Maigizo ya CIA na NASA yanajulikana, anzia kwenye tukio la kwenda mwezini na safari za masafa marefu.
NASA si katika marejeo ya kweli zaidi kutaka sifa na mengineyo.
Wewe ukionyeshwa mabaki haya ni ya Annunaki, mathalani unahakiki vipi habari hii ? Je utaridhika tu kisa wamesema CIA au NASA ?
Kuhusu uwepo wa Mola muumba ithibati yake au utambuzi wake unaanzia katika maumbile na hatua zake ni tatu, kisha ufunuo unakuja kithibitisha. Hatua ni hizi zifuatazo :
1. Fitrah (Innate disposition)
2. Maarifa ( Acquaintance)
3. Establishment of the proof, hapa tunakuja kuhitimisha kwa ufunuo toka kwake, baada ya kupitia hizo hatua mbili za mwanzo, kwa ufupi hatua ya kwanza ni kila mwanadamu ameumbwa kwa umbile la kukubali uwepo wwa Mola, ila wazazi wake au walezi wake huja kumbadilisha aidha akawa myahudi au mkristo au mkana Mungu na mfano wake, kwenye kipengele cha pili ule utambuzi baada ya kuona viumbe vya Allah na kuhoji kwa usahihi na kipengele cha tatu ndiyo hicho kinachothibitisha sasa uwepo wake ambacho ufunuo.
Anasema Allah aliye juu :
35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Turi : 35)
Hiyo aya inathibitisha juu ya uwepo wa Allah, kwa kuwauliza wale wote wanao kataa juu ya uwepo wake, kwamba je wao wamejiumba au wao wametokana pasi na chochote ? Basi leteni masimulizi kinyume na haya kama nyinyi mnasema ukweli.