Anthony Joshua afanikiwa kumtwanga Wladimir Klitschko katika pambano la uzito wa juu

Anthony Joshua afanikiwa kumtwanga Wladimir Klitschko katika pambano la uzito wa juu

Ni kweli klitschko hakuamini maana dogo alishapotea ila came back yake si mchezo ana punch nzito sana sipati picha akiendelea na moto huo na kupunguza mapungufu yake kwenye defencing sijui kama kuna mtu atamgusa
 
Hvi mshindi wa pambano kapata kiasi gani cha pesa?
 
Sijawahi kufurahia pambano la heavy weight kama leo toka enzi za kina Tyson, Lewis. Dogo anajua sana, ana moyo na ata improve sana kwani hili ni pambano lake la 19. Ile uppercut daah!!!
 
hivi akishaslimu inawasaidia nn haswa?? kwahy ht tyson walimconvice hao hao au
ni fahari kwao kuwasilimisha watu maarufu. Ni kama mashindano flani hivi. Pia wamejaribu sana kwa Usain bolt kawachomolea. Wakamuomba basi akishinda asujudu hili kuwafurahisha 2012 Olympic London aliposhinda alisujudu na kuamka nakufanya alama ya msalaba ya dini yake
 
Tyson Fury ana skillz sana.Fury vs AJ patachimbika.

Ila pia kuna Deontay Wilder.Naye yupo vzuri.
Fury sio mkali kivile anaweza chapwa na AJ, alizichapa na Klitschko akasinda kwa UD while AJ kamshinda kwa KO.
Fury ana 25 games kashinda 18 kwa KO na AJ ana 19 KO.

Wilder huyo ni namba chafu ana 38 games 37 KO 1 UD na 18ni KO Za 1st round. Alitaka kumua mtu ulingoni huyo.
 
He has put up a good fight.... hakukata tamaa round ya 5 , 6 na 7
 
Nimefurahi kijana mwenzangu,Muafrica mwenzangu umeshinda pambano "gumu" kwani huyo mzungu tunamjua,pambano ambalo kila mtu na hata sisi weusi wenzio tulijua unakalishwa hasa pale ulipolegezwa Na makombora mazito ya yule mzungu.
Kiufupi unajua kuzichapa ila ombi langu kama unajua kiswahili Mimi ndugu yako katika "Ngozi" naomba hebu Nenda kalifanyie kazi swala la "pumzi" usije ukatutia aibu ..pumzi huna kabisa Mkuu.
Ww mwenyewe unajua kwamba sifa yetu africa imebaki ktk ngumi tu kutengeneza "missiles" hatujajaaliwa bado.Yaani pambano la Leo kama ungekutana Na mtu kama Tyson, Haya maneno yako "Can I go home" ungeenda kuyatamkia hospitalini St Thomas.

Alichoka sana round ya 5 ile nadhani... ila pia kufikia round ya 11 dhidi ya mtu mwenye uzoefu kiasi kile sio utani.
 
Kumbukeni Wradimil keshakuwa mzee ni 41 now. Joshua only 27 . Kiuanamichezo Joshua alitakiwa amkalishe mapema sana. Kwamtazamo wangu Joshua ana mengi sana ya ku improve na muda anao bado. Hongera zake.
 
Kumbukeni Wradimil keshakuwa mzee ni 41 now. Joshua only 27 . Kiuanamichezo Joshua alitakiwa amkalishe mapema sana. Kwamtazamo wangu Joshua ana mengi sana ya ku improve na muda anao bado. Hongera zake.
Stamina bado ni changamoto sana kwa Joshua.Pumzi yake inakata mapema.
Alafu misuli yake ni mikubwa sana inamfanya awe mzito sana.
 
Sijawahi kufurahia pambano la heavy weight kama leo toka enzi za kina Tyson, Lewis. Dogo anajua sana, ana moyo na ata improve sana kwani hili ni pambano lake la 19. Ile uppercut daah!!!
Inaitwa chapa kidevu ile,nilikua nacheki pambano huku natetemeka, maana ilikua kama el classico flani hivi. Sitaisahau round ya 5 maana Joshua alishapotea.
 
hivi akishaslimu inawasaidia nn haswa?? kwahy ht tyson walimconvice hao hao au
Ah...mambo ya dini hya ya nn tena hmu? Tumejumuika pamoja hp kumpongeza kijana mwenzetu Anthony Joshua ni muislam usichachawe na jina ni km Paul Pogba tu so what?
 
Huyo mwingereza mwenye asili ya nigeria hataree. Naskia waarabu wanamfuata fuata na kumuhonga asilimu lakini jamaa kawachomolea
Mi nakereka sana na watu mnaoleta udini udini hp tunapeleka peleka muda wko walofurahi na wpo walohuzunika pia mambo ya dini ya nn tena? Anthony Joshua ni muislam najua utabisha sababu ya jina Paul Pogba pia muislam hya umefurahi eeeee!
 
Hata Mimi na majaji wengine tumeona hivo ila mchizi sijui kawaje round 11, yaani kapigwa kama kapuliziwa dawa,. Yaani kammudu round zote ila tu ya 11, afu dogo naye nafanya kama marehemu Muhammad Alli ,michezo ya kumtegea opponent
Jamani lazima tukumbuke ile ni heavyweight.
Si mchezo wa kitoto.

Mie nampongeza sana AJ kwa skills zake. Kama utafuatilia vizuri, AJ ana ngumi nzito sana na anazipeleka nyingi kwa haraka sana kiasi kwamba hata ukiweka guard haisaidii.

Alichokifanya AJ baada ya kwenda chini, alijivuta hadi kengere. Baada ya hapo alikua mpole akivuta pumzi wakati klitschko alikua anatafuta the best punch amalize mchezo. Dogo akawa anamuharibia target.

Baada ya kupata pumzi dogo akajitoa muhanga maana angesubiri hadi round ya mwisho points zingembeba klitschko, kwahiyo klitschko akijua ile knock down bado mmempoza dogo hawezi tena makeke, dogo akamstukiza. Kilichomaliza pambano na hadi mnamuona klitschko alilainika ni ile uppercut ya mwanzo ambayo mtu mzima alielewa kabisa. Pia dkk zilikua bado nyingi kufikia kengere hivyo hakupata muda wa kukaa sawa na dogo akajitoa muhanga zaidi kwa kuendelea kumnyeshea za kutosha hadi anaondoka mara ya pili, na ya tatu kukosa refa kuingia kati basi angedondoka vibaya zaidi ya kuchanwachanwa kabisa.

Bado nampongeza AJ....kajitahidi sana sana na anastahili ushindi ule.
 
Hivi wale kina matumla na wenzie utaskia wameshinda ubingwa wa dunia... Dunia ipi eti? Au dunia tambala bovu[emoji15]
Hawana tofauti na mapropesa wetu....wote wanakimbilia siasa badala ya kuzalisha vitu muhimu kwa taifa lao. Hata bajaj tu hawawezi.
 
Inaitwa chapa kidevu ile,nilikua nacheki pambano huku natetemeka, maana ilikua kama el classico flani hivi. Sitaisahau round ya 5 maana Joshua alishapotea.
Haunishindi mie. Nilikua natetemeka mbaya....round ya 11 nataka kusimama nishangilie nikajikuta kumbe nilipanda juu ya kabati, hata sijui nilifikaje Ikabidi niitishe stuli na kiti ili niweze kushuka. Waifu ananishangaa nilipanda kutafuta nini na nilipandaje maana nilikua peke yangu naangalia na si kwamba watu walijaa wakaniziba nisione screen.

Haya mambo tuyaache tu kama yalivyo.
 
kitambo nikiw dogo kuna pambano nililifumania liko mwishoni ila nachokumbuka yule boxa alikuwa ni black alikuwa na kasi ya ajabu halafu mikono yake ilikuwa muda wote iko chini,yani haweki guard ila anatia ngumi mbaya,,sikuwah kumfahamu asee,mwenye kumjua tafadhali
sio Roy Jones Jr huyu.
 
Back
Top Bottom