Annunaki created Man: Binadamu tunaoishi sasa tulitengenezwa (tuliumbwa) na Annunaki

Sawa. Ila nikuulize tena kama unaamini malaika walihasi kwa Mungu, kwa nini na hilo useme haliwezekani?
 
Kumbe ni issue ya kuamini au kutoamini.
 
Sumerian walitumia neno DIN GIR, likiwa na maana ya Mungu/Allah wao yaani Anu the righteous one of the sky chamber, Anu ni mjumuisho wa Annunaki yaani Miungu/miungu.
"Zecharia Sitchin, muhandishi na mtafiti na mtafsiri maandishi ya kale na msomi kutoka chuo kikuu cha London, anasema hawakuwa Mungu, japo walichukuliwa na kuabudiwa kama Mungu. Baada ya kufanya tafiti nyingi za maandiko ya kale aliitimisha kwa kusema kwamba, hawakuwahi kuwa Mungu, bali viumbe wa ajabu wenye nguvu waliokuja duniani kutoka sayari ya mbali Nibiru"

Nimekunukuu hapo maana ndio kwenye msingi wa swali langu ni sehemu ambayo sijaielewa niweke sawa.
 
Kwamba Mwafrika alilaaniwa baada ya kumchungulia Nuhu alipokuwa amelewa divai baada ya kutoka kwenye safina, akalaaniwa akawa mweusi kama mpingo, na atakuwa chini , na ndugu zake wazungu/waarabu, watamtawala kwa sababu wao wali barikiwa,
Haya mambo aisee hatari, ndiyo maana wao wanakwambia ni mambo ya imani.
 
Inawezekana vitabu vya dini viko sahihi kwa baadhi ya mambo, huku baadhi yakiwa ya uongo, hao waanzilishi wa hizi dini inawezekana kabisa walichomoa baadhi ya mambo nyeti na yenye ukweli na kupachika mengine yenye mlengo wao, ndiyo maana habari kama hizi zinazidi kuibuliwa.
 
jamaa unaakili nyingi sana wewe nipunguzie
 
Kipi ambacho hujaelewa hapo.
 
Mimi katika imani yangu asee naamini Mungu ni mmoja tu hakuna hao majamaa annunaki...Najua Mungu yupo mwenye uwezo wa kupeleka Jua na mwezi kutokea MASHARIKI kuelekea MAGHARIBI....na Kiyama kipo.

Mimi nitaendelea kumuamini Mungu mmoja tu hadi kifo changu...

Na stori iendelee pale ilipoishia......
 
Safi ni jambo jema. Ila niseme kwamba Annunaki ni Miungu iliyoabudiwa kama Mungu wao, kama ilivyokuwa huku Afrika mlivyoabudu Miungu yenu tena kwa majina kama Mungu wenu, kabla ya wamisionari kuwaambia kuna huyo Mungu unayemuamini atakaye leta kihama kwa watu wake.
 
Uzuri ni kwamba wakati waafrika wanaabudu hizo ibada hatukuziona....

Kwahiyo hainichanganyi...

Niseme tu hao majamaa walikuwa wanaabudiwa na hao watu wa kale kabla ya Mitume na Manabii kuletwa...kwahiyo Manabii na Mitume wamekuja kuwaelimisha watu juu ya MUNGU mmoja...

Kuna ambao wameelewa na bado wabishi wa kuelewa juu ya MUNGU mmoja.
 
Hao mitume ni uzao wa Annunaki pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…