Ansbert Ngurumo: Bashiru aangukia pua kwa Meya Chifu Karumuna

Ansbert Ngurumo: Bashiru aangukia pua kwa Meya Chifu Karumuna

Kwani mtu kuendwa akachaguliwa ni chuki binafsi ama ndo demokrasia yenyewe, ama unataka wa kuteuliwa tu fafanua kidogo walau itanifikirisha kidogo
 
Duh....!

Huu utakuwa uzushi Dr Mpango aache kuhangaika na uchumi unaoyumba dunia nzima aanze kumrubuni Meya ahamie CCM?

Hizi ni siasa za kiwango cha " SIFURI"
Ni kwa vile unajifanya hujui kuwa CCM inageuza watu kuwa wajinga!
 
CCM wana siasa za kipumbavu sanaView attachment 1406917

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM wapende wasipende yafaa wasome alama za nyakati.
La kuvunda halina ubani. Yaweza kuwa ngumu sana kwao kumeza, lakini mvuto wa kweli kutoka moyoni hujengwa juu ya haki na sio kwa ghiliba, vitisho wala mabavu. Yule Bashiru wa zamani akiamua kuzinduka atalijua hilo.
Wenye njaa na tamaa kali wataendelea kupatikana na kuja huko kwa bidii sana, debe zima. ILA wakiishajaa kama ambavyo yazidi kudhihirika, watararuana na kutimuana wakishandania njaa za matumbo yao.
Bado kitambo kidogo tu mwisho watauona wenyewe hukohuko kwao. Amen
 
Meya amebakiza siku ngapi asiwe Meya tena halafu namfahamu hana chochote cha maana wakati mwingine tumieni akili. Kwa nini CCM wasimtafute mapema waje wamtafute siku za lala salama??
hana cha maana kwa maana gani? wewe ni mjinga hujui lala salama kwenye halmashauri michezo ambayo huwa inafanyika kwenye masuala ya fedha. Ujinga wa kutoelewa mambo ndio unawafanya msijue ni kwanini CCM dakika za lala salama inafanya mapinduzi haramu kwenye uongozi wa halmashauri. Wajinga ndio waliwao!
 
Yaani katibu Mkuu aanze kuhangaika na meya ambaye October 2020 anaenda kubwagwa
Kuna madiwani wawili walinunulia kwa ml2 huko pwani. Aliyeshiriki kupeleka pesa alikuwa afisa biashara mmoja kifutu. Mla rushwa aliyekubuhu
 
Lucifar ameweka kmbi yake Tz awamu hii, matokea yake yatakuwa mabaya sana kwa waliomkaribisha!
 
Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye majuzi alimpigia simu Meya wa Bukoba, Chifu Karumuna, akamwita kwa dharura aende Dodoma kwa mazungumzo ya kikazi. Manispaa ya Bukoba inaongozwa na CHADEMA. Iilikuwa hivi:

Chifu Karumuna akapokea simu toka Waziri Mpango, akaitwa Dodoma. Akaenda.

Kufika ofisi ya Waziri, akakutana na Mkuu wa Mkoa Kagera na Mkuu wa Wilaya Bukoba.

Wakaanza kumbembeleza kuwa ameitwa kupewa hela ya miradi ya Stendi mpya na Soko.

Walipoingia ndani wakamkuta Bashiru. Waziri Mpango akaanza. Tumetenga hela kwa ajili ya miradi muhimu ya Bukoba. Akamsifia Chifu jinsi alivyo mtu makini. Ndipo Bashiru akaanza kuwa Mh Rais ana imani kubwa na Chifu. Kwamba anamuomba akubali kuunga mkono juhudi.

Kwamba njia ya kuwa waziri ni nyeupe. Miradi hiyo mikubwa fedha tayari. Akiingia CCM, wote wanaotangaza nia watanyamazishwa mara moja. Balozi Khamisi Kagasheki atafukuzwa kwenye chama kwa sababu ni mpinzani. Chifu akadakia, sisi wapinzani hatumtambui kuwa ni mwenzetu. Bashiru akasema, “Balozi ni wa ACT.”

RC na DC wakapiga magoti mbele ya Chifu kumsihi aunge mkono juhudi. Bashiru akataka kupiga magoti Chifu akamzuia. Ndipo Chifu akawaambia kuwa hawezi kufanya hicho kitu. Akawaambia yeye ni mseminari na anaheshimu viapo. Akawapa ofa, kuwa yuko tayari aache siasa kuliko kuunga mkono juhudi.

Bashiru akasema Bukoba ni kwao na amehakikisha fedha inatengwa lakini sasa Chifu amewaangusha wana Bkb.

Mkutano ukavunjika. RC na DC wakachukia kweli.

Awali, katika maandalizi, walikuwa wameshirikisha wabunge weote wa CCM kutoka Kagera. Anna Tibaijuka wa Muleba Kusini na Diodorus Kamala wa Nkenge waligoma. Charles Mwijage wa Muleba Kaskazini hakuwepo Dodoma wakti Chifu anafika. Innocent Bashungwa wa Karagwe alishiriki mipangi lakini hakuhudhuria kikao cha Dodoma.

Msione watu wanajidai, msione wabunge na madiwani wa CHADEMA wanapukutika. Mipango inaanzia mbali.
Sasa haya yalishapita,tunataka mapya.
 
Back
Top Bottom