheleza.
 
Wametanguliza hisia na Imani zao mbele na sio facts, Kuna maswali wanauliza alafu wao wanajazana upepo eti hili swali gumu sana kwao hawawezi kukujibu

ila kiuhalisia me sijaona swali gumu kutoka kwao ata Moja, ispokuwa ugumu wa swali unakuja kwenye mindset zao na Kwakuwa wao hawawezi kujibu wanahisi wote hawawezi

Swali la kijinga kabisa ambalo wao wanaona ni gumu na limejirudia mara nyingi humu kuliko swali lingine lolote ni nani kawaumba hao Annunaki?

ili ujue ugumu upo kwenye mindset zao, mtu anaeuliza Annunaki wameumbwa na nani, hajawahi kuuliza Wala kujiuliza Mungu anaemuabudu yeye kaumbwa na nani?

Ana hofu nikiuliza au kujiuliza natenda dhambi/nakufuru. ila ndo unakuta wanapongezana wenyewe eti ni swali gumu, kwahiyo ni vizuri tu kujua kwenye mada kama hizi utadeal na watu wa aina nyingi sana
 
Nimesoma hadi nikaogopa mpaka nikawaza haya mambo yalitokeaje? Inaonekana hao viumbe walokuwa against Mungu nao walikuwa na nguvu maana nao waliweza kujaribu kufanya alichofanya MUngu dah.
Usiogope endelea kumtolea Mungu sadaka, Yaani uwe unatoa hata laki kila sadaka, ni ya Mungu hiyo anaipokea, yaani inapaa hadi inamfuata huko alipo😃
 
Aisee Mkuu unajua sometimes napitia comments zao nabaki kucheka tu,hua najaribu kuimagine mpaka Leo ningekua kwenye kundi lao sijui ningekua na akili Gani Yaani😁
Sometimes japo hua Siamini Katika nadharia Zao za miujiza ila mpaka nikatoka kua brain washed hua Nakubali ya kwamba miujiza ipo maana Toka nitoke Huko najiona ni mbarikiwa sana na amani moyoni kiasi kwamba wanavyonishangaa humu imekuaje nakua hivi na kuona kama Nina pepo au wakala wa shetani
( according to Mathanzua)hata Mimi nawaona wanachelewa sana kuiona Nuru na kutoka walipo na kua free!
 
Hongera sana ndugu, haya majibu yameshiba na yanajitosheleza.
Shukrani sana mkuu, ila haya majibu yanaweza Kuwa yameshiba na kujitosheleza kwako tu ila sio kwao waliouliza maana wanauliza wakiwa na majibu yao teyari na ubaya zaidi ni majibu fake

kwahiyo tunaandika tu kwa sababu ya wale walio teyari kujifunza ili wanufaike ila sio hao ndugu zetu, hao kwenda nao toe to toe ni kama kumpigia mbuzi gitaa. All in all shukrani Kwa mada nzuri na fikirishi Mkuu
 
Sawa, umesema tunakuona wewe ni wakala wa Shetani,ambaye is associated with all evil,na kwa kuwa wewe ni mtoto wa Shetani, you must also be evil.Sisi unatuona ni wakala wa nani na tuko associated na uovu gani?
 
Usiogope endelea kumtolea Mungu sadaka, Yaani uwe unatoa hata laki kila sadaka, ni ya Mungu hiyo anaipokea, yaani inapaa hadi inamfuata huko alipo😃
hii Dunia Ina wajinga sana hahahahha
Nilikua nacheki series ya Vikings Kuna character anaitwa flok jamaa walitoka kwao Huko Scandinavian kwenda kuvamia great Britain wakafika Huko kituo Cha kwanza church mwenye cathedral Moja hivi Sasa wale vikings ni Pagans na hawajui taratibu za Christian,wakaua na kupora treasures zote za kanisa,mwisho aakamteka father,
Flock akamuuliza father mbona kwenye mahekalu yenu mnajaza vitu vya thamani kama gold,fedha nk Kwa wingi?
Father:Watu wanamtolea Mungu sadaka
Flok:Kwahiyo Mungu wenu anapenda Mali?
Father:Hapana Yaani tunaamini dhahabu na vyote ni Mali yake hivyo tunamrudishia yeye Mungu mtukufu aliyeumba vyote
Flok:😂😂😂😂 nyie wajinga sana Yaani Mungu kawapa halafu nyie mnamrudushia Tena,ina maana hampendi utajiri ama?
Father:😲😲😲😲
Flock:Sisi Vikings tunatafuta Mali Kwa shida nyie mnajaza kwa mahekalu yenu bila matumizi yoyote et mnamtolea Mungu wenu,Sasa tutawaonesha vikings hatupendi ujinga!
Flok: jamaa(anaonesha msalaba Kwa father)
Huyu ndie Mungu wenu?
Father:hapana ni Yesu kristo mwana wa Mungu alikuja duniani kutukomboa dhambi zetu,alikufa msalabani Ili binadamu tupate ukombozi
Flok:😲😲😲
Ina maana Mungu wenu alikufa?
Father:ndio ila alifufuka siku ya tatu na akapaa mbinguni
Flok:😂😂😂😂😂😂

Hapo utajifunza kitu,Kupitia wale Nordic people nilijifunza kitu japo ni movie ila wale vikings walikua na hoja sana na ndio maana utaona wafalme wao walikataa kupokea dini za kigeni,mpaka mmoja wa mfalme wao aliwahi sema
" Ni Bora nife nikiwa mpagani nikachomwe moto kuzimu na Babu zangu,Kuliko Kuliko niwe mkristo niende mbinguni nikakutane na maadui zangu"

Religion is Opium!
 
Mkuu umenipeleka mbali sana kwa sababu swali langu lilikuwa linalenga kwenye hii mijadala yetu humu JF na si kwa mtazamo wa kidunia kama ulivyofanya wewe, hapa Tz dini kubwa ni ukristo na uislamu hivyo ndio zenye waumini wengi. Sasa tunaambiwa kuwa biblia nayo imecopy kwenye maandiko ya zamani sana kabla ya ukristo huko na kwamba qur'an ikaja kucopy kwenye biblia, hivyo nilitegemea kwamba kama vinatumika vifungu vya biblia basi si na vya qur'an navyo vikatumika maana si wote wenye ufahamu na biblia hivyo wale wenye kuamini qur'an nao wakapata mwanga.

Qur'an na Biblia ni vitabu ambavyo vinatajwa sana humu kwa pamoja utasikia hivi mara vile, ila ajabu ni vifungu vya biblia tu ndio utaona vinatajwa tajwa.
 
Mkuu sisi hatujui kiarabu na Kiquraish kama vipi wewe weka reference Yako kutoka Kwa hicho kitabu itapendeza sana!
 
hahahaha naikumbuka vikinq.nimecheka hayo mazungumzo
 
Mkuu sisi hatujui kiarabu na Kiquraish kama vipi wewe weka reference Yako kutoka Kwa hicho kitabu itapendeza sana!
Mbona kama umepanic mkuu? Tunajadiliana tu hapa wala si ugomvi kama nakukwaza tusameheane.

Ila binafsi nadhani ipo sababu ya kuhoji hili kwa sababu ni kitabu ambacho hutajwa humu pamoja na biblia kuwa hivyo vitabu vinajaza uongo ukweli umefichwa na kwamba qur'an ni copy tu ya biblia kwa maana inajulikana kilichomo kwenye qur'an, sasa hayo ya kutokujua lugha ya kiarabu yanatoka wapi tena mkuu?

Ila kama swali langu unaona halina maana ni la ubishi tu basi achana nalo haina haja ya kutoana akili.
 
Nimesoma hadi nikaogopa mpaka nikawaza haya mambo yalitokeaje? Inaonekana hao viumbe walokuwa against Mungu nao walikuwa na nguvu maana nao waliweza kujaribu kufanya alichofanya MUngu dah.
Ila hizi mada zinanifanya nijiulize hivi neno Mungu linakusudia nini au lina maana gani hasa?
 
Usiogope endelea kumtolea Mungu sadaka, Yaani uwe unatoa hata laki kila sadaka, ni ya Mungu hiyo anaipokea, yaani inapaa hadi inamfuata huko alipo😃
Mimi staki kujua Mungu yupo au hayupo, nilichagua kumuamini kuwa yupo, nitakapoenda kwake nikimkuta sawa, nisipomkuta sawa. Sadaka natoa kile nilicho nacho.
 
Kwa sababu zipi mkuu?
Ok.

Kwa nionavyo mimi tukianza na zilipoanzia dini huko ulaya na kwingineko tunaona watu wameyakimbia makanisa ni wazi watu kadhaa (mapadri masista na washirika wengine)waliohudumu huko wanakiri hili. Hata hapa Tz hili limejidhihirisha ni vile wavivu tu. Kwa mahali nilipo takwimu za waumini wa dini flani ni 700+ ila wanaohudhuria hawazidi 150+ kwa j'2 data wanazikusanya kupitia jumuiya n.k.

Ukiangalia na kusikiliza mahubiri ni sadaka na mahudhurio hafifu.
Sababu kuu ni watu kua waamini wa miujiza tu.

Hivi ni vitu vinaniaminisha kusema hivyo.
 
Nina ba mdogo amesoma seminari ndogo na kubwa nearly to be padri safari yake ikakatishwa akafukuzwa (basi tu) aliwahi kusema hakujawahi kua na Adam na Eva.

Mdogo wake yeye pia seminari ndogo mpaka kubwa akabahatika kua padri naye alimjibu bro uliwahi kusema Adam na Eva ni fiction tu nimeamini ni kweli.
 
Dini zilizokuepo huko kale kabla ya ukristo ni zipi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…