Annuur: Serikali imefuta mitihani ya Dini !!!!!!!!!!!

Ndugu zangu; Sifa za habari za uchochezi kwenye chombo chochote cha habari ni kuwa na maneno kama haya "Yasemekana, chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutajwa kimeeleza, msemaji hakutaka kutaja jina, mwandishi amesikia, mpango wa siri kubwa, Hata hivyo haifahamiki, inafikiriwa kwamba, kwa vyovyote vile itakuwa, haikujulikana nani aliesema, hata hivyo habari ambazo hazikuthibitika zinaeleza.., alipotafutwa kuhojiwa hakupatikana, waliokuwepo walisimulia hata hivyo hawakutaka tutajwa, alietupa taarifa anadai kuambiwa ,na kuweka picha na vielelezo na picha visivyohusiana na habari."

Ndugu zangu; kokote mtakapoona maneno haya yametumika, someni habari hiyo kwa macho matatu.
 
Kama serikali haina dini na haitaki iwe chombo cha kusimamia dini za watu,basi mpaka watendaji wake wasiwe na dini ili waweze simamia ipasavyo mambo yake
 

Tanzania yenye vita na mavunjifu ya Amani inakujaaa... ! Kumbe kuandika ukweli ni Upuuzi sikujua kabisaa...
 
Ni jambo jema sana,ngoja wafute,kwanza matokeo ya dini hayakuwa yana hesabika katika kupanga daraja alilipota mwanafunzi,anayetaka somo ilo ajiunge na madrasa au bible school,kwani madrasa au bible school hakuna mitihani kama shida ni kufanya mtihani?
 
Hivi kumbe siku hizi bila somo la dini, huna sifa ya kujiunga chuo?

tragedy of the commons
 
Kwa akili yako unafikiri kuna kitu hicho cha kushirikisha Wakiristo tu? Hebu tuwe ni wapembuzi zaidi ya kulaumu.

Una maana Kawambwa anaitumia Wizara kuendesha Kikiristo? Hamtaamini mpaka lini? Au ukiona Sheikh momoja ameshika nafasi hizo ndo utaona nafuu.

Ila Ukweli hujifitini hata siku moja


 
Hayo ndo matatizo, mbona habari yenyewe haieleweki maana inaonekana kama imeegemea upande mmoja tu. Acheni uchochezi kama kazi hamna si mkae nyumbani kwenu mle ugali na mboga tu, damn it!
 
Wengi hii habari hamjaielewa, sio kwamba masomo na mitihani ya dini haitakuwepo, itaendelea kuwepo daima na milele amina, ila tu serikali haitatahini. Kwa hiyo PHD za theolojia zitaendelea kuwepo, naona huwa zinakukwaza sana mkuu. Hakuna anaeweza kuziondoa.
 
O.K lakini mbona walipoamua kuifuta walijifungia chumbani peke yao na Wakristo? kwa nini Waislamu pia ambao somo lao lilikuwa likitahiniwa hawakushirikishwa?

KWAHIYO WE MTOA MADA UNATAKA KUVUNJA AMANI AU., nshakusoma ndo wale wale. HAYA KACHOME PIA ...... !..
 
Sielewi kajarida kama haka kanawezaje kuendelea kua hewani miaka yote hii? Habari nzima haina hata direct quote kutoka kwa mtu halisi hata mmoja na imejaa cheap shots za uchochezi throughout, na inajikanganya tangia mwanzo! na kuna watu teyari wameshaichukulia taarifa hii kama absolute truth...halafu kesho serikali hiihii dhaifu na ya ajabu itashangaa kwanini extremism inakua kwa kasi Tanzania/
 
Waislam walalamishi jamani, hiyo mitihani yenyewe mlikuwa mnafeli utadhani mnafanya mtihani wa dini ya Galatia.
 

Kamata "LIKE"! kubwa... afu kama ni masomo ya dini yamefutwa mbona mleta mada anaongea as if limefutwa Islamic pekee na Bible knowledge ama divinity yameachwa...., we have discovered the masterminds to whom you owe the tune you are dancing to. pathetic.....!!!
 

Ni sehemu ya mfumo wa serikali yetu DHAIFU,haina nia ya counter check extrimism bali ina take advantage of it.. na kuna watu wanapenda kweli wakilishwa maneno yenye kuonesha wanaonewa, na kwa kuwa wameonesha kuyapenda basi kila siku watalishwa mapya...pathetic
 
kwahiyo unataka kutuambia wahusika wa pande zote walihusishwa kwenye mchakato wa kutotahini hiyo mitihan? hivi nchi hii lini mtakuwa wakweli? lini mtakuwa na akili ya kupima mambo bila kuegemea kamzizi mliojichagulia, ningekuona wa maana ungehoji ukweli wa kuwakutanisha watu wa upande mmoja tu huku wengine wakipewa taarifa tu.
 

Hivi hata Rais Kikwete na Shukuru Kawambwa hawakushirikishwa kweli? Hebu waulizeni bana!!
CC. Songoro & Coy
 
ok sawa lakini hebu niambie ni nani kaiwakilisha panel ya islamic knowledge? bakwata hawakuhusishwa, naomba niambie au labda alihusishwa ponda? SIKU ZOTE NTAPINGANA NA USIRI KTK MAAMUZI YANAYOGUSA JAMII KAMA HILI.
 
O.K lakini mbona walipoamua kuifuta walijifungia chumbani peke yao na Wakristo? kwa nini Waislamu pia ambao somo lao lilikuwa likitahiniwa hawakushirikishwa?
Nina shaka na hii thread kama sio mojawapo ya mikakati ya uchochezi wa kidini. Siamini kama Necta wanaweza kufanya kosa kama hilo.
 
kwahiyo unataka kutuambia wahusika wa pande zote walihusishwa kwenye mchakato wa kutotahini hiyo mitihan?
Wewe unaonaje? Msifikiri wote humu ni vichwa maji kama ninyi, wengine tunao uelewa wa kutosha jinsi wizara ya elimu inavyofanya kazi, na chain command na nani wa kulaumiwa hapa.
hivi nchi hii lini mtakuwa wakweli? lini mtakuwa na akili ya kupima mambo bila kuegemea kamzizi mliojichagulia, ningekuona wa maana ungehoji ukweli wa kuwakutanisha watu wa upande mmoja tu huku wengine wakipewa taarifa tu.
Siku tukianza kutumia akili za Annuur nadhani mtafurahi sana, but news flash, hio siku haitokaa itokee. Watu walishavuka reasoning ya kiwango hicho kidogo karne kadha wa kadha zilizopita. Poleni/
 
Ilianza wakati wa Utawala wa Mwinyi. Hata uvaaji wa Hijabu ulipoanza. Hata hivo masomo hayo yalikuwa hayana nafasi yoyote kama sifa za kujiunga na University.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…