Anthony Diallo anazeeka vibaya

Anthony Diallo anazeeka vibaya

Hata huo msamaha alioomba ni kichekesho tu. Kwamba amekosea kwa kutoa mfano uliopita! kuwa na refference ya wakati uliopita, uliopo ama ujao si kosa, kinachoangaliwa ni content ya ulichokizungumza.
Sijui mh diallo aliwaza nini. alitakiwa kujua kwamba ndani ya CCM kunawatu waliomchukia magufuli lakini si wengi katika kiwango ambacho yeye alidhani angepata watu wakumuunga mkono ktk hoja zake hizo.
Lakini bado tu anakosa anayesema hayo kwa nini hakuachia nafasi yake ili tungeamini kabisa kua alimanisha
 
Nilidhani unaandika kama mtu huru kumbe mwana CCM sijapoteza muda wangu kusoma.
 
Ni hulka is CCM kuja na maandiko kama haya... Hampendi kuambiwa UKWELI...

Zanzibar kujiunga na OIC mlikana kabisaa na mkalifungia gazeti la Motomoto hadi leo

Hata Loriondo kuuzwa mlikana pia na gazeti la Motomoto likapigwa stop hadi leo...
 
Ni hulka is CCM kuja na maandiko kama haya... Hampendi kuambiwa UKWELI...

Zanzibar kujiunga na OIC mlikana kabisaa na mkalifungia gazeti la Motomoto hadi leo

Hata Loriondo kuuzwa mlikana pia na gazeti la Motomoto likapigwa stop hadi leo...
Kama Diallo angejivua cheo hicho kipindi cha kichaa na kusema hayo leo tungemuelewa.
Yaani anafanya kitu ambacho na yeye ni mshiriki
 
Wazee wengi sana wa CCM ni wanafiki sana ila wote wanajua kuwa tulikuwa na kiongozi mwehu na kichaa. Watafuteni akina Butiku na Wasira watawapa habari.
 
Wazee wengi sana wa CCM ni wanafiki sana ila wote wanajua kuwa tulikuwa na kiongozi mwehu na kichaa. Watafuteni akina Butiku na Wasira watawapa habari.
Na mimi naongezea hata huyo Diallo ni kichaa kwa nini hakuachia nafasi yake kipindi cha kichaa hivyo na yeye alikuwa au mpaka sasa ni kichaa
 
Wazee wengi sana wa CCM ni wanafiki sana ila wote wanajua kuwa tulikuwa na kiongozi mwehu na kichaa. Watafuteni akina Butiku na Wasira watawapa habari.
Na mimi naongezea hata huyo Diallo ni kichaa kwa nini hakuachia nafasi yake kipindi cha kichaa hivyo na yeye alikuwa au mpaka sasa ni kichaa
 
Humu utatukanwa na kudhihakiwa na walotumwa kuua legacy ya JPM, shujaa kalala usingizi wa milele lakini mashoga, wauza ngada, mafisadi na wazembe bado wanaweweseka, mwanasiasa anayetaka kufa kibudu kisiasa asimame jukwaani amdhihaki JPM kama anajiamini aone kitachomtokea.
 
The problem with CCM sycophants is that they don't want to be told the honest truth.

It is undisputed facts that the late JPM went astray in his leadership.

He always beguiled Tanzanians that he's the best leader & begged to be considered a God's messenger sent from heaven to lead Tanzanians something which is not.

I know CCM sycophants don't want to hear the truth but must be told.
 
Kama Diallo angejivua cheo hicho kipindi cha kichaa na kusema hayo leo tungemuelewa.
Yaani anafanya kitu ambacho na yeye ni mshiriki
Nani alikuwa na uwezo wa kuyasema haya wakati huo..!? Ya kurudisha maduka ya fedha za kigeni si ni sawa na haya..!? Kumrudishia Mbowe hela zake kuna tofauti gani na haya,,!? Alichosema Ndugai kuhusu bandari ya Bagamoyo si sawa na haya..!? RAIS aliposema KUTIBU MAJERAHA, ulielewa nini!? Acheni unafiki semeni UKWELI, maana utawaweka huru
 
Kwa bandiko hili mataga mjitafakari sana kama kweli mnaweza kuendelea kuendesha nchi..wakati wewe ukimshaangaa Anthony Diallo mimi nakushangaa wewe kwa kutokushangaa inakuaje mtu mwenye uozo wa kupitiliza bado anaendelea kutumikia nafasi za juu ndani ya chama

Chama chenu ndivyo kilivyo hawana watu mbadala tofauti na nyie. Mwenzako analia kwa sababu mmempunguzia kipande cha mkate na wewe endelea na kujiona mzalendo kisa unamtetea katibu wenu wa UVCCM.

Eti uzalendo wa katibu ni kumkosoa mtu anayesema ukweli kuhusu mataga!!. Kwa hiyo kwenu uzalendo ni kusifia serikali yenu?
 
Kaongea ukweli mtupu ila wamejaribu kumtekenya kaanza kuukana ukweli mara anamanisha wakati ujao.
Kwani uzee huwafanya hivi na wengine?
Wametekenya mbavu kaanza kuingiza mkia katikati ya miguu 😅😅😅!!! Aulize kilichomtokea Sumaye baada ya kujitia msaliti maniner!

Bila support ya CCM wakimuanzishia spana haitaisha miezi 6 star tv na redio free yatakuwa makazi ya popo!
 
Mpasuko ndani ya CCM is coming soon

Diallo amesema ukweli, jamaa alikuwa kiongozi muovu na katili. Sana sana tunawashauri muanze mchakato wa kumvua uanachama maana ni mchafu mwenzenu, na huo ni ushahidi kuwa huko kwenye Chama chenu hakuna uhuru wa kutoa maoni.
 
KWANGU MIMI #Yona IWE ANTHONY #DIALO AMEFANYA KOSA AU HAJAFANYA KOSA, ILA KUNA FUNZO KUBWA KWANGU NA NI FUNZO KWA VIONGOZI Naa Joseph #Yona

#DIALO ambaye mwaka 2015 alikuwa mjumbe wa vikao vya CCM, vilivyompitisha Mgombea Urais wa Chama hicho Dola Milele, mbaya zaidi #Dialo kama mjumbe akapitisha mwenye Faili na akakaa kimyaa.

#Dialo huyo huyo akiwa amempitisha mgombea huyo, akagundua media nyingi hazimmuliki na kumuandika mgombea wake huyo, akaamua kutumia Rasilimali zake za vyombo vya habari bila kujali hasara ya kibiashara akamtangaza mgombea huyo na akashinda Urais, kwa mujibu wa Dialo aliweka pembeni faili la Milembe akajitoa ufahamu akampambania.

Baada ya ushindi Rais akaapishwa akaanza kazi ya kushughulika pamoja na mengi kubwa ni Mafisadi, Wezi na wabadhirifu, lakini #Dialo yeye aliamini kwa kuwa amempitisha kwenye vikao, akatumia Media zake kumpamba, kwa kuwa ni Msukuma mwenzake, wametoka kanda moja na ana kinga ya uongozi akajua hataguswa, lakini Rais huyo akaamua kusimamia haki bila ubaguzi wa ukabila, ukanda, uchama na upendeleo wa Media akanyoosha Rula na #DIALO Akajikuta kanaswa, hapo ndo #Dialo akaanza kuirundika nyongo rohoni na Nyongo ikawa kali zaidi ya nyongo ya Kobra.

Hivyo #Dialo ametoa Nyongo, na nyongo ina mambo mengi usipojizuia unaweza kuongea na kuongeza Chumvi, pilipili, Nyanya, Bamia nk kwa muonekano #Dialo alikuwa na hasira asitegemee kuguswa na Swahiba wake, kumbe Swahiba ni mnyoosha rula haangalii kabila, Dini, Rangi, ukanda, Msaada wako nk.

#Funzo Nimejifunza kwenye haki nyoosha Rula, usiangalie mtu usoni.

Asanteni.
 
ANTONY DIALLO ANAZEEKA VIBAYA

Kwanza kabisa nianze kwa dhati ya moyo wangu kumpongeza katibu wetu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tanzania (UVCCM) ndugu yetu, na kaka yetu Kenani Labani Kihongosi kwa jinsi anavofanya kazi kwa weledi mkubwa kama kijana mwenye maono na anaonesha kwa namna gani ni kiongozi bora kabisa ndani ya jumuiya yetu kwa muda mfupi ametuonesha dira kama vijana wa UVCCM tunatakiwa kuenenda kwa namna gani.

Katibu Kenani Labani Kihongosi anafahamika kwa uimara wake na misimamo thabiti isiyoyumba hasa linapokuja swala la kutetea masilahi ya watanzania wote hii tumeona maeneo mengi alipokuwa mkuu wa wilaya ya Arusha katika utumishi wake wote alisimama na wananchi vilevile kusimama kama kiongozi wa umoja wa vijana wa CCM Tanzania ndo maana hata tumeshuhudia amethubutu kumpa onyo bila woga mwenyekiti wa CHADEMA F. A. Mbowe kuwa awakanye na kuwafundisha adabu vijana wake maana wanakosa heshima kwa kiongozi mkuu wa nchi kiufupi vijana wa mzee Mbowe wanavuka mipaka yao na kuona wanauwezo wa kuamua au kuropoka chochote kitakachowajia akilini mwao,

Lakini ni katibu wa UVCCM Taifa ambaye ameinuka na kukemea kauli mbovu na za kejeli zilizotolewa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza ndugu Antony Diallo katika moja ya mahojiano yake na kituo cha runinga cha Star TV hapo Nyuma, kauli za mwenyekiti huyo zimekikashifu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Chama ambacho yeye mwenyewe ni kiongozi wake tena wa ngazi kubwa kabisa ya mkoa. Hapo Kenani Labani Kihongosi kama kijana wa nchi hii na jasiri, kijana mwenye uzalendo haswa ameshindwa kuvumilia nakuamua kutoka hadharani na kutoa onyo kali kwa waziri huyo wa zamani aliyehudumu zaidi ya wizara mbili ambaye ni kiongozi wa CCM mkoa wa Mwanza

Hivyo nimtie shime katibu wetu wa UVCCM Tanzania kwamba asonge mbele akaze buti sisi vijana tunamuunga mkono kwa asilimia zote tutamlinda, tutamshauli, tutamkosoa, lakini zaidi tutamtetea kwa nguvu zetu zote na kwa maarifa yetu yote kwasababu yeye ni jasiri mwongoza njia na tumeona kazi yake ameanza vizuri na kauli mbiu yake maridhawa kabisa ya Mtumishi wa wote hivyo hata mimi naungana na katibu wangu na kusapoti onyo lake kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza kwamba aache mara moja hicho anachokisema maana anakikosea Chama na serikali ambayo ameitumikia na bado anaisimamia kwa cheo chake

Katika vitu ambavyo vimeshangaza wengi sana ni hiki kituko alichokifanya mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza bwana Antony Diallo, ambaye kimsingi yeye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa lakini zaidi yeye ni mjumbe wa NEC ya CCM kwa cheo chake. Antony Diallo inawezekana uzee unamnyemelea kwa kasi tunaweza kusema hivo labda pengine ana truck record mbaya ya biashara zake ndo maana anaonesha chuki ya moja kwa moja kwa serikali ya awamu iliyopita, hebu tuangalia mambo yake kadhaa huko nyuma yanayozalisha chuki kubwa dhidi ya viongozi wa CCM

Antony Diallo akiwa hivo hivo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza lakini ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Sahara Media Group (SMG) inayomiliki kituo cha televisheni cha Star TV, kituo cha radio cha Radio Free Afrika (RFA) na kituo cha radio cha Kiss FM, na king'amuzi cha Continental decoder katika utendaji wake wa hizo kampuni mwaka wa 2017 alikutwa na makosa makubwa mawili ambayo yalimwondolea kabisa Legacy yake kama kiongozi wa CCM ndani ya mkoa wa Mwanza ambao ni moja kati ya Majiji makubwa ndani ya nchi yetu na Afrika Mashariki kwa ujumla lakini makosa hayo yalimshushia heshima yeye kama mkurugenzi mtendaji wa vituo vikubwa vya kurusha matangazo ndani ya Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

Antony Diallo alikabiliwa na kosa la ulimbikizaji wa kodi kutoka katika mamlaka za mapato Tanzania (TRA) kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 4.5 na vituo vyake vikafungiwa ndo maana leo anaanza kutoa maneno ya chuki dhidi ya serikali ya Chama anachokiongoza yeye mwenyewe (CCM) lakini bado serikali anayoikejeli leo kupitia TRA wakampunguzia masharti wakamwambia ili vituo vyake vifunguliwe alipe Billion 2 kutoka katika zile 4.5 anazodaiwa na akafanya hivyo na mambo yakaendelea vizuri kwake. Hivyo unaweza ukaona ukosefu wa uadilifu katika uongozi wa Antony Diallo ulisababisha hasara kwa Taifa na kupoteza mapato yake mengi sana ambayo alikuwa anayakalia ndani ya taasisi anazozisimamia pale Mwanza.

Pia ni huyu Antony Diallo aliburuzwa katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza kwa kushindwa kulipa mishahara wafanyakazi wake 20 kwa muda wa miezi 6 mfululizo na alikuwa anadaiwa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa wafanyakazi hao, halafu leo anasimama kuwasema vibaya viongozi wa Serikali baada ya serikali kukagua madudu yake ambayo alikuwa anajificha kwa mwamvuli wa kuwa mwenyekiti wa CCM huku akifanya ubadhilifu mkubwa na kuingizia hasara Serikali na kukwamisha shughuli za maendeleo kwa watanzania. Atuachie Chama Chetu kama anaona amechoka milango ipo wazi aende huko akachague viongozi anaowafahamu yeye lakini hatutakubali kejeli kama hizi kwa Serikali yetu tutasimama imara na kueleza kwanini anaichukia Serikali huku sababu kubwa ikiwa ni kuweka mazoea ya kukwepa kodi alipobanwa ndo anaanza kuona serikali ya CCM na viongozi wake ni wabaya kwake.

Kwa nafasi ya Antony Diallo kama mwenyekiti wa CCM mkoa yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa hivyo ana maamuzi makubwa ya kuchagua viongozi kama aliyaona hayo kwanini hakufunguka tangu awali? kitu anachokifanya kwasasa ni uchochezi usiokuwa na faida ndani na nje ya CCM.

Kiongozi yoyote yeye ni mbeba maono sasa inapotokea anakiuka taratibu ni lazima tumueleze ukweli kuwa njia anayopita si sahihi. Antony Diallo bado alishutumiwa kutokupeleka stahiki za wafanyakazi wake katika mifuko ya hifadhi za kijamii PPF/NSSF huko alipobanwa tayari akaanza kuiona serikali kama haipo upande wake kwasababu inafichua maovu yake na kuyaweka wazi na hapo ndipo chuki yake na viongozi wa serikali ilipoanzia na kuota ndani ya moyo wake.

Antony Diallo huyu huyu amewahi kuwa waziri wa Maji na umwagiliaji ni nini alikifanya katika wizara hiyo pia akaja kuwa waziri wa Maliasili na Utalii hivi hata leo najua kabisa hapa kati yenu mnae soma andiko hili kuna uwezekano mkubwa ulikuwa hufahamu kama huyo Diallo alishawahi kuwa waziri katika nchi yetu hii

Sasa leo hii anaanza kuongea mambo yanayokikashifu Chama chetu kana kwamba anaongea maswala ya wafanyakazi wake, amesahau kabisa kuwa CCM ni taasisi kubwa inayotoa viongozi wakuu wa nchi ambao wanaongoza watanzania zaidi ya milioni 60 halafu leo anaanza kuzungumza vitu ambavyo vinaleta mkanganyiko mkubwa na kejeli nyingi kwa viongozi wetu hatutakubali yeye kama anazeeka basi azeeke kwa amani atuache akae kwa kutulia asitake kuanzisha malumbano yasiyokuwa na tija ndani ya CCM yetu.

Uongozi ni dhamana huwezi kujificha ndani ya CCM kwa kufanya mambo yako mabaya kwa jamii halafu yanapokuja kufichuka basi unaanza kuiona Serikali mbaya inaongozwa na viongozi wa tofauti nadhani Mwenyekiti huyu Diallo kuna vitu alitarajia atavipata kutoka katika awamu iliyopita lakini baada ya kuvikosa ndo mambo yalipoharibikia hapo sasa aache asianze kuamsha tena haya yamepita viongozi wetu ambao wamekwisha kufanya kazi katika taifa hili wanapaswa kuheshimiwa na siyo kukurupuka na kuanza kutoa kejeli ambazo kwanza jamii inayokuzunguka inakuona kama umechanganyikiwa kwasababu unaanza kusema kitu ambacho wewe mwenyewe umekifanyia maamuzi huyu mwenyekiti katukosea sana ingawa ni mtazamo wake lakini yeye kama kiongozi amevuka mipaka jambo ambalo CCM wanatakiwa kuliangalia mara mbili.

Ahsante.
Vijana acheni kujipendekeza,mtatendwa vibaya.
Muda uliotumia kuandika hii makala,ungekuwa umeshajiingizia kipato halali kizuri tu.

Mwanzo 3 : 17 - 19
"17. Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;
18 .michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
19.kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi".
 
Back
Top Bottom