Annunaki created Man: Binadamu tunaoishi sasa tulitengenezwa (tuliumbwa) na Annunaki

Watu mnauliza maswali ya kijinga sana
 
Hiii season ina mafundisho Mengi sanaa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Yaani jitu linakurupuka na kuandika tu mawazo yake toka kichwani,Kama mtoa uzi kazungumzia Apes ndio asili ya mwanadamu hiyo page ntakuanimeiluka.
 
Siri Siri Siri!!

Hicho ndio kitu cha msingi kwenye masimulizi ya aina hii yani cha muhimu ni kwamba hizo ni habari za siri na wewe umebahatika kuzijua hivyo wewe zipokee kama zilivyo na kuziamini kwa sababu ni mambo ya siri. Haya masimulizi ukitaka uyaweke kwenye mtiririko mmoja hutoweza maana utakuta yanaji contradict. Chenye kuvutia watu kwenye haya masimulizi ni hilo neno siri!siri!siri ndio huwafanya kujihisi wameweza kujua mambo ya siri ambayo yalikuwa yamefichwa na kizuri zaidi yanapingana na habari za dini hilo pia huwapendeza waumini wa haya masimulizi. Ndio maana utakuta hadi atheist anaamini haya masimulizi ambayo mengine ndani yake yana mambo ya imani za miungu.

Yote hayo yanawezekana kwa sababu point ya msingi kwenye haya masimulizi ni ile hali ya kujiona umegundua siri ambayo imekuwa ikifichwa, muda mwengine utaona huyu kaeleza hivi kaja yule kaeleza vile wote hao wamegundua siri hata kama wanayoyaeleza yanapingana yenyewe kwa yenyewe.

Siri Siri Siri.
 
Embu elezea huenda unawajua kuna kitu nakiona unataka kukisema kuhusu wanao sali msikitini.
Hakuna watu ambao wanaamini kuwa imani/dini yao ndio sahihi kama hao, hata kama hivyo wanavyoamini si kweli ila kuna kitu spesho sana kwenye imani ya hao watu.
 
Najiulizaga kwa nini wasituambie ukweli, kwamba hizi sadaka ni kwa ajili ya kuendesha shughuli za kanisa.
 
hahahah waseme Siri Tena,acha wawavune wajinga!
Ila binadamu aisee, yaani unaambiwa mtolea bwana sadaka ubarikiwe, na sadaka inayothaminika sana ni pesa hayo matoleo mengine hawayatolei macho sana. Mchungaji anasimama anasema mtoleeni Mungu sadaka, wahumini wanatoa kwelikweli.
 
Yaani jitu linakurupuka na kuandika tu mawazo yake toka kichwani,Kama mtoa uzi kazungumzia Apes ndio asili ya mwanadamu hiyo page ntakuanimeiluka.
Mkuu watakuchanganya tu hao, wao chochote tu wanachoamini ni siri wao wanabeba tu we tizama hata huu uzi ulivyojazwa mikorokoro mvurugano ilimradi tu kila chenye kukiamini ni siri basi kinawekwa.
 
Mkuu watakuchanganya tu hao, wao chochote tu wanachoamini ni siri wao wanabeba tu we tizama hata huu uzi ulivyojazwa mikorokoro mvurugano ilimradi tu kila chenye kukiamini ni siri basi kinawekwa.
Sidhani kama kuna atheist humu kazungumzia habari ya uwepo wa Anunaki kama imani..labda uwe umewaelewa vibaya ndugu

Nadhani wapo kiuchambuzi zaidi

Ikiwa sumerian tablets ni za kale kuliko vitabu hivi vya kiimani hasa quran na biblia basi wana kila sababu ya kusikilizwa
 
Mimi nimefuatilia huu uzi na umenivutia sana nimejua vitu vingi sasa nina hoja zangu ningeomba tuzijadili action and reaction are equal but opposite to each other tunaona kwa ushahidi kabisa watu wakiuza soul zao hasa watu maarufu na wanamuziki na wakishauza katika miziki yao lazima waonyeshe evil occult kama sadaka za damu na vitu vingi kama kuhamasisha ushoga ambao sasa hakuna movie nzuri itakayotoka ambayo haitaonyesha mambo ya ushoga yaani wanajitahidi kila kitu ambacho sio sahihi kionekane sahihi kwa vyovyote hizo ni negative power zinazotaka wanadamu tutende maovu sasa lengo la kutaka wanadamu tutende maovu na dhambi nyingi ni kwaajili ya kumkomoa nani au ili nini kitokee baada ya hapo,

Upande wa pili kuna nguvu kupitia vyombo vya dini no matter ukristo na uislam vinavyosisitiza tusitende maovu tupandane tusiwe na tamaa tuheshimiane yaani kwaujumla tusitendeane maovu.

Hapa ndio tunapata lengo la dini duniani tumezungukwa na negative energy nyingi na ndio maana tunafundishwa kuhusu positive energies.

Yesu au Mohammad kama walikuwepo au hawakuwepo ila kupitia wao tunajifunza kuwa na positive energy among each other hata kama hakuna pepo wala jehanamu ila kama uliishi kwa kutenda mema hata ukiondoka nafsi yako huko ilipo itaishi kwa amani tofauti na aliyetenda maovu kama mtu anadhani anaweza kumlawiti au kumnajisi mtoto mdogo na akajua akifa nafsi yake huko ilipo haitapata adhabu kwasbabu hakuna hell then Dunia ingekuwa mahala pasipokalika watu wasingeogopa kutenda maovu dini zilikuja kutuweka sawa no matter the style ila dini zote zinataka tutendeane mambo mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…