Annunaki created Man: Binadamu tunaoishi sasa tulitengenezwa (tuliumbwa) na Annunaki

Annunaki created Man: Binadamu tunaoishi sasa tulitengenezwa (tuliumbwa) na Annunaki

Nakuomba sana Mkuu urelax alafu twende taratibu Mkuu, wala usiwe katika hali ya kujibu huku ukiwa umekasirika. Kuwa kama mimi (Open Minded)

Tuendelee, "Wametoka sayari nyingine, kwahiyo haijulikani ni walijiumba/wamejiumba"

Nukuu ya Quote yako hiyo, unasema haijulikani kama wamejiunda. Huoni kama unajichanganya?

Mwanzo nilikuuliza kuna kiumbe ambae yupo physical in shape ambae anaweza kujiunda? Ukanijibu na tukakubaliana kwamba HAKUNA.

Sasa, Kama kiumbe Annunaki ni kiumbe kama sisi binadamu yupo physical in shape unaweza kumuona na kumshika, ina maana (1) Hawezi kujiunda mwenyewe (2) Ana muundaji.

Nakuuliza,
UNAWEZA KUNITAJIA MUUNDAJI/CHANZO CHA KIUMBE ANNUNAKI?

NB: Naomba sana unijibu swali hilo kama jibu unalo, pia kama haujui pia niambie.

Tatizo lenu hampitii andiko Zima hayo maswali kama Yako yameulizwa post za nyuma na yametolewa ufafanuzi,tatizo hampitii andiko Zima kama kawaida ya wabongo wanaosoma kava nduki kuweka maneno Yao!
 
Nakujibu kwa ufupi sana kwamba muumbaji wa Annunaki hajulikani.
 
Na cha kukuongezea ni kwamba Annunaki ni uzao wa Anu, Anu ni kutoka Sayari ya Nibiru, kwenye reference zangu hakuna mahali panapo onyesha uumbwaji wa Annunaki. Kinachoandikwa ni viumbe kutoka sayari nyingine waliokuja hapa duniani kwa mission maalamu. Mungu wenu mnayemsema ni Yule ambaye mnasema ameumba dunia na vilivyomo kwahiyo hausiki na uwepo wa sayari nyingine kwenye hii solar system. Na kwa nadharia hii inaonyesha kuna Mungu zaidi ya mmoja(Miungu), Miungu inathibitishwa na kuonekana huyo Mungu mmoja mnayemsema hajawahi kuthibitishwa na hakuna namna unaweza kumthibitisha.
 
Mkuu Hiyo I'd ya huyo bwana inajulikana ni mhafidhina wa dini ya jangwani,mwandiko wake haujifichi mara nyingi kwenye mijadala na mada kama hizi ambazo zimemzidi Kwa kimo Cha ufahamu wake hua anakuja na mashairi mareefu ila ni non sense Hana alijualo ana undugu na @Jurjan au I'd yake ni kinyonga ila mwandiko humuumbua!
Hawataki kujifunza nje ya dini yao, ndiyo maana kila sehemu wanalalamika wanaonewa. Akili ya ziada utaitoa wapi kila wakati upo na vitabu vya dini tu.
 
Wao ndio walimuumba binadadamu(kwa mujibu wa mada)

Hivyo hawawezi kuja kumfanyia ubaya kiumbe waliyemuumba wao wenyewe,kiumbe aliyetokana na wao wenyewe.

Kiakili tu haiwezekani wajw dunia i kufanya fujo hata siku moja,pengine na sisi binaadamu tutapata vibarua vya kuchimba dhahabu tukapata viajira na kuendesha maisha yetu.
Kwao haiwezikan ila.kwa Mungu inawezekana kwann?
Dini zimetufunga akili sana
 
Tatizo lenu hampitii andiko Zima hayo maswali kama Yako yameulizwa post za nyuma na yametolewa ufafanuzi,tatizo hampitii andiko Zima kama kawaida ya wabongo wanaosoma kava nduki kuweka maneno Yao!
Mimi mtu akiuliza swali najua kabisa huyu kapitia mada au hajapitia. Ndiyo maana nawaambie rudini mkasome, wanaishia kulalamika sijibu maswali.
 
Ni kweli waafrika waliumbwa na anunnaki? Na vipi kuhusu Sumerians kwamba walikua blacks kuna ukweli wowote hapa? Watafiti wa anunnaki naomba msaada wenu please
Ni kweli hata mtu mweusi ni uzao wa Annunaki, vinasaba vyetu vipofanyiwa utafiti, iligundulika vilifanana kabisa na vile vya mabaki ya mwanamke (goddess ambaye ni Annunaki ) yaliopatikana kusini mwa Afrika. Sina hakika kama blacks wote ni Annunaki, ila kuna baadhi ya makabila ya blacks kama Dogon nchini Mali, wale asili yao ni sumerian. Taarifa zaidi kuhusu mtu mweusi alielezea Ushindi victory kwenye huu uzi.
 
Ndiyo uwepo wao hapa duniani umethibitishwa si kwa maandiko tu bali hata ushahidi wa kuonekana.
Nakuja hapa.

Safi kabisa, hili mbona hujathibitisha ? Tuthibitishie ni kina nani waliwaona Annunaki kwa macho.

Kama umeshindwa kuwataja hata Sumerians kumi tutajie wawili walio waona. Hii ziada hivi ushawahi kujiuliza ni kwanini Injili zile nne zina uongo mwingi ? Jibu sahihi ni kuwa sababu waandishi wa hizo Injili hawakumuona Yesu kwa macho.
 
SEHEMU YA KWANZA.

Ukweli uliofichwa, unaopatikana kwenye vipande vya mawe vyenye jumbe kutoka sumerians, Babylonians, Akkadians.

Ukizungumzia kuhusu watu wa kale, maisha ya kale na viumbe waliofika duniani kutoka sayari nyingine huwezi kuwasahau annunaki. Historia kutoka katika summerian culture inaeleza kwamba, Annunaki waliabudiwa na walihusika katika kuhukumu mema na mabaya, gods and goddesses waliokuja duniani kumtengeneza mtu (modern man) kutoka kwenye ulimwengu mwingine, ambao unasemekana ni sayari ya Nibiru (sumerian God & Goddesses -the Annunaki, 2016).

Annunaki walitawala maisha na mifumo ya imani ya watu wa kale waliojulikana kama Mesopotamia, lakini ambao kwa sasa wanajulikana kama Tigris-Euphrates river system. Je walikuwa Mungu? hili suala ambalo linazua mkanganyiko kwenye hii saga.

Zecharia Sitchin, muhandishi na mtafiti na mtafsiri maandishi ya kale na msomi kutoka chuo kikuu cha London, anasema hawakuwa Mungu, japo walichukuliwa na kuabudiwa kama Mungu. Baada ya kufanya tafiti nyingi za maandiko ya kale aliitimisha kwa kusema kwamba, hawakuwahi kuwa Mungu, bali viumbe wa ajabu wenye nguvu waliokuja duniani kutoka sayari ya mbali Nibiru inayopatikana kwwnye mfumo wa sayari, ambayo uikaribia dunia kila baada ya miaka 3,500 ikiwa kwenye muhimili wake.

Creation of Human Race
Kutokana na ushahidi uliopatikana kutoka kwenye maandiko ya kale, inasemekana zaidi ya mamia ya maelfu ya miaka iliyopita walikuja viumbe waliofanana na Annunaki kwenye sayari ya dunia- Enki na Enlil, ambao walikuwa watoto wa Annunaki, katika kipindi hicho Anu alikuwa bado anaishi hadi millennia karibu na kuzaliwa kwa Jesus Christ.

Viumbe hao walikuwa na ujuzu mkubwa katika genetic manipulation, hivyo kwa kutumia ujuzi huu walifanya majaribio mengi (proto-human) ya kumtengeneza binadamu wa sasa(modern man) kwa kutimia teknolojia ya human cloning. Kivipi?, ntaelezea mbeleni.

Hebu turudi kwanza kwenye biblia na historia ya kuumbwa kwa mwanadamu. Historia ya Biblia ya uumbaji inatueleza kwamba, mwanaume na mwanamke hawakuumbwa kwa wakati mmoja, bali mwanamke alitolewa kwenye ubavu wa mwanaume (Adam), Adam akiwa mtu wa kwanza kuumbwa hapa duniani kutokana na maandiko ya Biblia, Kwahiyo Adam ndiyo mwanadamu wa kwanza kutokana na maandiko matakatifu ya Biblia takatifu. Je mwanamke alitolewaje kwenye ubavu wa mwanaume? (hapa imani ndiyo inatuongoza tuliache kwanza lilivyo).

THE CREATION OF MAN
Ushahidi wa kwanza kabisa, uliotafsiriwa na sumerians unaonyesha ya kwamba mtu (binadamu wa sasa) alitengenezwa/kuumbwa na Nefilim. Ushahidi huu umezua mkanganyiko kuhusu theory of evolution na Judeo-Christian tenets ambayo imeegemea kwenye Biblia, lakini ukweli ni kwamba ujumbe uliopatikana kutoka Sumerian texts, ndiyo unaoweza kudhibitisha hizo nadharia mbili.

Ukisoma kutoka epic of creation ya sumerians, imeelezwa kwamba uwepo wa mtu, ulitokana na uwepo wa Nefilim zama hizo, ambapo matukio mbali mbali yalirekodiwa, ,mfano tukio la Enlil na Ninlil, tukio lililotukia kabla hata ya uumbaji wa mtu, wakati ambao kwenye Nippur waliishi gods tu, vile vile maandishi haya yanaelezea kuumbwa kwa dunia na maendeleo ya mimea na maisha ya wanyama, hii inaweza kudhibitisha theories za mabadiliko (evolution) za sasa.

Sumerians texts zinaeleza kwamba, wakati ambapo Nefilim alikuja duniani kwa mara ya kwanza, sanaa ya kupanda mbegu za mazao, matunda na ufugaji wa wanyama ulikuwa bado haujaanza duniani. Vile vile Biblia inasema hivyo, kuhusu kuumba mtu kwa siku 6. Kitabu cha Genesis kimegusia hatua za kwanza za mabadiliko (earlier evolution stage):

No plant of the cleared field was yet on the earth,

No herb that is planted had yet been grown,

And Man was not yet there to work the soil.

Lakini vile vile Sumerians texts zote zinaeleza kwamba Miungu ilimtengeneza mtu ili afanye kazi yao. Creation of epic imelithibitisha hilo (Nukuu zote nitaziambatanisha zilivyo kwenye vitabu bila kuzitafsiri ili nisipindishe maana kwa msomaji):

I will produce a lowly primitive,

Man shall be his name.

I will create a primitive worker ,

He will be charged with the service of the gods,

that they might have their ease.

Neno mtu(man) limetokana na lugha ya Sumerians na Akkadians, ambalo lilitokana na maneno lulu (primitive ), lulu amelu (primitive worker), an awilum (laborer).

Turudi kwenye biblia, baada ya Mungu kumuumba mwanadamu, akampa bustani ya Eden aitunze na kuitawala dunia na vyote vilivyomo, lakini Adam na Eve wakamkosea Mungu kwa kula tunda la mti wa ufahamu. Mungu akasema tazama, mtu amekuwa mmoja wetu, kufahamu mema na maovu. Je huyo Mungu alikuwa anamwambia nani?, na Mungu anayezungumziwa hapa katika Sumerians ni Elohim (Annunaki).

Agano la kale limeweka wazi ya kwamba mtu hakuwa Mungu wala hakutoka mbinguni. Mtu wa kwanza aliitwa Adam kwa sababu aliumbwa kwa "adama" ambayo ina maana ya udongo wa dunia (mtu akifa tunasema ametoka mavumbini, amerudi mavumbini).

Adam aliumbwa katika picha na ufanano wa Muumba (Mungu), kuumbwa kwa ufanano huo, hakuachi wasiwasi wowote ya kwamba Mtu alifanana na Mungu kimwili, kimuonekano wa nje na ndani. Je mtu angewezaje kufanana na muumba wake? Mtu alitengenezwaje? (Majibu utayapata mbeleni).

Mnamo mwaka 1859 Charles Darwin alichapisha utafiti wake kuhusu evolution "On the Origin of Species by Means of Natural Selection, or the Preservation of Favoured Races in the Struggle for Life". Darwin kutokana na utafiti wake huo, alihitimisha kwa kusema kwamba, viumbe hai wote akiwemo mwanadamu ni matokeo ya mabadiliko(evolution by natural selection). Mwanzoni kanisa lilikuja juu kwa kumpinga lakini badae kadri wanasayansi na watafiti walivyozidi kutoa machapisho yao, kanisa likakubaliana.

Lakini je tumetokana na apes, kama ni hivyo mbona wa sasa hawabadiliki. Evolution kwa ujumla inaweza kuelezea matukio yaliyosababisha mabadiliko ya maisha na aina mbali mbali za maisha zilizokuwepo duniani, kuanzia kwenye kuumbwa kwa mtu, lakini evolution haiwezi kuelezea kuhusu uwepo wa binadamu wa sasa (modern man/Homo sapiens) na haina udhibitisho wowote wa kuonyesha jinsi mabadiliko ya ghafla kutoka Homo erectus kwenda Homo sapiens yalivyotokea.

Hominid ya genus Homo ni matokea ya evolution, lakini Homo sapiens ni matokea ya tukio la mabadiliko na mapinduzi ya haraka sana. Homo sapiens(binadamu wa sasa), ilitokea miaka 300,000 iliyopita, muda ambao ni wa karibu sana.

Watafiti na wanasayansi hawana maelezo ya nini kilitokea, kupelekea mabadiliko ya ghafla hivyo na kutokea kwa binadamu wa sasa, lakini jumbe kutoka sumerians na Babylonian zimeelezea. Agano la kale pia limeelezea.

Homo sapiens-modern man-aliletwa na miungu wa kale (ancient gods).

Aliletwa kivipi? na wapi?. Endelea kufuatilia hapa hapa.

N.B. Andiko hili linaweza lisiishe karibuni kwa sababu nataka niweke kila aina ya ushahidi ili kudhibitisha ukweli huu.

View attachment 2099862
Kwanin picha nyingi zilizokuwa zikionesha mfano wa viumbe waliopatikana kabla wa yule aliyekusudiwa zimekaa katika picha za mapenzi, ukitazama vzr utaona mpka viumbe hao wakibusiana?

Lakin piah hawa viumbe waliokuwa wanakosewa, vip waliuwawa au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo wewe references zako za ukweli, mimi za kwako hazina ukweli na sote tunatumia vitabu kama reference?
Sababu huu ni mjadala huru, ni juu yako kuzipa nguvu "references" zako kuonyesha ni za kweli na mimi nitazipa nguvu za kwangu kuonyesha ukweli wake, ndiyo maana tunahoji na kuulizana.

Naendelea....
 
Alafu mimi situmii kitabu kimoja kama wewe. Mimi nimetumia the 12th planet (ninachokiamini kama wewe na hicho kitabu chako), vitabu vy dini, Annunki Genesisi, The end of days, Stairway to heaven, immortality of the Gods, Epic of Summer&Babylonian etc.
Hicho kitabu ninachokiongelea mimi kimekusanya vyanzo zaidi ya mia, na kila kilichoelezewa kimewekewa marejeo. Hizi ndiyo kazi wanazofanya wanazuoni wetu kutukusanyia habati toka vyanzo tofauti na kuzihakiki. Unaweza ukasoma vitabu mia ila vyote vikawa havina marejeo mama, kwahiyo wingi wa vitabu si hoja, hoja kile kilichoandikwa kina ukweli na je kimehakikiwa ?

Kitabu cha dini gani kimeelezea habari za Annunaki ?
 
Huu ujinga mwingine. Ukisoma katika kitabu kiitwacho "Al-Bidayat wa al-Nihayyah" cha Imam Ibn Kathir utaona asili ya tamko "Ustaarabu(Civilization)" limetoka wapi. Ustaarabu umeletwa na mitume na manabii, sababu walikuwa wanapewa muongozo toka kwa Allah, mathalani ukisoma maana ya Ustaarabu, kwanini umeitwa kwa jina hilo, sababu walikuwa wakiwafanyia wema wanawake, ndiyo maana Waarabu wa kale wakaitwa "Wastaarabu/Mstaarab".

Swali langu la msingi bado liko pale pale huwezi kukuta maandishi kisha ukayafasiri ukahitimisha ya kuwa ni ukweli bila kutafuta asili na kulinganisha na maandiko yasiyo kuwa na shala ndani yake.

Nitakuuliza je hao Sumerians walikuwa walikuwa wanapata habari za mambo yaliyo fichikana kupitia nini ?

Hata Waarabu walikuwa wanatunza maandiko yao kutunza maandiko hakumaanishi ya kuwa maandiko yao ni ya kweli.
kumbe muislam, nyie ndo wale mnaosema peponi mtapewa bikra 72[emoji706][emoji706][emoji706][emoji3]
 
Kwahiyo watu wanaothibitisha uwepo wa hao viumbe, hujawaona kwenye sehemu ya Annunaki, CIA & NASA, mabaki yao na nyayo zao zilizogunduliwa hujaviona. Wewe unaweza kuonyesha uthibitisho gani wa kuonekana kwamba Mungu huyu hapa yupo au alikuwepo duniani.
Maigizo ya CIA na NASA yanajulikana, anzia kwenye tukio la kwenda mwezini na safari za masafa marefu.

NASA si katika marejeo ya kweli zaidi kutaka sifa na mengineyo.

Wewe ukionyeshwa mabaki haya ni ya Annunaki, mathalani unahakiki vipi habari hii ? Je utaridhika tu kisa wamesema CIA au NASA ?

Kuhusu uwepo wa Mola muumba ithibati yake au utambuzi wake unaanzia katika maumbile na hatua zake ni tatu, kisha ufunuo unakuja kithibitisha. Hatua ni hizi zifuatazo :

1. Fitrah (Innate disposition)
2. Maarifa ( Acquaintance)
3. Establishment of the proof, hapa tunakuja kuhitimisha kwa ufunuo toka kwake, baada ya kupitia hizo hatua mbili za mwanzo, kwa ufupi hatua ya kwanza ni kila mwanadamu ameumbwa kwa umbile la kukubali uwepo wwa Mola, ila wazazi wake au walezi wake huja kumbadilisha aidha akawa myahudi au mkristo au mkana Mungu na mfano wake, kwenye kipengele cha pili ule utambuzi baada ya kuona viumbe vya Allah na kuhoji kwa usahihi na kipengele cha tatu ndiyo hicho kinachothibitisha sasa uwepo wake ambacho ufunuo.

Anasema Allah aliye juu :

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Turi : 35)

Hiyo aya inathibitisha juu ya uwepo wa Allah, kwa kuwauliza wale wote wanao kataa juu ya uwepo wake, kwamba je wao wamejiumba au wao wametokana pasi na chochote ? Basi leteni masimulizi kinyume na haya kama nyinyi mnasema ukweli.
 
kumbe muislam, nyie ndo wale mnaosema peponi mtapewa bikra 72[emoji706][emoji706][emoji706][emoji3]
Haswaa ndiyo sisi, na hakuna yeyote anaye weza kupinga haya kwa elimu na hoja zaidi ya dhihaka na mfano wa hayo.

Shukrani.
 
Haswaa ndiyo sisi, na hakuna yeyote anaye weza kupinga haya kwa elimu na hoja zaidi ya dhihaka na mfano wa hayo.

Shukrani.
dhihaka iko wapi hapo so ndo Hadith zenu zinavyosema haya na wanawake watapewa nin peponi
 
Naanzia hapa. Tusiwe tunaongelea mambo juu juu. Tujadili kielimu, mimi ni Muislamu, naomba unionyeshe uongo uliopo kwenye Uislamu na uthibitishe ya kuwa huu nu uongo.
Mabikra utawakuta kweli una uhakika? Unamfahamu Muhammed umewahi kumuona? Huu ndiyo ulaghai wa kwanza.
 
Nakuja hapa.

Safi kabisa, hili mbona hujathibitisha ? Tuthibitishie ni kina nani waliwaona Annunaki kwa macho.

Kama umeshindwa kuwataja hata Sumerians kumi tutajie wawili walio waona. Hii ziada hivi ushawahi kujiuliza ni kwanini Injili zile nne zina uongo mwingi ? Jibu sahihi ni kuwa sababu waandishi wa hizo Injili hawakumuona Yesu kwa macho.
Mbona nshakujibu au hayo majibu huyataki.
 
Hicho kitabu ninachokiongelea mimi kimekusanya vyanzo zaidi ya mia, na kila kilichoelezewa kimewekewa marejeo. Hizi ndiyo kazi wanazofanya wanazuoni wetu kutukusanyia habati toka vyanzo tofauti na kuzihakiki. Unaweza ukasoma vitabu mia ila vyote vikawa havina marejeo mama, kwahiyo wingi wa vitabu si hoja, hoja kile kilichoandikwa kina ukweli na je kimehakikiwa ?

Kitabu cha dini gani kimeelezea habari za Annunaki ?
Na mimi hivyo hivyo tena ni zaidi ya vyanzo mia 50 na marejeo juu. Kwahiyo kama unakiamini hicho na mimi nakiamini cha kwangu, na nazani hapa tumeelewana.
 
Back
Top Bottom